Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa CHADEMA, Lissu kaahidi Bima ya Afya kwa wote


..basi tununue ndege nyingi, afya haina umuhimu.
 
..basi tununue ndege nyingi, afya haina umuhimu.

Afya na Elimu ni maeneo ambayo serikali yoyote hutakiwa kupimwa kwa makini iwe CCM au Chadema.

Hata wewe wafahamu wazi kwamba suala la elimu bure lipo na sasa vijana wanasoma bure kuanzia shule za msingi hadi kidato cha sita.

Na huduma za afya kwa sasa zimeboreshwa na kule MSD kunahitaji usafi zaidi wa Ufisadi na wizi wa dawa.

Hivyo ni suala la serikali kuweka juhudi zaidi kupambana na hawa wapumbavu wanaokwamisha juhudi zake.

Hizo ndege ni muhimu pia, zitaongeza ajira mapato kwa wageni watalii wanaokuja TZ na pia kurahisisha biashara kadha wa kadha kama usafirishaji mizigo na vifurushi na biashara zingine nyngi tu zinazohusu logistics.

Sasa hivi bado kusafirisha vifurushi kwenda Tanzania huchukua siku hadi 21, lakini kukiwepo ndege za moja kwa moja hadi Msalato au JNIA basi wateja watakuwa na uhakika wa mizigo kufika kwa muda mfupi zaidi.

Sasa haya si mambo ya kuilaumu serikali bali ni la watanzania wenyewe kujiwezesha kwa mipango mizuri ya biashara na ubunifu.
 
Umesoma vizuri ilani ya CDM? Hebu isomeni vizuri kisha utuambie kama jibu la swali lako hakuna
 
Nina kubaliana na wewe asilimia mia moja. Sasa hivi kifurushi cha nafuu zaidi cha bima ya afya kwa mtu binafsi kina gharimu 192,000 kwa mwezi. Kifurushi cha gharama kuliko vyote kinacho jumuisha wanandoa na watoto wanne kina gharimu 2,220,000 kwa mwezi. Uwezekano wa ku kusanya fedha hizo kila mwezi ni mgumu sana
 
Kea akili yako ya kawaida unazani Lissu atakuletea maisha Bora?
 
Kama mmewweza nunua ndege,kujenga chato inashindikana vipi kutoa bima ya afya.
 
Mpaka sasa tume ya uchaguzi imepokea rufani na mapingamizi 557 na game ndiyo kwanza mbichi. Mkuu, hii si rocket science, bima ya afya kwa wote inawezekana, ni mipango tu.
 
Manake we mwenyewe tokea urudi, zaidi ya mwezi sasa, huvai cha barakoa na wala hujitengi na jamii!. LISU HAKUWEPO NDANI YA NCHI. ALIZUNGUMZIA COVID-19 AKIWA KWA MABWANA ZAKE, KWA KUELEZWA NA MABWANA ZAKE AMBAO LEO HII NDO WANAITUMA KENYA KUITANGAZA TANZANIA KUWA INA HALI MBAYA YA COVID-19 WAKATI WAPO KENYA.

AKILI ZA WAZUNGU ZA AJABU. HUWEZA KUSHUPALIA JAMBO WAKATI HALIPO KWA KIWANGO HICHO. LEO UNICEF HAWATAKI KUKIRI KUWA TZ TUKO SALAMA KISA NI MASKINI.
 
Wewe mwenyewe umekimbia nchi yako. Kama wewe ni ngosha kweli rudi kwenu
 
Ukitaka CCM wahare damu gusia suala la kuwapa wananchi hasa wazee na walemavu bima ya afya na swala la kuwaongezea mishahara wafanyakazi ambao wameteswa na CCM kwa miaka 5 bila kuongezewa mishahara.
Kuwaongezea mishahara? Nyongeza ya kila mwaka haipo? Au unazungumzi ongezeko la kima cha chini? Hilo watapata tu ngoja miradi mikakati ikamilike na watanzania wafaidi matunda.
 
Povu
 
hauna lolote mleta mada, ukabila tu ndo unakuwasha!.
 
Na magufuli naye jana kaahidi kuwa kila mtanzania atapata bima ya afya..Hapo unasemaje
 
Kama mmewweza nunua ndege,kujenga chato inashindikana vipi kutoa bima ya afya.
Hiyo ya kiwanja cha ndege CH Charo, wakisema igawike kwa watanzania wote unadhni itakuwa sh ngapi kwa kila mtu?
Je itamsaidia kuishi hata kwa mwezi mmoja?
Tumia akiri dogo
Unafikili Tundu lisu akisema atulipie bima kila mtanzani kuna kazi ingine hapa inchini itafanyika?
Kila kitu kitasimama na hata pesa ya dawa itakosa, sasa unabaki na bima kisha dawa hamna.
 
Acha ujinga wako.
Soma universal healthcare ya Uingereza NHSinavyofanya kazi. Tena waliianzisha wakiwa kwenye umaskini mkubwa baada ya vita kuu ya pili 1948. Wakati huo wananchi wengi hawakuwa na kazi na afya ilikuwa issue kubwa. Mfumo wao kila huduma ya afya ni bure na ni hiyo hiyo Bila kujali wewe ni tajiri au maskini.

tuje kwenye bima ya afya ya Lissu. Mpaka sasa wafanyakazi wote wanalipa hii bima Tanzania. Ila huduma za afya zimekuwa mbaya sana wakati huu awamu ya tano kwasababu serikali hii inachukua hizi pesa kwenda kununulia ndege na miradi mingine isiyo na tija badala ya kuzitumia kuimarisha huduma kwa wanachama.

Lissu anasema itakuwa ni lazima kwa makundi mengine kuwa bima. Serikali yake itaweka utaratibu. Kwa wale ambao hawana uwezo kabisa serikali itawalipia.

Afya sio tatizo kwa kila mtu. Kwasababu watu wote watachangia hizo pesa zitatosha kuboresha huduma za afya kwa wale robo ambao mara nyingi ndio wagonjwa. Lazima pia ukumbuke kwa TZ wazee zaidi ya miaka 60 ni chini ya asilimia 15. Watu wetu wengi ni vijana na hawana magonjwa mengi.

kwahiyo anachokisema Lissu kinawezekana kabisa.


 
Kwa taarifa yako hata msukule wako umedandia hiyo hoja, Acha Ujinga aisee
 
Lissu hajasema atamnunulia kila mtu bima. Kasema kila mtu atakuwa na bima.

hata sasa zaidi ya asilimia 30 wana bima. Kuna kundi lingine wana uwezo lakini hawana bima. Itakuwa lazima kukata bima Kama ilivyo lazima kulipa kodi.

mwake ambao hawana uwezo kabisa ndio serikali itawasaidia kwa kulipia. Hili kundi halifiki hata asilimia 20.

na kwasababu kila mtu atakuwa na bima, ina maana bima itashuka bei. Pia sio kila mtu anaumwa na taifa letu wazee zaidi ya miaka 60 hawafiki hata asilimia 15. Wengi ni vijana ambao hawahitaji matibabu yoyote.
 
Ya Magufuli siyajui. Si ajabu naye anaongea tu.

Ndo maana pale mwanzo nikasema mimi sitegemei mwanasiasa kuniboreshea maisha yangu....
Hiyo caveat yako hakuna aliyeielewa. Tatizo wanabebwa tu na upepo bila kufikiri, yaani kutekelezeka kwa hizo ahadi ndiyo swali la msingi. Angalau hata CCM could stand their ground given that they control and manage the exchequer
 
Mgombea wako mbona kasema atatoa bima kwa wote means wanajua vyanzo vya pesa
 
Hiyo bima kwasasa ni aghali kwasababu ni watu wachache wanalipa. Kila mtu akitakiwa kuwa na bima bei zitashuka sana.

pia asilimia ndogo sana ya watu wetu ni above 60. Wengi ni vijana miaka mitano mpaka 40. Hawa hawahitaji matibabu makubwa.
Hapo economy of scale itatumika kushusha bei.

pia pesa za bima ya afya kwasasa zinatumiwa vibaya kupelekwa miradi isiyo na tija.

bima ya laki moja kwa mwaka kwa familia ya watu watano. Unaweza kupata watu milioni 20 wanaolipa maana wengine hawana familia na wengine Baba na mama wote wanafanya kazi na wote wanalipa bima.

Hapo kwa kwa mahesabu ya haraka haraka ni trilioni 2.

kakini ukweli kuna wengine watalipa milioni wale wenye mishahara mikubwa na wengine laki tano nk. Kirahisi tu unapata trilioni tatu ambayo ni zaidi ya bajeti ya wizara ya afya.

contribution ya serikali itakuwa ndogo kuliko mnavyofikiria

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…