Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

Aisee nieamini makamanda wa hapa JF ni bendera fuata upepo, hakuna hata mmoja mwanachama halisi wa Chadema, pereree tu

Mpaka sasa jamaa ameshachukua fomu hakuna hata picha moja

Chadema ni mitandaoni tu, tena kwa watu wachache wenye ID's nyingi
Mwaka huu lazima roho ziwatoke
 
You have nailed it. Yaan kila mtu ni mpiga mskofi hakuna mwenye uthubutu wa kuhoji as if wao ndio waajiri wetu.
Inashangaza sana unampa mtu kura akuongoze afu anaanza kukutisha
CCM inamtaji wa wajinga wengi sana.
 
Wajumbe wa mkutano mkuu cdm wakiwa wote wamevaa barakoa na vitakasa mikono vikiwa mikononi mwao ikiwa ni tahadhari KWA ugonjwa wa corona
FB_IMG_15968540130999549.jpg
 
Wewe umesomea taaluma gani kwanza? Kwa maelezo yako unazungumza porojo. Wapi duniani ambako serikali ndio inalisha watu? Yaani wewe ukae serikali ikujengee, ikusomeshee watoto, ikutibie. Endelea kujidanganya nyuma ya key board huku wenzio tukihangaika kuniletea maendeleo.
Jukumu la serikali ni kuweka sera, sheria, kusimamia amani , usalama , kukusanya kodi na kutumia kwa huduma zinazochichea ukuaji wa kiuchumi.
Tafuta mtu aliyesomea uchumi akuelezee abc za uchumi ili usikalie ndoto za alinacha. Mwananchi analo jukumu la kufanya ili aweze kuwa na maisha bora na sio kuwa serikali ndio itamletea maisha bora.
Jiulize unatoa mchango gani katika maendeleo ya nchi.
Kabla ya ku comment huu upuuzi wako hapa labda nikuulize uliisoma vizuri na kuielewa comment yangu??? Au umekurupuka tu kuja kujibu baada ya kupewa hela za bundle na Polepole na Gwajima???
 
Aisee nieamini makamanda wa hapa JF ni bendera fuata upepo, hakuna hata mmoja mwanachama halisi wa Chadema, pereree tu

Mpaka sasa jamaa ameshachukua fomu hakuna hata picha moja

Chadema ni mitandaoni tu, tena kwa watu wachache wenye ID's nyingi
picha za nini unazozitaka?
 
Kutoka maeneo mbalimbali kwenye viunga vya mji wa Dodoma, Tundu Lissu leo anachukua Fomu ya Urais.

===



Tundu Lissu leo kwa Mara ya kwanza anarejea katika mji wa Dodoma akienda kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea Urais. kumbukwe Tundu Lissu m,ara ya mwisho kuondoka katika mkoa huyu ni baada ya kupigwa risasi.

Fuatilia baadhi ya matukio na picha mbalimbali za tukio hilo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA Tundu Lissu akiwa amewasili katika Ofisi za Chadema Kanda ya Kati zilizopo jijini Dodoma na kupokelewa na viongozi mbalinbali wa Chama, wanachama, wapenzi na mashabiki wa Chadema, kabla ya kuelekea Ofisi za Tume ya Uchaguzi kuchukua fomu, leo Jumamosi 08/08/2020.

====

TUNDU LISSU AFIKA OFISI ZA NEC KUCHUKUA FOMU YA UTEUZI

Mgombea Urais Tanzania kupitia Chama cha CHADEMA, Tundu Lissu amefika katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu ya Uteuzi ya kugombea Urais

Lissu amefika katika Ofisi hizo na Mgombea Mwenza Salum Mwalim huku wakiwa wamesindikizwa na Wanachama wengine. Wamekabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage

Uchukuaji fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza Agosti 5 hadi 25,2020.

#JamiiForums #Siasa #JFSiasa #Uchaguzi2020

Naona umeedit maana ulikuwa umeandika Bernard Membe.
 
Back
Top Bottom