Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Kuna ubaya gani TRA kuwataka muorodheshe store zenu mnazohifadhia mali, mnaficha kitu gani, wanataka wazifahamu ili wawe wanazikagua, kwasababu huko Kariakoo kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi.

Hata kama hizo kodi zinatumika hovyo serikalini, vyema store zenu zifahamike, ili mkiwatoroka bandarini mkakutane nao store, anyway niwapongeze hao wafanyabiashara kwa uthubutu wao, hata kama sikubaliani na madai yao.
Acha upumbavu wako na ujinga wako peleka kijijini kwenu huko hujui chochote
 
Muhimu Ujumbe umefika ..
Wafanyabiashara wengi kariakoo sio wasomi ni watu wenye elimu ya kawaida tu.
Hajui kwamba watu wameandika wakiwa na hasira hapo wamefura hasira hatari ndio maana wamokosea hadi kuandika
Hebu jifikirie hata wewe ukiwa na hasira huwa unapangilia maneno kweli ?
 
Tuna viongozi wa ajabu sana kulamba kodi zetu wanaona haitoshi wanaenda kutuongezea madeni ya nje na yenyewe tuyalipe tena kupitia tozo aaaah! Tutafika mbinguni tumechoka mno.
Mimi mwenyewe nisingekubali kulipa kodi ili nikamuongezee kitambi yule waziri..kodi zote zinaishia kwenye matumbo ya watu na bado tunakopa kufidia mashimo
 
Hapo ukifungua duka lako sasa hivi inaonekana wewe ni Snitch/Msaliti hupendi umoja na wenzako

Kaa kitaalamu sana
 
Kkoo wawe na msimamo usio yumba vinginevyo wataendeshwa
Kuna wengine wameanza fungua maduka
 
Ndio maana wamegoma ili wakasikilizane na Serikali.
Hayo yote utayapata vizuri baada ya wao kusikilizwa.
Kuna kitu hakipo sawa hapo. Nimeona update na banner inasema kamata kamata imewafukuza wanunuzi wa nje?
Kivipi tena.?...hii ya mambo Sheria ya Usajili wa stoo imeunganishwa.

Mie naona ni Vita kati ya Wachuuzi na Wenye maduka yao hapo. Nasema hivi kwasababu naona wachuuzi wapo, maduka yamepigwa geti! Je wenye maduka hawawataki 'Machinga'? ...haya tusubiri.
 
Najuwa hilo nilijibu tu kwa hoja ya mtu kusema kuna mipaka lakini shida kubwa hapa watu wa TRA wanajuwa kuwa kukiwa na mfumo usioingilika utaziba mianya ya rushwa watakufa njaa wanataka tubaki na hii analog mtu aweze tu kuamua kuna nini ndani ya container na gharama waamue nadhani kuna wakala wa kufanya clearance hawa wanatakiwa kuonesha 100% kuna nini na gharama zake ni zipi na viwango vya kodi viko kisheria ukiweka number kodi ni hii sasa kuwe na hali kuweka kiwango kuambatane na doc ku support gharama japo najuwa kuna ujanja mwingi mzigo wa mil 1 wanaweza kuweka laki moja hapa ndio tunatakiwa tutafute tech kuziba hii mianya kama shida kodi ni kubwa hilo na la kisera na serikali ina wajibu kuangalia. Mbona magari hakuna shida hizi, unaleta gari unaingiza model inakupa kodi hii wala huwezi kuchezea ndio maana ukija huku mitaani kwa wauza magari bei zinafanana sana.
Kwenye magari kwenyewe tunapigwa sana aiseee. Hakuna unafuu wowote huko.
 
Hawa wafanyabiashara ni wahini na wanatumia uhuru wao vibaya kuhujumu uchumi wa Nchi..

Hoja zao hazina mashiko Kwa mfano wanasema urasimu bandarini,swali kwamba Wafanyakazi wote wa Bandari wanafanya urasimu? Jibu ni hapana Kuna wachache tuu Sasa Kwa nini hao wachache wasiwaripoti Kwa mamlaka Ili wachukue hatua?

Pili wanasema Kamatakamata ya TRA,Sasa kama hawatoi risiti Kwa nini wasikamatwe? Kuna TRA anaweza kamata mizigo bila sababu?

Mwisho Hawataki Sheria ya usajili wa stoo lakini ukweli ni kwamba hizi stoo zinatumika kuhifadhi mizigo ya magendo na hivyo kukwepa Kodi..

Mtu anaingiza au kununua mzigo mkubwa ametoa lisiti ya uongo au hajakata kabisa harafu anapeleka stoo then analeta mzigo kidogo..

Alipata mteja anamuizia mzigo wa stoo bila malipo ya Kodi,hii ni hujuma na Hawa wasichekewe..

Serikali haiwezi kuwashindwa Hawa wapuuzi wachache,
20230515_100024.jpg
 
Ulishawahi sikia kesi nyingi za Kontena za mitumba alafu ndani kuna Range Rover?
Hiyo Sasa ni issue ambayo haiwahusu TRA ni issue ya Usalama wa Taifa, jeshi la polisi, na mahakama. Ni sawa na useme eti mbolea na madawa feki yanakamatwa unataka MSD wawakamate wanaoleta hizi bidhaa feki wakati kuna TBS.
 
Back
Top Bottom