Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Habari wakuu nipo mtaa wa mchikichi huku kariakoo maduka hayajafunguliwa hadi muda huu kuna nini kwani?

Ngoja niangalie na mitaa mingine...
Waziri aliyetoa taarifa za uong Bungeni Afukuzwe mchana huu. Mgomo unaendelea halafu yeye analidanganya BUNGE kwa faida ya nani?

Ili iweje au anataka kutuambia kuwa serikali hii ni janja janja afukuzwe mara moja na gazeti la Mwananchi liache mara moja ukahaba wa kila tatizo anasingiziwa wazir mkuu.

MAJALIWA ni muungwana sana sema Team january makamba, msoga gang na mawakala wao Zitto na nape wanakataliwa MADEAL yao
 
Tusichukulie poa, mazingira ya biashara kwenye nchi yetu ni magumu sana yani kuna utitiri wa kodi kibao.
mfano mimi biashara yangu nauza samaki wabichi mtaji milioni 4 ...
kodi nazokumbana nazo kwa mwaka..
1. TRA NALIPA 370,000
2. LESENI NALIPA 41,000
3. LESENI YA FISHERIES NALIPA 100,000
4.TAKA NALIPA 60,000
5. FIRE NALIPA 150,000
6.TMDA NALIPA 150,000
7. SERVICE LEVY 50,000

Apo bado gharama zingine kama kupanga frame, na gharama za uendeshaji.

Kuna haja kubwa ya kuangalia hiz kodi ni nyingi lazma ukwepe tu ili uweze kupata chochote.
Nimepiga hesabu kodi tu hapo ni 25% ya mtaji.
Ndio maana baadhi huwa wanaamua kukwepa baadhi ya kodi.
 
Pengine wewe upo ofisini unashika peni na karatasi hujui maisha ya mfanyabiashara alafu kama hujui kitu kaa kimya Tu.
Biashara itafanyika kimyakimya na serikali itakosa mapato haijawahi kutokea kumbuka Sisi tunafanya biashara na watu wa mikoani na nje ya nchi na kuna watu foreigners kibao wapo hapa hawaelewi waende wapi.
Mfanyabiashara hawezi kufa njaa hata sikumoja.

Leo risiti za efd hazitolewi na biashara zinafanyika
Serikali haijaamua tu!!ishu kubwa hapo ni mlipoambiwa store zenu zitambulike!!mnapenda kufanya biashara ki ujanja ujanja sana!na tatizo na nchi hii kila kitu kinaingia siasa,Fuateni sheria kuna kipindi kulikuwa na matatizo kama kile cha awamu ya 5?leo mmeo kila mkija na hili serikali inaufyata na nyie ndio mmeona sasa ni muda wa kila siku kulalamika!!serikali itoe tamko anayetaka kufungua afungue atalindwa ambaye hataki afunge,na ndani ya siku tatu,tunachukua leseni yetu.
 
Watu kama nyie ni hasara kwa taifa na kwa wazazi wako pia. Nina uhakika haujawahi Fanya biashara yoyote Tanzania ukawajua hawa TRA au yawezekana unajibu huu uzi ukiwa kwa shemeji yako umetanua miguu unasubiri tu kwenda chooni.
Wewe mtoto wa mwalimu wa UPE huna hoja zaidi ya kuwa mlamba mavi tu
Hakuna mjomba wa kuwajengea Nchi,sio lazima Kila mtu afanye biashara,Kodi ya mtumishi ni kubwa kuliko Mfanyabishara mkwepa Kodi..

Serikali ikisema isimamiwe Sheria wote mtakuwa jela Kwa uhujumu uchumi,Sasa ni ajabu hata hiyo ndogonataka msilipe.
 
Kuna ubaya gani TRA kuwataka muorodheshe store zenu mnazohifadhia mali? mnaficha kitu gani? wanataka wazifahamu ili wawe wanazikagua, kwasababu huko Kariakoo kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi.

Hata kama hizo kodi zinatumika hovyo serikalini, vyema store zenu zifahamike, ili mkiwatoroka bandarini mkakutane nao store, anyway niwapongeze hao wafanyabiashara kwa uthubutu wao, hata kama sikubaliani na madai yao.
Kama Mjadala wa bungeni ulikuwa wa Kweli kwamba Container la vitenge lenye ulefu wa futi 40 hapa Tanzania linatozwa Kodi ya Tzs 280milioni, Kenya Container la vitenge lenye ulefu wa futi 40 linatozwa Kodi sawa na Tzs 35 milioni, na Zambia container la vitenge lenye ulefu wa futi 40 linatozwa Kodi sawa na Tzs 30 milioni. Kodi za hapa Tanzania ni za kishenzi! Na zinaharibu uwezo wa Watu kununua bidhaa na hivyo kuvuruga mzunguko wa biashara na kuua mtaji ya watu.

Lakini pia nimeona wasafirishaji wa Malory wakisajiri Malory kwa plate number za Zambia na Congo. Kuna Tetes kuwa hela ya kununua na kusajali Lory moja hapa Tanzania ni hela ya kununua na kusajali Malory mawili kule Zambia na change kubakia. Nchi hii inatoza Kodi za kukomoana sana.
 
Watu kama nyie ni hasara kwa taifa na kwa wazazi wako pia. Nina uhakika haujawahi Fanya biashara yoyote Tanzania ukawajua hawa TRA au yawezekana unajibu huu uzi ukiwa kwa shemeji yako umetanua miguu unasubiri tu kwenda chooni.
Huyo jamaa hajui kitu wala haina haja ya kubishana nae
 
IMG_7575.jpg
 
Hakuna mjomba wa kuwajengea Nchi,sio lazima Kila mtu afanye biashara,Kodi ya mtumishi ni kubwa kuliko Mfanyabishara mkwepa Kodi..

Serikali ikisema isimamiwe Sheria wote mtakuwa jela Kwa uhujumu uchumi,Sasa ni ajabu hata hiyo ndogonataka msilipe.
Badala ya kutulalamikia sisi walipa kodi kwanini usingewekeza hizo nguvu kuwapigia kelele wanaokwapua pesa za umma? Kwenye ripoti ya CAG ulipiga hizo kelele? au hauna kazi ya kufanya unapoteza mda JF?.
JamiiForums-1200957838.jpg
 
Back
Top Bottom