Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa CHADEMA, Lissu kaahidi Bima ya Afya kwa wote

Lissu hawezi kuwa Rais wa JMT, labda akagombee kwa mabeberu hukooo![emoji23]
 
Rwanda: the beacon of Universal Health Coverage in Africa

Sikatai wao huita Mutuelle kwani wenye uwezo wa kulipa hulipia hiyo UHC na waso na uwezo husaidiwa na serikali kulipia gharama za afya.

Ni suala la umakini kwenye matumizi ya fedha za serikali ndo maana wanaweza kutenga fedha za kuwasaidia waso na uwezo.

Na ndicho ambacho kinafanywa hata na serikali ya CCM inakusanya kodi na hayo makato kisha waboresha huduma za afya na kuwasadia wananchi khasa watoto na wazee ambao sasa hivi hawalipi gharama za matibabu kwani ni bure.

Ndo maana wanataka angalau kila kata sasa hivi iwe pana kazahanati na tabibu wa kuhudumia na MSD inahakikisha dawa zafika pale.

Rwanda walianza mbali na ndo wanafikisha dawa huko vijini kwa kutumia "Drones"
 

Bima bure,
Kupunguza kodi,
Kuongeza mishahara
Kulipa pesa ambazo hazikulipwa kwa miaka mitano za kupandisha mishahala
Kulipa fidia watu wote waliobomolewa
Kulipa watu vyeti fake

Hoja kuu hizo pesa zitatokana ni chanzo kipi?
Je ataenda kuongeza deni la taifa wakati kila siku wanasema deni ni kubwa?

Je atapunguza kodi za wawekezaji na madini ili.kuweka mahusiano ya kimataifa na kodi itapungua hivyo bajeti yake itatokana na nini?
Ni wapi atapata kodi wakati inabidi aipunguze?
Jambo hili la kutumia akiri sana kwa huyu mgombea,
Ameona watanzania wote anweza kuwadanganya kwa sasa?

Mwenye kuweza kujibu haya amsaidie kujibu, hiyo pesa atatoa wapi?
 
Sera za Lissu hazitekelezeki aisee!!
 

..mimi naamini deep in your hearts mnaelewa manufaa ya UHC.

..lakini mna tatizo lenu binafsi na Tundu Lissu.
 
Badala ya kutoa hili povu ungekuja na analysis za hizo ahadi za Lisu kwamba hela atatoa wapi?
.
Vinginevyo umusukule wako uko palepale
 
Mkuu kwa hili ACT wako serious zaidi ha huyu Lisu.
 
Sera za Lissu hazitekelezeki aisee!!
Hata ya elimu bure mlisema vivyo hivyo,mwisho wa siku nini kimetokea!?
Wewe wakati ule nani angeamini kuwa ungeendelea na kale kamchezo ulichokuwa unafanyiwa "at the hill"!?
 
Hizo hela atazitoa wapi? Ataenda kuziomba kwa nchi hisani? Ataongeza viwango vya kodi ili kuongeza mapato yatayotumika kuileta hiyo bima? Au ataomba kwa Mungu atudondoshee hizo hela toka mbinguni?
Swali la kipumbavu kutoka kwa mtu mpumbavu!
 
2010 CHADEMA,kupitia mgombea wao Dr Silaa,walikuja na Elimu bure kwa kila Mtanzania anayetakiwa kupata Elimu, shule za sekondari kila kata,mlibisha kwa mistari mirefu Kama Hii,baadae mlianza kutekeleza hayo yote japo kwa wrong way
 
ukitaka CCM wahare damu gusia swala la kuwapa wananchi hasa wazee na walemavu bima ya afya na swala la kuwaongezea mishahara wafanyakazi ambao wameteswa na CCM kwa miaka 5 bila kuongezewa mishahara.
Hata hela za kuongeza mishahara mataahira ya Lumumba yatauliza zitatoka wapi?
 
Badala ya kutoa hili povu ungekuja na analysis za hizo ahadi za Lisu kwamba hela atatoa wapi?
.
Vinginevyo umusukule wako uko palepale
Makamanda hawatumii akili hata kidogo. Wao ni hisia tu.
 
Tanzania ya viwanda ulielezwa kwa push up,na ukashangilia
 
..mimi naamini deep in your hearts mnaelewa manufaa ya UHC.

..lakini mna tatizo lenu binafsi na Tundu Lissu.

Kuiwezesha UHC unatakiwa ueleze utaipatia fedha ama zinazotokana na kodi au zinazotokana na bima za afya.

Hivyo ili uwe na "best UHC" ni lazima ueleze fedha za kuiendesha bila wananchi kuchangishwa chochote yaani bure utazipata wapi.

Kwa mfano Brazil na Uingereza ndizo nchi mbili pekee duniani ambazo zina best NHS zinazoendeshwa kwa kutumia kodi za wananchi na kiasi fulani cha makato ya bima.

Ukisema ni bure basi ni kwa kila raia wa Tanzania ambae anatakiwa kuwa registered kwenye system na si vinginevyo.

Na hata wao (hizi nchi mbili) si kila kitu ni bure kuna huduma kama za macho, meno na kununua dawa ni lazima ulipie.

Kuna mtu kaniambia pale UK kupima macho sasa hivi ni pauni 25.

Suali laja unaposema itakuwa ni bure ni kwa vipi?
 
Logically kama mtu aliweza kuahidi milion 50 kwa kila kijiji laptop kwa kila mwalimu ni jambo rahisi kwa mh. Tundu lisu kutekeleza Bima kwa kila raia. Na kama nchi inauwezo wa kulipa pesa ya kustaafu wabunge zaidi ya million 200 X majimbo zaidi ya 200 pesa ya kustaafu inashindwaje bima
Ukijua ni kiasi gani cha pesa kinatolewa bure cash transfer kwa TASAF inashindikanaje kuwafanyia jambo jema kama hili wananchi wako
Inawezekana kabsa usitie hofu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…