Uchaguzi 2020 Mgombea wa Urais wa Tanzania, Tundu Lissu afungiwa na NEC kufanya Kampeni siku 7

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemfungia kufanya kampeni Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu kwa siku saba kwa madai ya kukiuka maadili ya uchaguzi...
Ni vyema ikaeleweka kuwa si NEC ndio wamemsimamisha Lisu bali ni kamati ya maadili ambayo kwa sehemu kubwa wajumbe wake ni wawakilishi toka vyama vya siasa nakushauri utafute muundo wa kamati ya maadili usome vizuri.
 
Tume waoga sana yaani. Baada ya Magufuli kwenda Likizo ya kujipangia siku 8, tume wameona na Tundu Lissu aende likizo ya lazima kwa siku saba. Moto hauzimwi kwa petrol.


Hahahaaa hiyo ni tawi la sisiemu mbona limemganda sana lisu,wanamuogopa sana huyu jamaa
 
Mkuu wewe ni hatari yani

wewe ni mfanyabiashara
wewe ni mtumishi wa umma
wewe ni mwanachuo
wewe unasota mtaani
wewe umetumbuliwa na kuonewa
wewe mstaafu hujalipwa mafao
wewe ni mwananchi uliebomolewa nyumba
wewe ni "nk"

zote hizo ni title zako mkuu? kweli wewe unamuhitaji Tundu Lissu.
 
Uwezo huo wa kumfuta hamuna hata munganyisho pamoja na Mungu wenu wa chato hamuwezi

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemfungia kufanya kampeni Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu kwa siku saba kwa madai ya kukiuka maadili ya uchaguzi....

Kumbe ni Kamati ya Maadili ya Uchaguzi Ngazi ya Taifa ndio iliyomfungia bwn. Tundu Lissu na sio NEC.
 
''...Hivyo wajumbe 11 kati ya 15 wamekubali kuwa malalamiko yamezingatia utaratibu na wajumbe 2 kati ya 15 wamesema uwasilishaji haukufuata utaratibu...''

Swala la kanuni linakuwaje na upigaji wa kura?

Hesabu; 11+2=15, je wajumbe wengine 2 waliobaki wao walisemaje?
 
Hii ni technical rest for TAL , ili awe sawa na mwenzie wa CCM mana nae anaenda kumpumzika .
 
Sasa nimeamua mwaka huu nampa Lissu kura, mie nimuumini wa Haki, ccm yangu imekuwa ya kibabe sana kwa jina la taasisi tendaji kama tume.

Mimi ni muumini wa St. Thomas Aquinas , Mwanafalsa wa Sheria na Mpenda haki.

Aquinas alipata kusema "...ikiwa nikaletewa kesi kati ya Baba yangu mzazi na Shetani, na katika kesi hiyo Shetani ndiye mwenye haki, basi nitamtendea haki Shetani na kumuhukumu Baba yangu" Mwisho wa kunukuu.

#Haki Huinua Taifa#
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…