Atakapokuja naomba mmchomekee na ki memo kutoka kwa Ad Majorem, Rais wa Wauza mahindi ya kuchoma , Moshi Manispaa:
1. Kuanzia Disemba mwaka Jana, DUNIA ilikubwa na janga la ugonjwa wa COVID-19, na hapa kwetu Tanzania, tangu Wakati huo, tulishuhudia wagonjwa wengi kabla serikali haijasitisha kutangaza wagonjwa wapya, baadae kusema hakuna wagonjwa. Chadema Kama Chama na Mgombea Urais(TL) na baadhi ya wanaharakati, tunaamini COVID-19 bado ipo na inaua japo serikali haitaki kutangaza. Sasa,
1. Je, Chadema na Lissu baada mnaamini kuwa COVID-19 bado ipo nchini?
2. Yapi maoni yako juu ya namna serikali ilivyopambana na janga Hilo? Na Je, iwapo wewe ndo ungekuwa rais, ungefuata njia gani kupambana na janga Hilo?
3. Mmeonekana kwenye mikutano yenu bila kumaintain social-distancing, kunawa mikono Wala kuvaa Barakoa. Je, ndo mmeamua msambaziane corrona hiyo mnayoamini bado ipo nchini na inauwa watu wengi?
Swali la Pili.
Kumekuwa na kauli zinazosemwa na washindani wako, kwamba ukichaguliwa kuwa Rais, Basi utahalalisha Ndoa za Jinsia Moja. Je, Upi ni msimamo wako juu ya changamoto za Wapenzi wa jinsia moja? Uhuru na haki yao ya faragha na kufurahia maisha Kama raia wengine?
Swali la tatu.
Inasemekana kuwa Robert Amsterdam's, mawakili wanaokusimamia na kukushauri kwa masuala ya kisheria, kwa Wakati fulani, waliwahi kufanya kazi na kampuni ya uchimbaji wa madini ACASIA, ambayo, Wakati fulani iliingia mgogoro na serikali ya JMT baada ya serikali kuzuia usafirishaji wa makinikia, Kama njia ya kulinda raslimali za Taifa. Raia wengi tunaamini, kitendo hiki Cha serikali, kilisaidia kulinda raslimali madini, kuhakikisha zinawanufaisha watu. Hivyo, kitendo Cha kutumia mawakili waliowahi fanya kazi na kampuni iliyokuwa kwenye mgogoro na serikali huoni Kama kina Leta Mgongano wa Kimaslahi( Conflict of interest) Kati ya pande zote tatu? Je, unauaminishaje umma wa Watanzania kuwa mawakili hao hawalipwi na ACASIA kwa lengo la wewe ukifanikiwa kushinda, uwarudishe kwenye industry ya Madini kwa Tanzania ili waendelee kutunyonya?
Asante.