Wahitimu vyuo vikuu na sekta zinginezo hawana ajira, na wachache wanaajiliwa kwa upendeleo na hira.
Wafanyakazi hawakupandishwa mishahara wala kupewa nyongeza ya mwaka iliyopo kisheria kwa miaka5.Wametukanwa na kudhalilishwa hadharani.
Wakulima wamepolwa mazao yao, bei ya mazao imeshuka na wakulima kutishiwa kupigwa wao na Shangazi zao.
Wafanya biashara wamepokwa Mali zao, biashara zinasua sua na wafanya biashara wengine wameswekwa rumande mpka sasa na hakuna hukumu iliyotolewa kama kweli ni waharifu miaka5 mtu yupo mahabusu hakuna ushahidi lakini amefungwa kibabe.
Raia wameuwa, kupotezwa na kuteswa kikatili.
Ni mtanzania wa aina gani ambaye hana Akili atachagua Utopolo huu wa CCM.
Safari hii tunamchagua Mtanzania mwenzetu anaye jali utu wetu, tamaduni zetu, haki zetu na Uhuru wetu.
Hatuwezi kumchagua mtu anaye jali madaraja au reli kuliko utu wetu na Uhuru wetu.
Makaburu wa Afrika kusini walijenga barabara, madaraja ya juu, reli tena bora kuliko hivi anavyo jenga Magufuli.Lakini Tanzania tulikuwa mstari wa mbele kuwasaidia Afrika Kusini kupigania haki yao ya Uhuru.
Tuliamini kuwa Uhuru wa mtu unazidi thamani ya vitu. Hata wakoloni hapa Tanganyika walijenga reli, shule, barabara na mengine mengi mazuri. Lakini tuliwaondoa kwa kuwa hawakutupa uhuru wetu. Hatuwezi kurudishwa utumwani tena mara ya pili.
Maendeleo hayana vyamaa.