Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023

Bro kama jirani pana supu na chapati kula nalipa mimi.
 
Leo Kuna mgomo kwa wafanya biashara soko kuu kkoo kutokana na kila wiki uzinduzi wa kodi mpya

Baadhi ya kodi unazotakiwa kulipa

1: TRA.
2: FIRE.
3: JIJI.
4: USAFI.
5: Kodi ya store.
6: Makato 10% kweny commission (watu wa mihamala)
7: Kodi yakupeleka lori kkoo kubeba au kushusha mizigo

Makadilio ya kodi yamekua makubwa mno kiasi kwamba mtu akiangalia biashara yake na kodi haviendani. Kupungua kwa wateja wa nchi jirani kama Kongo,Zambia,Zimbabwe kutokana na kero ya TRA

Kwa wanaofnya biashara ya kusafirisha mizigo Jioni lzm TRA waje wafanye tasmini na Rushwa yao wanataka 3M kutokana na ukubwa wa mzigo
 
Kwan mipakani ndio hazichajiwi kodi mkuu au ulitaka kusemaje sijakupata vema?!
Hiyo comment yangu ni jibu la comment nyingine. Na kuna kitu umekikwepa umechukua kipande chako wacha nikuulize hapa.

Muuza madawa yaliyotengenezwa Tanzania ambayo hayajapita bandarini na mipakani hastahili kulipa kodi? Ukikata kodi mpakani na bandarini analipaje yeye.

Ulishawahi vuka mipaka ukaona mianya ya kupita bila kukaguliwa. Kule Arusha, Kilimanjaro na Tanga kuna mamia ya kilomita za mpaka na Kenya ziko wazi watu wanavuka. Mpaka sio ile border post pekee. Sasa hawa watalipaje kodi mpakani.

Simaanishi nawapinga ila jenga hoja isiyo na mashaka msije onekana mnakwepa
 
Huko kusumbuana ni neema kwa wafanyakazi wa Tra!! Ndipo wanapopatumia kuleta ubabaishaji kwa walipakodi ili wapate rushwa
Mambo yakinyoooka kama tech inavyoruhusu kuna watu watakufa njaa
 
Picha
 
kurekebisha katika hili la kuzungukwa na nchi 8 halina shida ni baraka sasa tusifanye kuwa ni laana. Kazi ya nchi kuweka mifumo mipakani sio bidhaa imefika dukani ndio mnakaa nje kuvizia watu na huko viwandani ndio rahisi kabisa kukusanya kodi hakuna sababu yoyote ya haya kila changamoto kuna solution japo haiwezi kuziba 100%
 

BIla kugoma, maandamano na kukomaa nao hakutapatikana tija. Tangu lini mhuni au mlamba asali akawa na huruma?
 
Hao wafanyabiashara wameweza, kuna hawa waajiriwa wanaoadhibisha siku yao Mei Mosi. NSSF, NHIF, Compensation fund, Michango ya kuzikana n.k inakusanywa na kunenepesha wengine lakini inaitwa pesa ya mfanyakazi. Kafikishe miaka 60 uende kudai chako ndo utajua hujui.
 
Sasa hivi hadi store nayo wanataka waitandike kodi!
 
Hakuna mantiki yoyote ya kupiga Kodi dukani tena unapiga Kodi stoo kwenye bidhaa zile zile. Huo ni wizi siyo kodi

Ingekuwa awamu ya 5 waandaaji wa mgomo wangetekwa jana kabla ya mgomo kuanza leo..
 
Kwa Taarifa yako BANDARINI ni mpakani, kwa hiyo huduma zote za kikodi zinazotolewa na TRA mipakani zinatolewa pia Bandarini
"Bandarini ni mpakani..." nani kakwambia hivyo? Wewe ukiona bandari pale Dar es Salaam, Mtwara na Tanga unaona ile ni mipaka. Ukitoka bandarini kuna exclusive economic zone ya Tanzania ina mamia ya kilomita majini, kule ndio kuna mpaka na international waters.

Alafu mpaka ni lazima upakane na nchi, pale Dar es Salaam bandari inapakana na nchi gani. Taratibu za kimamlaka hazibadilishi maana, mkoa wa ki-TANESCO haulifanyi eneo kuwa mkoa wa kiutawala wa TAMISEMI.

Hapo Kariakoo muuza furniture inavyotengeneza nchini atalipaje kodi kama mnataka walipishwe wanaotumia bandari na borders pekee?
This is a challenge kwenu, nishaona nchi wana mfumo mzuri sana wa kodi na unakata kodi ndani
 

Sio shida kuorodhesha shida ni kila mwezi wakati wewe ni duka sio kampuni huo muda utawezaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…