Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

Sijaelewa swali lako. Unamaanisha kuvunjiwa nyumba au kukosa makazi ili eneo lipangwe???

Kama ni kuvunjiwa nyumba ndio, Nipo tayari.

Kama kukosa makazi hapo ndo sipo tayari!! Ninamaanisha nini kusema hivi???
Katika kutengeneza mipango miji na makazi bora, hili jambo linaweza kufanywa kwa hatua na likafanikiwa hakika!!! Litafanikiwaje???

Kama nchi tuna maeneo ambayo hayajaendelezwa, tunaweza kusema tunajenga nyumba za wakazi 5000- 10000 kwenye eneo ambalo likizo wazi tuliloamua kuliendeleza na tukishamaliza tunawahamishia Mf. Wakazi wa tandale kwenye eneo hilo. Tukiwahamishia tunachofanya sasa ni kupabomoa pale tandale tulipowatoa watu na kupajenga kisasa. Tukimaliza kupajenga hapo tunawahamishia wengine ambao tutaenda kupabomoa kwao ili kupajenga na kupapanga vizuri.

Tatizo CCM mmeishiwa watu wenye akili mmeishia kuwa na watu wasio na akili wanaowaza matumbo yao.
Haya mambo ni CHADEMA tu wanaweza kuyafanya kwa ufanisi
Hata miji midogo inayoanza kukua hawapimi viwanja, badala yake watu wanauziana viwanja pasipo kupimwa , unategemea nini kama siyo squatters zingine? Yaani kweli bongo under this system ni bahati mbaya.
 
Kuna tatizo mahali...mitandaoni cdm kinatoa mwanga na matumaini ya ushindi.

Kwenye kura sasa! Kila mtu na analolijua moyoni mwake.
Sijui upinzani unafeli wapi.
Ndo maana katiba yetu haiwezi kubadilishwa bila damu kumwagika maana ccm inapendwa sana
 
Uchaguzi hausimamiwi na rais bali tume ya uchaguzi, anaahidi yeye kama nani wakati tunajua fika kuwa yeye ndio huwa anaagiza box la kura linajisiwe?

Hakuna uwezekano wowote wa ccm kushinda hata kama itashinda kwa zaidi ya 60%. Na hata hizo 60% ccm itafikisha kwa sababu tume sio huru, na kila taasisi ya nchi hii inadhani ina wajibu wa kuibeba ccm itangazwe washindi fullstop.
Kwani kura zikipigwa hazihasabiwi? Wakala wako anashuhudia kura ikitumbukizwa, anashuhudia uhesabuji na anapewa nakala ya fomu ya matokeo. Mnaweza kujumlisha na kulinganisha na kilichotangazwa. Katika dunia ya leo usipojitahidi kujenga uwezo wa kufikiri critically na badala yake ukaruhusu kuongozwa na mihemuko utapata taabu sana. Wewe endelea kuamini unaibiwa lakini mradi usichezee amani.
 
Wahitimu vyuo vikuu na sekta zinginezo hawana ajira, na wachache wanaajiliwa kwa upendeleo na hira.

Wafanyakazi hawakupandishwa mishahara wala kupewa nyongeza ya mwaka iliyopo kisheria kwa miaka5.Wametukanwa na kudhalilishwa hadharani.

Wakulima wamepolwa mazao yao, bei ya mazao imeshuka na wakulima kutishiwa kupigwa wao na Shangazi zao.

Wafanya biashara wamepokwa Mali zao, biashara zinasua sua na wafanya biashara wengine wameswekwa rumande mpka sasa na hakuna hukumu iliyotolewa kama kweli ni waharifu miaka5 mtu yupo mahabusu hakuna ushahidi lakini amefungwa kibabe.

Raia wameuwa, kupotezwa na kuteswa kikatili.

Ni mtanzania wa aina gani ambaye hana Akili atachagua Utopolo huu wa CCM.

Safari hii tunamchagua Mtanzania mwenzetu anaye jali utu wetu, tamaduni zetu, haki zetu na Uhuru wetu.

Hatuwezi kumchagua mtu anaye jali madaraja au reli kuliko utu wetu na Uhuru wetu.

Makaburu wa Afrika kusini walijenga barabara, madaraja ya juu, reli tena bora kuliko hivi anavyo jenga Magufuli.Lakini Tanzania tulikuwa mstari wa mbele kuwasaidia Afrika Kusini kupigania haki yao ya Uhuru.

Tuliamini kuwa Uhuru wa mtu unazidi thamani ya vitu. Hata wakoloni hapa Tanganyika walijenga reli, shule, barabara na mengine mengi mazuri. Lakini tuliwaondoa kwa kuwa hawakutupa uhuru wetu. Hatuwezi kurudishwa utumwani tena mara ya pili.

Maendeleo hayana vyamaa.
 
Hata miji midogo inayoanza kukua hawapimi viwanja, badala yake watu wanauziana viwanja pasipo kupimwa , unategemea nini kama siyo squatters zingine? Yaani kweli bongo under this system ni bahati mbaya.
Kuna sababu 1000 za kuiondoa CCM madarakani mwaka huu ndugu. Lissu ndo jibu
 
Hata miji midogo inayoanza kukua hawapimi viwanja, badala yake watu wanauziana viwanja pasipo kupimwa , unategemea nini kama siyo squatters zingine? Yaani kweli bongo under this system ni bahati mbaya.
Hivyo viwanja unavyotaka vipimwe ni mashamba ya watu ndimo wanapata riziki zao na ndio chakula unachokula kinazalishwa. Matumizi ya ardhi sio kwa ajili ya kitu kimoja tu.
 
Niko area D watu wabugujika machozi ya furaha kwa kutaka kumuona Mh, Lissu ..aaah Magufuli yuko ICU hawezi kutoboa hata mshindi wa tatu hataingia ,nadhani hii coalition yake na Tlp ndo itamsaidia kuingia top 5
Cha kufanya ni kuhakikisha tume inatenda haki.
 
Pamoja na maendeleo aliyoyaleta,Kaburu afrika kusini haikua nchi yake, ndo maana wazawa walikua na sababu ya msingi ya kupigania uhuru wa kujitawala na kupinga ubaguzi wa rangi. Sasa unataka hapa Tanzania Mimi nipinge nini labda? Tunajitawala wenyewe na maendeleo yanafanywa nasisi wenyewe.

Hujui unaloongea, hao makuburu wako huko Afrika kusini miaka na miaka ndio maana weusi hawakuwa wanapigania uhuru, bali kupambana na ubaguzi wa rangi. Nitajie baada ya ubaguzi wa rangi kuisha, kuna mzungu yoyote aliondoka kama wakoloni walivyoondoka hapa kwetu baada ya uhuru?

Ww hapa Tanzania unapinga upinzani maana unajua siku ccm ikitoka madarakani, ndio itakuwa mwisho wa kula mema ya nchi hii bila kuvuja jasho. Ndio maana unatumika kunajisi chaguzi za nchi hii, na kutumikia kundi la watu wasiojulikana, ili ccm iendelee kukaa madarakani kwa shuruti na vitisho bila ridhaa ya wananchi.
 
Imekuingia hiyo naona kinena kina nepa nepa tuu!! Ni Lissu pombe mwisho kaunta.
Tukana mengine tena!

Maana unavyozidi kutukana ndio mafuriko ya kumsindikiza Lisu kuchukua form yanaongezeka na kura kwa Lisu za mng'oa jiwe oktoba zinaongezeka!

Ni mafuriko dodoma!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
  • Thanks
Reactions: nao
Kutoka maeneo mbalimbali kwenye viunga vya mji wa Dodoma, Tundu Lissu leo anachukua Fomu ya Urais.

===



Tundu Lissu leo kwa Mara ya kwanza anarejea katika mji wa Dodoma akienda kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea Urais. Ikumbukwe Tundu Lissu mara ya mwisho kuondoka katika mkoa huu ni baada ya kupigwa risasi.

Fuatilia baadhi ya matukio na picha mbalimbali za tukio hilo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA Tundu Lissu akiwa amewasili katika Ofisi za CHADEMA Kanda ya Kati zilizopo jijini Dodoma na kupokelewa na viongozi mbalinbali wa Chama, wanachama, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA, kabla ya kuelekea Ofisi za Tume ya Uchaguzi kuchukua fomu, leo Jumamosi 08/08/2020.

====

TUNDU LISSU AFIKA OFISI ZA NEC KUCHUKUA FOMU YA UTEUZI

View attachment 1530861
View attachment 1530862
View attachment 1530863

Mgombea Urais Tanzania kupitia Chama cha CHADEMA, Tundu Lissu amefika katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu ya Uteuzi ya kugombea Urais

Lissu amefika katika Ofisi hizo na Mgombea Mwenza Salum Mwalim huku wakiwa wamesindikizwa na Wanachama wengine. Wamekabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage

Uchukuaji fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza Agosti 5 hadi 25,2020.

Lissu amechukua fomu, wamezihakiki na kujiridhisha kisha wameondoka katika Ofis za NEC ili kuendelea na taratibu nyingine za kichama.

#JamiiForums #Siasa #JFSiasa #Uchaguzi2020

WAANGALIE VIZURI HIYO FOMU NA WAANDIKISHIENE HADI IDADI YA KURASA NA RANGI YA FOMU, HAO JAMAA WA NEC HAWACHELEWI KUJA KUSEMA LISSU AMERUDISHA FOMU FEKI KWA KUWA HAINA UKURASA WA 3 NA IMEGONGWA MUHURI UNAOONYESHA YUPO UBELGIJI. MARA OOOH FOMU ZA NEC TULIZOMPA ZILIKUWA NA RANGI ZA TAIFAILA HII ALIYORUDISHA HAINA. USHINDI WA CCM HUWA NI MKUBWA NJE YA BOX LA KURA. WANA MSEMO WAO KUWA NDANI YA BOX LA KURA HAKIJULIKANI KILICHOMO. TUKIJUACHO NI KILE TUNACHOKIONA NJE. KUWENI MAKINI SANA NA RAFU ZA CCM NJE YA SANDUKU LA KURA. YULE MZEE HAPENDI USHINDANI KABISA.

NAOMBA WALE WALIOKUWA WANAOMBA KUANDAA MDAHALO KATI YA MAGU NA LOWASSA SASA RUKSA WAANDAE KATI YA MAGU NA LISSU
 
Hivyo viwanja unavyotaka vipimwe ni mashamba ya watu ndimo wanapata riziki zao na ndio chakula unachokula kinazalishwa. Matumizi ya ardhi sio kwa ajili ya kitu kimoja tu.
Samahani una elimu gani??? Mbagala kuna mashamba??? Tandale kuna mashamba?? Manzese kwa mfuga mbwa Kuna mashamba??? Mbeya kwenye zile squatters kuna mashamba??? Mwanza kule milimani watu wamejenga bila vyoo hovyo Kuna mashamba?????

Kweli CCM ni wapuuzi!!!

Umewai kufika Oysterbay na Masaki??? Mzungu alipima vile viwanja na zile nyumba Mbona still zina maeneo na watu wanalima hata mbogamboga na ndizi????

Kweli CCM mnanipa hasira , nilipanga kushawishi watu 1000 wampigie kura Lissu na Chadema Ila mwaka huu nitashawishi watu 5000 peke yangu
 
Yeye ameongea kama mkuu wa nchi. Hayo mengine unayosema wewe ni siasa za kawaida sana.

Kuwa mkuu wa nchi kunatoa ruhusa kuagiza vyombo vya dola kukandamiza wengine? Hayo mengine sio hisia, bali habari ndio hiyo.
 
Ndo maana katiba yetu haiwezi kubadilishwa bila damu kumwagika maana ccm inapendwa sana
Sasa tukiwambia humu kwamba ccm iko imara mbona knabisha?

Umeona kwanza mafuriko yq Lisu dodoma kwenye kuchukua forom?
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Sasa tukiwambia humu kwamba ccm iko imara mbona knabisha?

Umeona kwanza mafuriko yq Lisu dodoma kwenye kuchukua forom?
[emoji3][emoji3][emoji3]
Mkuu ningeshangaa sana Kama Kuna mwanaccm angeleewa nilichoandika
 
Back
Top Bottom