Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

jamani msijifariji? nani anaweza kuwa mgombea binafsi na kushinda tanzania?????????? hizi sio zile wanazoita ndoto za mchana?????????? wananchi wa tanzania uelewa wao ni mdogo sana hatujafikia level hiyo wakuu, angalia tu kamati ya mwakyembe na kuchonga koooooote kule kumbe hakuna kitu!!!!!!!!!!! tuendelee kujenga demokrasia taratibu, tutafika tu..............

Kama ni ndoto mkuu waambie Chama Cha Majambazi waruhusu uone moto.
 
Masikini yule jamaa aliyejitangaza hapa jana kama mgombea binafsi wa Moshi Vijijini,sijui itakuwaje kwake..itabidi atafute tu chama mapema.
 
Masikini yule jamaa aliyejitangaza hapa jana kama mgombea binafsi wa Moshi Vijijini,sijui itakuwaje kwake..itabidi atafute tu chama mapema.

pole zake, halafu inaonekana hafai hata kuwa mwanasiasa kwani kashindwa kusoma alama nyepesi hivi ya wakati! mmmmmhh
 
Tofauti ya sasa na hiyo 2015 ni nini kulindana?


hata hiyo 2015 ni uwezekano wa kuzungumzwa tu, utekelezaji wake unaweza kuchukua hata miaka 50 ijayo.

hapa usiwalaumu CCM, tujilaumu wananchi kwa kasi ya konokono katika kuielewa na kuizoea demokrasia ya vyama vingi.
 
Kamanda,

Mimi ninavyoona Marmo kaingilia shughuri za mahakama kwa nini amezungumzia hiyo kesi bungeni wakati anajua bado iko mahakamani jamani kuna mwanasheria yeyote humu au anayejua sheria zetu zinasemaje kuhusu hilo atusaidie.
 
Akili Kichwani,

Wewe ni kichaa usiye na nafuu. Ungekuwa na nafuu ungegundua kwamba kuna watu wana uwezo kuliko wewe.

Unaamini bado uelewa wa wa-TZ ni mdogo kiasi hicho? Bado unaamini wabunge hushinda kwa sababu ya uanachama wa CCM?

Kwa nini malawi iliweza kuwa na Rais asiye na chama?
Kwa nini Museveni aliweza kutawala Uganda bila chama cha siasa?
Miaka ya sitini, Salwat alishinda ubunge bila chama cha siasa.

Kama hayo yamewezekana kwa nini wewe bila chama usiweze kuwa kiongozi.

Energize your cerebral!

Angalia maamuzi ya majaji haya ktk attachment.
 

Attachments

hata hiyo 2015 ni uwezekano wa kuzungumzwa tu, utekelezaji wake unaweza kuchukua hata miaka 50 ijayo.

hapa usiwalaumu CCM, tujilaumu wananchi kwa kasi ya konokono katika kuielewa na kuizoea demokrasia ya vyama vingi................


Si bure?
 
nilishatangaza hapa kugombea moshi vijijini kama mgombea binafsi nitafanya hivyo wakati wa kuchukua fomu, nitaichukua tume ya uchaguzi, na hakuna wa kunizuia kwa kuwa mahakama imeshaamua huo mchakacho wa kubadilisha katiba watauleta wenyewe mahakamani pindi tutakapoanza kukurupushana
 
nilishatangaza hapa kugombea moshi vijijini kama mgombea binafsi nitafanya hivyo wakati wa kuchukua fomu, nitaichukua tume ya uchaguzi, na hakuna wa kunizuia kwa kuwa mahakama imeshaamua huo mchakacho wa kubadilisha katiba watauleta wenyewe mahakamani pindi tutakapoanza kukurupushana

hizo bangi sasa mkuu, halafu ulishindwa nini kusense mapema kuwa kitu kama hicho mwaka huu ni ndoto za alinacha?........................

pole sana..........
 
Mahakama ya Rufani itakapoendelea na kesi hii itatoa sentensi ambayo itamfanya Marmo ajisikie vibaya. Alichofanya Marmo ni kuijibu mahakama; kwani mahakama imesema uamuzi wa Mahakama Kuu tayari unaendelea kuwepo na wagombea huru wanaruhusiwa 2010. Marmo hawezi na hana mamlaka ya kusema kuwa haiwezekani. Hakuna mabadiliko ya Katiba yanayohitajika kuruhusu wagombea huru.

Wanachotakiwa ni kubadilisha sheria yao tu kwani vifungu vile vinavyotaka mtu awe mwanachama wa chama cha siasa agombee vimeshatangazwa kuwa vimetenguka na havina nguvu.
 
Mgombea binafsi hawezi kuruhusiwa kushiriki uchaguzi kabla ya modus operand hazijatungwa na kuwekwa, pia kuna some constitutional ammendments zinahitajika kabla ya kuanza rasmi utekelezaji.

Hata kama muda uliopo unatosha, madam serikali (mtekelezaji) hajaridhia, vitapatikana visingizio na ikibidi agizo jinine la mahakama litatafutwa na litapatikana bila shida. Believe me!!!!!!!!!

After all mtikila?

Sasa si mnaniona mie mwendawazimu, nyie subirini tu mtaona
 
Chama Cha Majambazi hawawezi kukubali mgombea binafsi kwa sababu wakifanya hivyo wanafahamu tonge limeshatoka kinywani.

Mgombea binafsi ni sawa na "Concentrated Oil of Vitriol" on flesh kwa Chama Cha Mapinduzi. CC na NEC za CCM zitakuwa hazina nguvu tena ya kukata majina ya wagombea kidectator kwani kwa kufanya hivyo ni kumwambia mtu agombee kivyakevyake na akishinda (Kama kweli tume ya uchaguzi itakuwa huru tofauti na sasa) itakuwa ngumu kumshawishi ku-rubber stamp kwani atakuwa anawakilisha wananchi waliomchagua na si CCM iliyompitisha kugombea.

Huu ni mwanzo tu, kama kweli nchi inaendeshwa kisheria basi mgombea binafsi ni muhimu na katiba inatoa uhuru kwa raia yoyote mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea mwenye akili timamu kuchagua au kuchaguliwa katika nafasi za uongozi wa nchi kwa mujibu wa katiba ya nchi. Hakuna sehemu iliyosema ni lazima watanzania wote wawe wanachama wa chama cha siasa.
 
Akili Kichwani,

AK
Sijakuona unakuja na hoja zaidi ya kupayuka obvious mara ndoto za alinacha tuambie hizo ndoto zitatokana na sababu zipi kama ni mahakama kuu au mahakama ya rufaa sema kama ni serikali kuzuia kwa mabavu sema unaposhupalia obvious obvious bila kutoa sababu utaonekana kichaa.
 
AK
Sijakuona unakuja na hoja zaidi ya kupayuka obvious mara ndoto za alinacha tuambie hizo ndoto zitatokana na sababu zipi kama ni mahakama kuu au mahakama ya rufaa sema kama ni serikali kuzuia kwa mabavu sema unaposhupalia obvious obvious bila kutoa sababu utaonekana kichaa

actually ninasuume kuwa tulio wengi tuaweza kuunganisha na kupata mnyororo. serikali ndiye mtekelezaji na hapendi kutekeleza, mahakam inaonyesha kuwa haina pingamizi kwa mujibu wa sheria. seria zenyewe zinatungwa na kupitiswa na kutekelezwa na Serikali.

bunge halina nguvu, linatumiwa ana serikali, mahakama vilevile ni kachombo (tena dhaifu zaidi ya bunge) ka serikali, kila siku kanalia njaaa inauma, kanaililia serikali baba yake. jaji ramadhani anastaafu mwaka huu, atatamani akumbukwe japo kwenye ka-tume fulani aendelee kusaini bahasha akisubiri kumalizana na Mola wake. Sasa katika situation kama hii, unatarajia nini hapo Mkuu.
 
there will be a showdown between the government and the courts as I had prayed for. Subirini msikie Majaji wote wa Mahakama ya Rufani na Kuu wakijiuzulu kama ilivyotokea Pakistani.. Kutakuwa na wagombea huru mwaka huu.
 
Kuna baadhi ya mambo wakubwa wetu wanayafanya, yatawaongezea majuto miaka ile inayokuja ambayo kwa kweli watahitaji wapate mapumziko ya amani. They forget that we move in circles.What if next turn would come with something different?Politics is not gambling.
Anyway, without any prejudice, I believe we do everything at our own peril.
 
Back
Top Bottom