Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
SIJAWAHI KUPIGA KURA, may be 2025 nitapiga maana nami nitakuwa mgombealowasa na slaaa ndio walikuwa wapinzan wa kweli na bila shaka uliwapa kura
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
SIJAWAHI KUPIGA KURA, may be 2025 nitapiga maana nami nitakuwa mgombealowasa na slaaa ndio walikuwa wapinzan wa kweli na bila shaka uliwapa kura
Huyu kachero ni mharibifu tu maana nna uhakika baada ya uchaguzi ataombara radhi na kurejea ccm....
Tunakwenda na Tundu Lissu
Eti akaleta usanii kule kwao Rondo.Membe ni CCM kwa 100%+
Hivi Membe kabisa yupo serious ?Hope mbeleni atamwachia Lissu. To be honest Ukijumlisha kura za zote upinzani mwaka 2015 ,upinzani walimshinda Magufuli tatizo ushindi wao waliugawana.
Sasa mbona wanatuchanganya siamuachie TL au wote wautaka Urais? Mwaka huu kazi ipo.
Akijitoa na amesharudisha form,jina lake litakuwepo kwenye karatasi ya kupigia kura.Hapo pana mtego unachezwa dk za mwisho member anajitoa
Hisia zangu zinanituma kuwa Membe huenda yupo ACT kimkakati! Atagawa kura za Tundu Lissu na kumpa gap kubwa la kiuongozi Mzee baba.Ila Membe anahangaika nini?
Washauri wake naoni viazi.
Huyo yupo kazini kurudi maslahi mapana ya ccmHuyu mzee anapapara tu, angebaki ccm nchi ingekuwa yake
Eti akaleta usanii kule kwao Rondo.
Akajisemea wanaCCM zaidi ya mia tatu wamerudisha kadi zao. Kadi zenyewe zote mpya . CCM ilaaniwe kwa kueneza ujinga na upumbavu Tanzania
Halafu wanadai eti wataungana na CDM thubutu. Labda kama kuachiana itakuwa ubunge na udiwani lakini urais wa Tanzania Lissu na Membe kila mmoja atashiriki. Ila mmojawapo akienguliwa na Tume hapo ndipo watashirikiana. Kwa Zanzibar no choice CDM hata wakishiriki mgombea wao hana impact kwa Maalim.Mgombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo pamoja na mgombea mwenza Profesa Omar Hamad leo Agosti 7, 2020, wamechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za NEC Jijini Dodoma.
View attachment 1529783TAARIFA KWA UMMA
View attachment 1529827
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mh. Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage akikabidhi fomu za kugombea kiti cha Rais kwa Mgombea wa Chama cha ACT-Wazalendo, Bernard Membe katika Ofisi za NEC Njedengwa Jijini Dodoma leo Agosti 7,2020, kushoto ni Mgombea Mwenza, Prof. Omar Faki Hamad . Chama hicho kinakuwa cha nane kuchukua fomu.
View attachment 1529828
====
MEMBE ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Mgombea Urais wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ndugu Bernard Kamilius Membe leo tarehe 7, Agosti 2020 amechukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Membe amekabidhiwa fomu hiyo ya uteuzi na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage Jijini Dodoma.
Katika uchukuaji huo wa fomu, Membe aliambatana na Mgombea mwenza wake, Profesa Omary Fakih Hamad.
Aidha msafara huo wa Membe uliongozwa na Mwenyekiti wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu, Ndugu Ado Shaibu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Ndugu Mhonga Said Ruhwanya, Katibu wa Mambo ya Nje Ndugu Bonifasia Mapunda, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma, Ndugu Janeth Rithe, Katibu wa Ngome ya Vijana Ndugu Mwanaisha Mndeme na viongozi wengine waandamizi wa Chama.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa fomu hizo, Ndugu Bernard Membe amesema kuwa amejiandaa kufanya kampeni kabambe kila Kona ya nchi ili kuipatia ACT Wazalendo ushindi mnono na kuhakikisha ifikapo tarehe 28 Oktoba 2020, utawala wa Rais Magufuli unafikia tamati.
Imetolewa na:
Janeth Joel Rithe
Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.
Imetolewa leo tarehe 07 Agosti 2020.