Uchaguzi 2020 Mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, Bernard Membe achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC

Kama ana nia njema amuunge mkono lissu. Atafikiriwa hata ugavana wa benki Kuu.
 
Ni vizuri Membe analeta amshaamsha, lakini kama hajatumwa basi hii kitu inaweza mpotezea umaarufu.
 
Hivi Membe kabisa yupo serious ?Hope mbeleni atamwachia Lissu. To be honest Ukijumlisha kura za zote upinzani mwaka 2015 ,upinzani walimshinda Magufuli tatizo ushindi wao waliugawana.

Wewe utakuwa either ni mchaga wa siasa za Tanzania au hujui mahesabu ... Hata wapinzani wakiungana kamwe hawawezi kuishinda CCM!
 
hili ni pandikizi kuu la ccm, kazi yake kuu ni kuhakikisha anapunguza kura za upinzani.........mtanielewa siku fulani..
 
Ila Membe anahangaika nini?

Washauri wake naoni viazi.
Hisia zangu zinanituma kuwa Membe huenda yupo ACT kimkakati! Atagawa kura za Tundu Lissu na kumpa gap kubwa la kiuongozi Mzee baba.
 
Huyu mtu si alisema bila muungano wa vyama vya upinzani (grand coalition) hatagombea urais??? Akatudanganya kuna "tsunami" ya wanachama wapya toka upande ule wanakuja kumfuata! So far hatujasikia hata mwenyekiti wa kitongoji kamfuata huko aliko.
 
Eti akaleta usanii kule kwao Rondo.
Akajisemea wanaCCM zaidi ya mia tatu wamerudisha kadi zao. Kadi zenyewe zote mpya . CCM ilaaniwe kwa kueneza ujinga na upumbavu Tanzania


Chama cha upinzani Tanzania ni kimoja tu nacho ni CHADEMA na Mgombea wake ni Tundu Lissu. Vyama vingine vyote ni matawi ya CCM.

Kwa maana hiyo CCM ina wagombea wengi ambao watazigawa kura za CCM, na upinzani una mgombea mmoja tu Tundu Lissu ambae atapigiwa kura zote za upinzani. Sijui hofu yako kwa Membe kugawanya kura za upinzani inatoka wapi? Wewe shangilia tu CCM inagawanya kura zake hivyo kumpa uhakika wa ushindi Mgombea wetu wa upinzani Tundu Lissu.
 
Halafu wanadai eti wataungana na CDM thubutu. Labda kama kuachiana itakuwa ubunge na udiwani lakini urais wa Tanzania Lissu na Membe kila mmoja atashiriki. Ila mmojawapo akienguliwa na Tume hapo ndipo watashirikiana. Kwa Zanzibar no choice CDM hata wakishiriki mgombea wao hana impact kwa Maalim.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…