Swali zuri kaka, na hii ndio jibu la kwanini tumekuwa na wanasiasa wajinga wajinga, siasa imegeuka kuwa mtaji wa kutokea kimaisha. Ndio maana unaona watu wanaagalia tu hizo nafasi za kisiasa na kuzipigania lakini sio kuleta mabadiriko yoyote kimaendeleo kwa watanzania.Hivi ni kwanini tunatumia muda mwingi sana kujadili nani atakuwa Rais wakati matatizo yanayokabili maisha ya kila siku tunapishana nayo bila kuyapa nafasi ya kuyajadili?
Na CHADEMA inayosemwa hapa ya Tundu Lissu ambaye ni mropokaji halafu anakimbilia kusema....eti ilikuwa HEARSAY. Hivi mimi si naweza nikasema mkulu ni shoga story ikapewa front page coverage nikiulizwa nitasema hearsay piaMnasuka mpango tutawaliwe na chinga mwingine siyo! To hell with this. Heri kura yangu ya kula niwape CDM.
Hivi umesoma post yangu yote kweli? Swali lako linaashiria umesoma kichwa cha uzi tu; Vinginevyo nimefafanua kwa kirefu sana kwanini nime pick hao wawili;
What about the Zanzibar factor? - Shein kwa mfano.Una hoja za msingi sana lakini kwa sasa naomba nikazie kwenye hoja yako kuhusu uwezekano wa CCM kuja na jina jipya kabisa la mgombea Urais dakika ya mwisho, ambalo hatulisikii hivi sasa:
Ukweli unabakia kwamba - CCM haina resources wala muda wa kumnadi mgombea atakayeibuliwa from nowhere a few months before elections; CCM ilifanya kosa hili mwaka 1995 kwa kumchagua Mkapa, na ikalazimika Nyerere azunguke nchi nzima kumuuza; Pamoja na intervention hii ya Nyerere katika kumuuza, Mkapa akapata the lowest victory in CCM's history (lower 60s in percentage); CCM haitaenda huko tena kama unavyofikiri, Rais ajae (iwapo CCM itahinda) atatoka miongoni mwa majina haya haya tunayoyasikia, na ingawa mbio hizi zinakemewa kwamba zinaharibu chama, kwa upande mwingine CCM inafurahia kwani inasaidia marketing ya candidates to its Members of National Congress lakini pia the electorate at large, na wakati muafaka ukifika, watachagua kati ya majina haya haya;
Nilishakubali matokeo zamani!. Mgombea wa CCM could be anyone between Membe, Magufuli au Pinda. The bottom line ni akiwa Mkristu ni lazima awe Mkatoliki, masikini Lowassa sio Mkatoliki!.Hujamuweka Lowassa??? Unatafuta ugomvi na Pasco and Co.
Mwisho kabisa niseme tu kwamba nia yangu hapa sio kupigia debe viongozi hawa wawili kwani mbali ya siasa za NEC nilizojadili na pia conditions nilizojadili hapo juu, bado wana kazi kubwa ya kuaminisha watanzania kwamba atakayepita atakuwa Rais Bora na sio Bora Rais; Na mpaka tufikie hatua hiyo, Chadema wakifanyia kazi mapungufu yao, Rais Bora kwa Tanzania 2015 ni Tundu Lissu, na hii ni changamoto kwa Wagombea wa CCM kwamba muda ukifika, waanze kujieleza kwa wananchi kwamba wanasimamia ISSUES gani, kwani suala la PERSONALITY halitakuwa kigezo tosha cha kumpelekea mgombea Urais ikulu 2015; Inawezekana huko mbeleni wagombea wa CCM wataanza kunadi issues wanazosimamia, lakini mpaka tufike huko, mimi binafsi nadhani iwapo kutakuwa na uchaguzi wa Rais leo, Rais bora wa Tanzania ni TUNDU LISSU;
Mchambuzi, nashindwa kuelewa na nashangaa kwanini una m-exclude kipenzi chetu Dr. W. P. Slaa!Asante kwa mchango wako kiongozi; Nia yangu katika hatua ya mwanzo ilikuwa sio kuelezea sifa za hawa wawili bali sababu kwanini nadhani matukio ya sasa yatapelekea kuwa top three kwenye kinyang'anyiro hicho; Lissu nimemtaja kwa makusudi kama njia ya kuchokoza mada, hasa kuonyesha kwamba jina lako kupita CCM haitakuwa automatic kushinda Urais, hasa iwapo Chadema watafanyia kazi mambo kadhaa niliyojadili hapa na kwingineko; Vinginevyo nchi yetu inahitaji rais ambae:
1. Ana msimamo unaoeleweka juu ya muungano, hasa wenye kuweka maslahi ya Tanganyika na Tanzania kwa pamoja, na hafichi msimamo wake kwa kuogopa kuangamia kisiasa kwa kudai Tanganyika ndani ya Tanzania;
2. Ambae atakuwa ana heshimu utawala wa sheria;
3. Ambae atakuwa mkali juu ya ufisadi/rushwa;
4. Ambae ataendana na demographics zilizipo sasa katika population i.e. taifa kuwa ni la vijana;
5. Ambae anaonyesha uwezo wa kujenga hoja kuhusiana na maslahi ya taifa nje na ndani ya bunge;
6. Mwenye elimu, uelewa na pia upeo juu ya masuala la kisiasa, kijamii, kiuchumi, na kisheria, ndani na nje ya nchi;
7. ETC
Lissu anatosha katika mengi kama sio yote juu ya haya, na ni vizuri wagombea wa CCM muda ukifika nao wao tuwapime kwa haya na mengineo;