Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

Unajua kanuni za uchaguzi za safari hii kuwa sio lazima upewe fomu ya matokeo? Toka awamu hii iingie madarakani, tumeshuhudia chaguzi za kishenzi, kihayani na kikatili kuliko wakati wa ukoloni. Tumeona wapinzani wakipigwa na vikundi vya wanaccm kwa uratibu wa jeshi la polisi, tumeona kwenye chaguzi za marudio wasimamizi wa upinzani wakilazimishwa kusaini fomu fake za matokeo na polisi, tena hayo yamefanyika mbele ya msimamizi wa uchaguzi, na wakala yoyote aloyegoma kusaini alipewa kipigo kikali. Tumeona wasimamizi wa uchaguzi wakifunga ofisi ili wapinzani wasirudishe fomu, hatimaye mgombea wa ccm apite bila kupingwa. Hayo ni baadhi tu yaliyofanyika mbele ya macho yetu. Ww huongolei amani, bali unazungumzia ukondoo ili ccm iendelee kukaa madarakani.
 
Zaidi ya kusababisha ugumu wa maisha , ukosefu wa ajira kwa miaka yote , kejeli kwa wahanga , dhuluma za mazao na matusi kwa mawaziri , Magufuli kafanya kipi cha kukumbukwa na wananchi ?
 
Sema anaweka historia ya kumsindikiza magufuli kwenye ushindi wake wa kishindo,sio lisu atashinda haiwezi kutokea kamwe,nje ya CCM hakuna binadamu wa kumshinda mgombea wa CCM, hajazaliwa bado
akili za kichovu sana ! nyie ndio mtakaokufa wima baada ya Magufuli kuangukia pua
 
Ukosefu wa ajira upo duniani kote , hilo lijisu litafanya nini cha ziada? Na makelele yake mengi alionayo?
Mkuu hii point yako Ina mdhalilisha rais wetu. Rais wetu anaweza akaidhibiti corona inayotikisa dunia,huku ikiua maelfu ya watu harafu ashindwe issue ndogo Kama ajira? Nadhani wewe umetumwa na beberu si bure
 
Zaidi ya kusababisha ugumu wa maisha , ukosefu wa ajira kwa miaka yote , kejeli kwa wahanga , dhuluma za mazao na matusi kwa mawaziri , Magufuli kafanya kipi cha kukumbukwa na wananchi ?
Lissu atafanya nini kuhusu ajira ? Kama si kudanganyana ili kupata kura, dunini kota hakuna ajira.
 
Lissu atafanya nini kuhusu ajira ? Kama si kudanganyana ili kupata kura, dunini kota hakuna ajira.
Atajenga viwanda ambavyo CCM wamechukua pesa wakazitumia kudidimiza demokrasia, ataleta wakulima wa kimataifa kuja kulima mashamba makubwa kwenye mapori kutoa ajila na pia kuingiza pesa za kigeni kwa kuuza nje na Nchi Jirani
 
Mkuu hii point yako Ina mdhalilisha rais wetu. Rais wetu anaweza akaidhibiti corona inayotikisa dunia,huku ikiua maelfu ya watu harafu ashindwe issue ndogo Kama ajira? Nadhani wewe umetumwa na beberu si bure
Kweli kabisa kwa msaada wa Mungu hakika tumemshinda ibilisi korona, lissu atafanya nini? Zaidi ya kelele anazopiga?
 
Reactions: nao
Zaidi ya kusababisha ugumu wa maisha , ukosefu wa ajira kwa miaka yote , kejeli kwa wahanga , dhuluma za mazao na matusi kwa mawaziri , Magufuli kafanya kipi cha kukumbukwa na wananchi ?
Ugumu wa maisha Jpm kausababisha vipi??Tatizo mirija ya pesa hakuna ndo Mana mnalalamika ugumu was maisha, watu waliozoea pesa za janja janja !. Sa hivi hakuna . Unaposema Ajira mbona serikal imeajir karb madaktar 1000 na kada ya ualimu?..Serikali haiwez kuajir watu wote, ndo mana kuna private sectors . Matusi kwa mawazir so what?? Yupi alishatukanwa? Kama ni uzembe si wanafanya wao. Ndo mana serikalini nidhamu imerudi tofauti na tawala zilizopita.
 
Mkuu usipige kura!
 
Kura yangu nakupa lisu ukiingia madarakani tangaza ajira utukomboe
 
Siyo suala la kuahidi, uchaguzi unapaswa kuwa wa huru na haki. Maana hii siyo hisani ya Rais hadi mpaka aahidi.
Sawa mkuu. Mimi binafsi nawapenda sana cdm lakini mujitahidi sana kuwa wazalendo kwa mama Tanzania. Kuisema vibaya Tanzania nje ya mipaka sio jambo poa. Lakini jitahidini kuheshimu mamlaka za kiserikali.utovu wa adabu kwa mhe rais, hii kitu sio nzuri.
 
Kweli kabisa kwa msaada wa Mungu hakika tumemshinda ibilisi korona, lissu atafanya nini? Zaidi ya kelele anazopiga?
Sasa kwanini umdhalilishe rais wetu kumlinganisha na watu wengine duniani? Rais wetu amejenga viwanda vingi zaidi ya vile vilivyojengwa na wajapani kwa miaka 100,yeye amevijenga kwa miaka mitano Sasa hilo tatizo la ajira Tanzania linatoka wapi?
 
...
Safari hii tunamchagua Mtanzania mwenzetu anaye jali utu wetu, tamaduni zetu, haki zetu na Uhuru wetu.

Hatuwezi kumchagua mtu anaye jali madaraja au reli kuliko utu wetu na Uhuru wetu.
...
Maendeleo hayana vyamaa.

Kuna ushahidi gani huyo Mtanzan8a anajali utu wakati kwa kauli na matendo ni mtu mnafiki, mwenye majivuno, hasiheshimu mamlaka?

Kwa kuwa "hujui kuwa hujui" ndiyo maana thamani ya miundo mbinu imara na bora kwako si kitu.
 
Wakati kule mtaani TL anajulikana katumwa na beberuzi. Kwenye mitandao manaandika Mambo ya kutiana moyo.

Nendeni mtaani mkawaambie kwa nini TL ametumwa na beberuzi, kwa nini anaukubari Ushoga uje TZ. Kwa nini anapenda kutumia Media za kizungu kuongelea mambo ya chumbani/TZ?

Humu munatusumbua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…