Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Kipindi cha JPM wafanyabiashara halali walikuwa wanasikilizwa vizuri na kero zao zinatatuliwa. Lakin sasa serikali ya KULA KWA UREFU WA KAMBA TRA wanakula kwa urefu wa kamba zao na hakuna anayejali sawa
Sio wanakula urefu wa kamba zao tu mkuu, kamba wamekata kabisa wanakula tu umbali wowote ule.
 
Leo asubuhi nimefika kariakoo kwenye biashara zangu lakini nimekutana na mgomo wa maduka kutofunguliwa

Nilikuwa bungeni kwa wiki kadhaa hivyo sikufuatilia sana mambo ya biashara nikiwaachia vijana...
Kila mfanyabiashara azingatie kulipa kodi kama inavyostahili!
 
Washinde Kwa lipi we ropo ropo,Hawa wamelelewa kizembe na Serikali,angekuwa Mwendazake hapo angeshafuta leseni na kuwaondoa huko Kariakoo....
Usimuhusishe JPM na serikali yenu iliyofeli,

Si ndo nyie mlioanzisha tozo na hatuoni zinafanya nini zaidi ya porojo za madarasa,

 Sidhani kama hapo kariakoo wana tabia ya migomo ila kwasababu ni serikali ya makodi acha wagome tu
 
Washinde Kwa lipi we ropo ropo,Hawa wamelelewa kizembe na Serikali,angekuwa Mwendazake hapo angeshafuta leseni na kuwaondoa huko Kariakoo...
Kwani kipind cha uyo mwenda zake kariakoo hawaja kufanya mgomo ? Alifanya nini zaid ya kukaa nao chin ku solve we unadhani kariakoo ni mnada wa uko kwenu nachingwea [emoji23] …kama ww sio mfanya biashara huwezi kuelewa wanacho zungumza.

Hii nchi ukiwa mfanya biashara ukafwata kodi ambazo tra wanataka ulipe utakuwa unawafanyia biashara wao
 
huu mgomo umejazwa matiushio kwa wanaotaka kufungua maduka, serikali iwachukulie hatua kali wachache wanaowatisha wengine wasifungue maduka
 
Aisee ubebe mabeli kichwani kutoka godown
 
Hawajuwahi Kigoma ndio? Pili kwani wewe unashabikia una maslahi na mgomo.au?
 
Kwan mipakani ndio hazichajiwi kodi mkuu au ulitaka kusemaje sijakupata vema?!
Bidhaa nyingi itakuwa zimeingizwa kinyemela thats the point ! Sasa zilipitia wapi hilo ndilo swali kuu !
 
Usimuhusishe JPM na serikali yenu iliyofeli,

Si ndo nyie mlioanzisha tozo na hatuoni zinafanya nini zaidi ya porojo za madarasa,

 Sidhani kama hapo kariakoo wana tabia ya migomo ila kwasababu ni serikali ya makodi acha wagome tu
Tozo na kulipa Kodi vinahusianaje? Tozo na kukwepa Kodi vinahusianaje?

Hawa wamelelewa vibaya sana,kama huoni inachofanya basi endelea Kigoma utapata majibu Yako
 
Umezungumzia mafuta..niulize kuwa vituo vya mafuta hawalipi kodi??
 
Ukiingiza siasa tayari uneshaharibu,

otherwise umetumwa kuuvuruga. haya ni madai ya Wafanyabiashara dhidi ya Serikali na pengine kwa chini chini kuna mkono wa watu wa CCM kuhakikisha Serikali inasikiliza madai yao tupunguze ujuaji
Mmmh hii ngumu kumeza Yaani CCM itumie mgomo kuishinikiza Serikali ya CCM itekeleze madai ya wafanyabiashara.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa CCM ndiye Rais.
 
Duh 🙄 !! Hatari sana !
 
Sijawahi na pengine sitakuja kuwahi kuelewa hizi kodi zinavyokatwa
Mzigo ukifika bandarini unatokutana na tra...
Mkuu haya mambo ya double taxation na kuwawekea wananchi masikini tozo ni kutokana na matumizi mabaya ya pesa za umma yanayofanywa na viongozi wa serikali na wanasiasa kupitia matumizi yasiyo na msingi kama kununua magari ya kifahari na kufanya ubadhirifu wa kutisha hasa kupitia manunuzi na kutekeleza miradi ya serikali.

Chukulia mfano mmoja tu wa invoice ya ndege iliyopandishwa bei mara mbili ya gharama yake halisi, kuna utitiri wa upigaji wa aina hiyo.​
 
Ndio maana wengine tukaonya kwamba tukiendekeza kazi na Bata hatutafika popote! Kila siku pesa itakayokuwa inakusanywa haitotosha kwa kuwa Bata lipo juu zaidi !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…