Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

huu mgomo umejazwa matiushio kwa wanaotaka kufungua maduka, serikali iwachukulie hatua kali wachache wanaowatisha wengine wasifungue maduka
Nimeshangaa wafanyabishara ambao hawana shida na serikali wanashinikizwa wafunge kwa maslahi ya wengine.

Ukiona wafanyabishara wanakua na kiburi namna hiyo ujue hakuna serikali.
 
Tozo na kulipa Kodi vinahusianaje? Tozo na kukwepa Kodi vinahusianaje?

Hawa wamelelewa vibaya sana,kama huoni inachofanya basi endelea Kigoma utapata majibu Yako
Sasa mnawatisha wakati ni kweli kodi iko juu kwani uongo?

Imefikia kipindi TRA wamekuwa wamekuwa kama majambazi walioidhinishwa na serikali.

Na kingine hamuwez wafanya lolote sababu 90% ya maduka pale kalriakoo ni mali za watu binafsi na si serikali
 
Sasa mnawatisha wakati ni kweli kodi iko juu kwani uongo?

Imefikia kipindi TRA wamekuwa wamekuwa kama majambazi walioidhinishwa na serikali.

Na kingine hamuwez wafanya lolote sababu 90% ya maduka pale kalriakoo ni mali za watu binafsi na si serikali
Kodi gani ambayo Iko Juu? Lini Kodi iliwahi kuwa chini kiasi kwamba Leo ndio imekuwa Juu?
 
Nimeshangaa wafanyabishara ambao hawana shida na serikali wanashinikizwa wafunge kwa maslahi ya wengine.

Ukiona wafanyabishara wanakua na kiburi namna hiyo ujue hakuna serikali.
Boss tusikuze mambo, Hakuna serikali unadhani ungekaa hapo salama bila kupopoliwa na wahuni?
 
Umezungumzia mafuta..niulize kuwa vituo vya mafuta hawalipi kodi??
Wanalipa ndio maana wanatoa risiti lakini huwezi kusikia wamevamiwa sababu kila kitu kiko recorded na huko mitaani ilitakiwa kampeni ya muda mrefu mpaka iwe tabia nunua na pokea risiti hili ni changamoto nyingine lakini kama tumeweza kwenye vituo vya mafuta kwanini tushindwe lakini kwa vituo ni kwa sababu nadhani bei ni elekezi hakuna budi utalipa tu na risiti utapokea huko mitaani anakwambia kama unataka risiti bei hii kama hutaki bei hii mtu anaona bora a save lakini mfanya biashara anakuwa anakwepa mapato sasa hili litafutiwe solution. Solution yangu kata VAT hukohuko halafu VAT refund ije baada ya kuuza baina ya mfanya biashara na TRA sio mteja.
 
TRA wahakikishe kodi inalipwa kwa haki, pia wafanyabiashara walipe kodi stahiki, waache kukwepa Kodi.
 
Kuna ubaya gani TRA kuwataka muorodheshe store zenu mnazohifadhia mali? mnaficha kitu gani? wanataka wazifahamu ili wawe wanazikagua, kwasababu huko Kariakoo kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi.

Hata kama hizo kodi zinatumika hovyo serikalini, vyema store zenu zifahamike, ili mkiwatoroka bandarini mkakutane nao store, anyway niwapongeze hao wafanyabiashara kwa uthubutu wao, hata kama sikubaliani na madai yao.
Na hiyo nfio sababu kubwa unakuta mtu ana ki fremu tu ukienda kununua mzigo anaenda store kuchukua!!Hao wengine wanatumika tu ilq matajiri ndio wameguswa!!serikali ishikilie hapo hapo,siku tatu ni nyingi watafungua wenyewe!tatizo sasa hivi wafanya biashara wa kariakoo wanajiona kama wao wanatakiwa kuwa treated tofauti na wengine!!
 
Kero ya kukamata mizigo imezidi sana, mtu uko mkoani umeagiza mzigo Dar muuzaji katoa risiti, na TRA hawajaridhishwa na risiti unashikiliwa mzigo wangu, na hiyo inaweza kuchukua hadi mwezi mzima kama hujatoa rushwa.
 
Sio kila bidhaa inayouzwa inapitia bandarini, nyingine zinapitia mipakani ambapo Tanzania inazungukwa na nchi nyingi. Nyingine zinazalishwa ndani ya nchi
Kwahiyo mipakani TRA hawapo ila wapo bandarini tu?
 
TRA wahakikishe kodi inalipwa kwa haki, pia wafanyabiashara walipe kodi stahiki, waache kukwepa Kodi.
Je ulishajiuliza hizo kodi za haki zinakwenda wap CAG ametoa report ya upotevu wa mabillion hakuna kiongoz aliechukuliwa hatua ila kila siku kuongeza kodi kwa wafanyabiashara
 
Kipindi cha JPM wafanyabiashara halali walikuwa wanasikilizwa vizuri na kero zao zinatatuliwa. Lakin sasa serikali ya KULA KWA UREFU WA KAMBA TRA wanakula kwa urefu wa kamba zao na hakuna anayejali sawa
Kipindi cha JPM si ndio maduka yalikuwa yanawekwa kofuli na biashara nyingi zikafungwa? Au upo kulinda legacy?
 
Back
Top Bottom