Elections 2015 Mgombea Urais CCM 2015: Ni Bernard Membe au January Makamba

Mchambuzi

Uchambuzi wako nimeukubali kwa kiasi fulani ila kama mchangiaji mwingine aliyesema uliharibu kidogo kwa kumpigia debe Tundu Lissu mwishoni.

Kwa manufaa ya wasomaji ungeandika sifa chanya na hasi za wajumbe wote wa NEC Taifa. Wajumbe wa bara na Visiwani maana wajumbe hawako kumi tu wako kumi toka bara na kumi toka visiwani. Labda uanze kuandika mjumbe mmoja baada ya mwingine kwa kutumia vigezo vitano ulivyoambatanisha hapo juu. Mfano katika kumi bora Mjumbe namba moja ana vigezo hivi hapa 1,2 3 hana vigezo 1,2,3 then u go down the line. Start with Wassira, Makamba, Nchemba mpaka Mukangara. Vivyo hivyo kwa upande wa Visiwani Dr. Mwinyi, Prof. Mbarawa, Samia Hassan mpaka wa kumi Khadija Aboud.

Swali jingine kati ya Dr. Mwinyi na Wassira nani amepata kura nyingi zaidi. Maana nimeona kura zote za bara lakini kwa visiwani naona yamebandikwa majina tu bila idadi ya kura
 
Last edited by a moderator:

Hivi ni kwanini mnasema nimeharibu kwa kumtaja Lissu mwishoni wakati ukweli ulio wazi ni kwamba hii ni timu ya CCM inayojipanga kuingia katika ushindani na chadema 2015? Ni dhahiri mgombea wa Chadema 2015 atakuwa ni mtu makini kama vile Dr. Slaa au Lissu, na ni muhimu CCM ikajipima kwa mtazamo huo, kwani hawa wawili ni viongozi bora kwa vigezo vingi na itaendelea kuwa hivyo mpaka pale CCM itakapokuja na jina ambalo nalo over time lita convince umma kwamba na yeye pia ni kiongozi Bora; Ni muhimu mkaelewa kwamba Chadema wao ni kama wapo tayari in terms of candidates wenye sifa, kinachosubiriwa ni upande wa CCM tu, na ni kwa maana hii, katika maandalizi hayo, ni vyema CCM ikajipima kwa majina kama LISSU, otherwise mchakato wao wa huko Dodoma kujipanga 2015 utakuwa ni kupoteza tu muda;

Bila ya CCM kuja na mkakati ambao utazaa mgombea mwenye kuweza kuwathibiti Lissu au Dr. Slaa 2015, zoezi zima la Dodoma litakuwa limepoteza tu muda na fedha za chama; Na iwapo mjadala wangu ungepuuzia hili, mjadala huu ungekuwa na mapungufu makubwa sana, kwani Membe na January wakipitishwa wataenda kushindanishwa na nini, JIWE?

Hoja yako juu ya haja ya kuchambua sifa za wajumbe wote wa NEC ni nzuri lakini maudhui ya uzi huu haikuwa hiyo; Kama kuna umuhimu wa kufana hivyo, hata wewe ungekuja tu na uchambuzi huo kwani tungechangia kwa wingi tu kwa hoja, na kwa kujenga, sio kubomoa;

Kuhusu kura za Mwinyi na Wassira, nadhani Wassira amepata kura nyingi zaidi, kwani kama vile niliona sehemu kwamba Mwinyi kapata kura around 1,800, ila nita confirm nikipata taarifa kamili;
 

Kipimo kizuri juu ya kura za CCM kufikia 50% au zaidi ni matokeo ya ubunge katika mikoa yote ya bara uchaguzi wa 2010.

Kwa mfano, katika mikoa yote ambayo kwa juu juu mtu unaweza kudhania ni ngome za Chadema, ukiangalia jumla ya Kura za ubunge kwa kila mkoa, CCM iliishinda chadema kwa at least 55%; hata Arusha ambayo inadhaniwa kuwa ni ngome ya Chadema, jumla ya kura za ubunge katika majimbo yote saba ya mkoa, baina ya CCM na Chadema, CCM ilipata wingi wa kura kwa asilimia at least 55%; Ukichanganya kura zote zilizopigwa for chadema na CCM katika majimbo haya, CCM won (in total katika majimbo yote saba) by at least 55%, i.e:

  • Longido (CCM)
  • Monduli (CCM)
  • Ngorongoro (CCM)
  • Arumeru Magharibi (CCM)
  • Arumeru Mashariki (Chadema)
  • Arusha Mjini (Chadema)
Ni muhimu Chadema wakatumia takwimu hizi kama changamoto yao kuelekea 2015; Vinginevyo kutumia takwimu za kura za Urais 2010 kidogo kuna tatizo kutokana na hoja kwamba kura katika ngazi ya Urais zilichakachuliwa; Tofauti na kura za Urais, kura za Ubunge kwa kiasi kikubwa ziliakisi uhalisia wa mambo on the ground;
 

Naomba utembelee uzi wangu mwingine ufuatao:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/350624-wagombea-urais-tiketi-ya-ccm-tunawapimaje.html
 
Ukisoma mstari kwa mstari na kuelewa maudhui yangu ambayo hasa ililenga kuelezea utamaduni wa CCM katika nyakazi hizi, ungeelewa kwamba mimi sipo hapa kumpigia kampeni January; Lakini nashukuru wapo wengi walioelewa maudhui yangu ilikuwa ni nini;
 
Mleta uzi kaamua kumhujumu makusudi Dk SLAA kwa maslahi ya ccm. Hata hivyo GT wameshamwelewa kusudio lake la ndani nalo sio hao Membe na Makamba bali kupima upepo juu ya Dk Slaa baada ya chaguzi hizi za ccm.

Unachosema sio sahihi, iwapo umekuwa unasoma michango yangu mbalimbali, na hata kwenye uzi huu, nathamini sana mchango wa Dr. Slaa katika siasa za nchi yetu, hasa katika kuinyoosha CCM kwani ilidhania wananchi wataendelea kulala; Dr. Slaa au Tundu Lissu - haya ndio majina ambayo nimekuwa nayajadili kwa CDM 2015, lakini kwa mtazamo wangu, Dr. Slaa anaweza kukumbwa na suala la umri, kwahiyo ni muhimu kwa CDM kuangalia CCM inamsimamisha nani; Vinginevyo iwe, isiwe, ni muhimu Dr. Slaa akawa kwenye safu ya uongozi wa juu wa nchi, aidha kama Waziri Mkuu au Makamo wa Rais, iwapo Urais utaenda kwa mtu mwingine ndani ya CDM, hasa Lissu;

Mimi sioni mtu mwingine ndani ya CDM mwenye qualities za Urais nje ya Zitto, Slaa na Lissu; Na ni muhimu CDM ikaendelea na mchakato wa kumpata mgombea ambae atatokana na CDM die hard aliyepo ndani ya CDM sasahivi, wasifanye kosa la kutegea mtu atakayejitoa CCM na kumweka huyo ndio mgombea; Itaharibu ladha na maana yote ya mabadiliko ambayo wananchi wanaounga mkono CDM leo wamekuwa wanayasubiria kwa hamu kubwa;
 

Ndio maana nilisema awali kwamba kitendo cha membe na january kuamua kuingia kutafuta ujumbe wa NEC kupitia nafasi zile kumi za kifo ulikuwa ni uamuzi wa busara sana kwani whether you lose or win, tayari wapiga kura wa mchakato wa kumtafua mgombea urais 2015 watakuwa wameshakuona; Kumbuka kwamba ni hawa hawa waliompa kura January na Membe Dodoma ndio watakaopigia kura jina la mgombea mteule wa ccm 2015 kwani wajumbe hawa watakuwa kwenye nafasi zao hizo mpaka 2017;

Hata hivyo, naamini CCM bado wanaweza kumleta mtu mwingine nje ya wajumbe wa NEC au watu wengine wenye mvuto ambao ni wajumbe wa NEC kupitia wilaya. Kama walivyofanya kumleta Mangula , nafasi ya m/mwenyekiti.

Mtu aliyegombea ujumbe wa NEC kupitia wilaya atakuwa amecheza pata potea iwapo nia yake ilikuwa ni kuwania Urais 2015, partially kwa maelezo hayo juu; Wilay zimezaa wajumbe wa NEC zaidi ya mia moja, na wajumbe wa mkutano mkuu wa Taifa pengine wanajua majina kama 10% ya wajumbe wote waliopita ngazi za wilaya; Exception iliyopo ni kwa majina ya Lowassa, Nchimbi, Mwandosya na wengine wachache, ambao pamoja na kwamba wamepitia wilayani, majina haya yanajulikana na wajumbe wengi wa mkutano mkuu wa taifa, hivyo suala la wajumbe hawa wa NEC kuji - market kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa 2015 iwapo watagombea Urais haitakuwa kubwa sana; lakini kwa mtazamo wangu, it is less likely kwa nchimbi kupita, hivyo mwishoni kuamua kujiunga na kundi la aidha membe au January; Same applies to Lowassa na Mwandosya;

Kwa jinsi ambavyo siasa za makundi zilivyoitesa CCM, si ajabu wakatumia ule mkakati wao maarufu wote wakose na wakaja na mtu mpya.

CCM haiwezi ku-risk na mchezo huu; kwanza itakuwa haina muda wa kutosha kuuza mgombea mpya kwa wapiga kura, na pili haitakuwa na resources za kutosha kufanya hivyo; Suala la time and resources constraints litachangiwa sana na ukweli kwamba CCM ina vita zaidi ya moja na itabakia kuwa hivyo mpaka 2015; Vita ya kwanza ni kuua makundi ndani ya CCM, vita ya pili ni kudhibiti M4C, na vita ya tatu ni kutafuta mgombea anayefaa kusimama 2015; Muda na resources kukamilisha haya yote haupo; Atakayepitishwa itakuwa ni miongoni mwa hawa hawa ambao tayari umma umewasikia, hivyo kuirahisishia CCM kazi kwenye kampeni huko mbeleni; Kilichobania ni CCM mwezi May 2015 kuamua nani ni serpent na nani ni angel, na je, kati ya angel na serpent yupo atafaa zaidi kuithibiti Chadema kweney uchaguzi mkuu?

Pia ni muhimu ukumbuke kwamba mwaka 1995, CCM ilifanya makosa unayoshauri yafanywe tena 2015 ya kuja na a surprise - kwa mfano Mkapa kuwa mgombea 1995; Nyerere alilazimika kufanya kazi ya ziadi kuzunguka nchi nzima na Mkapa lakini aliambulia kumpatia ushindi wa only 62%, lowest in CCM's history; Na huyo alikuwa nyerere, je leo hii au 2015, nani ndani ya CCM atakayekuwa na uwezo wa kumpigia debe mgombea mpya nchi nzima aibwage Chadema kwa kishindo uchaguzi wa 2015????


Good and valid argument;
 
Mchambuzi kuna mtu mwingine umemsahau naye Dr. Hussein Mwinyi!! Huyu naye ni figure ingine CCM wakitaka kurudisha imani kwa wananchi kuwa ni msafi wananweza mleta huyu!!

Nakubaliana na wewe lakini kwa mtazamo wangu, iwapo Mwinyi ata attempt, basi ataingia kwa gear ya kuwa mgombea wa zamu yetu wazanzibari, na nadhani ndio maana aliamua kuacha ubunge wa mkuranga (Bara)na kwenda kugombani Zanzibar 2000; Kwa bahati mbaya, itakuwa ni vigumu kwa Mwinyi kuwa a preferred choice ya CCM (Zanzibar) ahead of Amani Karume, na pengine Bilal kama atakuwa bado ana nguvu (umri); Nje ya hawa, Mwinyi pia atapata ushindani mkubwa kutoka kwa Nahoda ambae pia ana wafuasi wengi kutoka CCM (Zanzibar);
 
Nilisikia jamaa wakisema kijiweni.....ni ili kushinda kwa wepesi kwa vyama vyote, raisi ajaye lazma awe mkristu! Hata ukiweka jiwe tu ushindi nje nje kwani wakristu wamepotezwa sana katika kipindi hiki cha 2005 kuelekea 2015. Mi simo ila nilikuwa napita tu!
 

Kama alivyosema mchambuzi mgombea wa urais ndani ya CCM atatokea kundi la kifo kati ya bara na visiwani. Kwa maoni yangu huyo mgombea atakuwa ni kati ya wale waliokuwa kwenye tano bora kutokea kundi ka kifo. Exception pekee ya haya maoni yangu ni ni wafuatao Edward Lowassa (Mjumbe wa NEC Wilaya ya Monduli), Bernard Membe (Mjumbe wa NEC Taifa kundi la kifo lakini ameshika nafasi ya #6 ) na Asha-Rose Migiro (Mjumbe wa NEC wa kuteuliwa na Mwenyekiti)


Bara
Wassira Stephen - 2,135
January Makamba - 2,093
Mwigulu Nchemba – 2,012
Shigella Martine - 1,824
Lukuvi William - 1,805


Zanzibar
Mbarawa Mnyaa - 1,850
Mohammed Seif Khatib - 1,668
Khadija Hassan Aboud - 1,625
Shamsi Vuai Nahodha - 1,603
Dkt. Hussein Mwinyi - 1,579

Ntakuja kurudi na uzi mpya kuchambua sifa za wajumbe niliowataja hapo juu
 
Umetoa ufafanuzi mzuri sana, ila umeharibu hapo kwenye para ya mwisho na hasa mstari wa mwisho kabisa ulipompa pande Lissu! Kwa maoni yangu nadhani Dr. Salim atatufaa sana uraisi kwa sasa ili kuvunja makundi yanayoiharibu CCM.
 
Haya sasa baada ya kizota kufunga kazi ma agent wamerudi kazini km kawaida, membe membe mara makamba nadhani kambi ya membe ma agent wake sasa active kazini, kaza buti waweza pata hata ubunge wa viti maalum 2015 in case bwana membe atapita
 
Umetoa ufafanuzi mzuri sana, ila umeharibu hapo kwenye para ya mwisho na hasa mstari wa mwisho kabisa ulipompa pande Lissu! Kwa maoni yangu nadhani Dr. Salim atatufaa sana uraisi kwa sasa ili kuvunja makundi yanayoiharibu CCM.

Kwani mwisho wa siku, mgombea wa CCM ataenda kushindana na kivuli au vyama vya upinzani? Sijui kwanini hamuoni mantiki ya kuweka hoja inayopambanisha mgombea CCM na potential candidate wa Chadema, vinginevyo zoezi zima la CCM kule Dodoma ambalo basically ni kujipanga kwa 2015, litakuwa limepoteza tu muda na fedha;

CCM ijipange kwa kumtafuta mtu atakayepambana na Dr. Slaa au Lissu, nje ya hapo, CCM itakuwa na wakati mgumu sana kupita 2015;

Tatizo la CCM sio makundi, tatizo la ccm ni kukosa dira, na pia ufisadi;
 

Mkuu hapo ndio huwa tunakosea sana, hivi January anahusika kivipi na kazi za dada yake! January ni January na Mwamvita ni Mwamvita.
 

Kwa kuwa tangu uhuru tumekuwa na marais wanaotoka katika makabila madogo nchini, huenda hoja zako zina ukweli ndani yake kama hutumiwi!
 

Kumbe Mbarawa Mnyaa ni maarufu kuliko hata Dkt
 
Mkuu Mchambuzi,
Asante kwa mchanganuo wako kimantiki.
Nadhani tunaelewa kuwa kura za mkutano mkuu ni za itifaki na haziwezi kutueleza kwa kina kuhusu wagombea watarajiwa.

Pili, mkutano mkuu una influency ndogo sana katika kupatikana kwa mgombea. Ule ni mhuri mkubwaa usio na madhara kama yupo aliyepita kikwazo cha NEC

Kugombea kwa NEC kuna mikiki sana siku hizi si kwa maana ile ya wajumbe kumfahamu mgombea au mgombea kuonyesha umahiri wake. Heka heka za NEC zinatokana na NEC kuipora madaraka CC kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Kikwazo cha wagombea ni NEC,ndiyo maana wengi wanapigania sana huko.

Kupigania maana yake ni kuwa na uwezo wa kujenga kundi la kuunga mkono. Ukiwa nje ya NEC kwa utaratibu wa CCM ya sidhani hata jina lako laweza kutajwa.

Kwa mtazamo wangu January na Membe hawakuchukua risk kwa mintaarafu ya kujulikana. Wamefanya hivyo kwa kujua kuwa risk ya Wilayani itawaondoa machoni kabisa kama ilivyomfanya Mzee F.T.Sumaye ambaye keshasahaulika hadi tunaandika haya. Jan na Membe walifahamu kuwa uwepo wao NEC ni muhimu sana na hivyo kuchukua risk was the best option on the Table.Kama italipa au la ni suala la muda.

Mgombea wa CCM anaweza kutoka nje ya ''circle''. Nimeangalia sekretariati naona wameitwa wenye chama kuokoa jahazi. Wengi hatutawasoma majina yao lakini wanafanya kazi nyuma ya pazia.
Angalia link ya Mangula, Kinana, Seif Khatibu kwa kuanzia tu na tujue sekretariati inaunda 1/3 ya CC.

Kuna mtu hatajwi sana lakini amebeba karata muhimu sana ya CCM. Endapo mdodoro wa chama utakuwa kama ulivyo na uwezekano wa kura za itifaki au 50.01% hautakuwepo basi itatumika karata ya mwisho.
Udini na Ukabila unaonekana kutofanya kazi kama walivyotaraji, sasa tutaona JINSIA na hapa ndipo jina la Asha Rose linapoingia.

Jina la Asha Rose halitaletwa kama mwanamke, litaletwa kama mzooefu wa chama, kimataifa, asiye na makundi ataunganisha wanachama na hana kashfa. Kwenda katika mpambano na Chadema tutasikia hii ni zamu ya wanawake. Mtindo huo anaujua Samwel Sitta.

Ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…