Mgonjwa aidai TMJ, Hindu Mandal fidia ya shilingi milioni 500

Sasa ulitaka wamdanganye?
 
Sasa kwenye ugonjwa kuna sababu ya kumficha mhusika?
 
mie nawafananisha Madaktari wetu na Mafundi Magari wetu wa chini ya Mwembe

anaweza akakusababishia ukashusha engine kabisa ya gari kumbe tatizo lipo kwny shockup au ukanunulishwa spare kadhaa na bado tatizo likabaki pale pale kwa kuwa bado hajajua tatizo la gari

kuna watu wanatumia dawa za miguu kwa miaka kadhaa kumbe tatizo ni UTI wa mgongo

inakuaje tuna Regulatory Authorities kwny mambo mengi kama Mabasi, simu, insurance n.k lakini kwny huduma za Afya hakuna regulatory Authority inayojitegemea na ku deal na ubora tu wa hospital kuanzia Wafanyakazi wenye sifa na vifaa tiba ?

kuna Hospital ni haramu kupima Malaria na UTI au typhoid na kuambiwa majibu ni negative
 
unakuta hospital zote hizo staff ni yule yule anahama Hama

hapo si umeona huyo Dr Mavura ndio kamuona Muhimbili akapiga rufaa aende Hindumandal huko Hindumandal akakutana na Dr huyo huyo

unapiga kona halafu unawahi kupiga kichwa
Mbona kama ni ngumu kufanyiwa operation bila kuambiwa kinachoenda fanyika?
Sidhani kama hospital zote 3 zitafanya kosa hilo hilo
 
Maskini anapaswa kuwa makini sana kwa kuwa akitoa Boko ajue hana uwezo wa 'kudaka penalt'
 
unashauri Madaktari wasome

Sasa Dr wako akawa anasoma ukasusa ukatoka nje

mie sijakuelewa Mzee
Kwanza hatuna medical scientist
Pili, daktari wetu hawasomi.
Hii field inataka sana kusoma.
Mi mwenyewe kuna dokta niliwahi kumuona tena wa Muhimbili, akawa ana google khs tatizo langu ndio ananipa maelezo
Nilimuambia excuse me, nikatoka mazima.
 
Kaka hakuna namna ya kumshughulikia daktari wa hivi kwa njia zetu zile?😁
 
Medical Negligence in Tanzania is the norm.

Tatizo amuelewi kipi kizuri kwenu; unakuta mtu hana ata ABC za usimamizi wa huduma za afya lakini anatukana jitihada za wengine.

Nilipowadharau watanzania ni majungu na kuacha Dr Gwajima atolewe hiyo wizara; sidhani wengi wetu tunaelewa how good she was kama angepewa backup ya raisi na serikali kubadili culture ya ufanyaji kazi kwenye hiyo wizara. She was more than capable na alikuwa anajua kweli kweli yule ata ulaya anaweza simamia management ya ‘university hospital’.

Mtaalamu wa management ya afya wamempeleka social services kule sasa ndio anaropoka na kufura tu uelewa wake wa intervention za ile wizara ni mdogo sana.

Matatizo mengine tunajitakia wenyewe.
 
Inasikitisha sana kwakweli,,,kuna jamaa yangu ameacha kwenda muhimbili kuchukua dawa zake za presha na za mafuta,,,anasema toka aende miaka 2 ilipita hata kuandikiwa vipimo kujua hali yake/moyo wake au cholesterol vipi,yeye akifika docta anampa dawa tu muda mwingine hata pressure hapimwi.,,,,akaamua kwenda hosp nyingine,akapimwa cholesterol ilikua Normal akaambiwa aache dawa ya cholesterol na hiyo dawa ya pressure aiache akapewa nyingine ile inaharibu figo,,,Africa sijui tulikosea wapi!!!
 
Minister of Health unasisitiza Nyungu ambayo since std 1- University level hujawahi kubukua sehemu... badala ya watu wawe Vaccinated..
 
Hakuna Cha Gwajima Wala Nani!!

Mfumo mzima wa utawala sekta ya AFYA Ni TRASHY takataka.

Kuanzia KATIBU MKUU ( DAKTARI ), Naibu Waziri Afya ( DAKTARI ), MGANGA MKUU WA SERIKALI ( DAKTARI ), RMO ( DAKTARI ), DMO ( DAKTARI ), IN CHARGEs wote vituo vya Afya ( DAKTARI )

Na Wana tabia ya KULINDANA wenyewe.

Wote hao MADAKTARI wameshindwa kuleta MABADILIKO Sekta ya Afya kwamba huyo GWAJIMA ndio angeBadili Nini??
 
Hospital ya Rufaa Mbeya ishampima mtoto mdogo ikaonekana ana tatizo la Moyo wakampa dawa anze kutumia bahati nzuri ndugu mmoja akajiongeza na kumwambia wampeleke Dar Muhimbili Jakaya,kuja kupimwa hana tatizo la moyo ila ni kifua sababh ya baridi.
 
Sasa mbona anadai fidia ndogo hivi?!!!, yaani hapo kiwango cha chini alitakiwa adai bilioni 2, ili hakimu akipunguza ndio apewe walao bilioni 1.

Hizi Hospitali hizi, mi walitaka kumpa mwanangu dozi ya mwaka mzima ya Kifafa wakati mtoto ana degedege, na alisahaanza kutumia wiki, tena ilikuwa anywe kila siku! nilipoingilia kati ndio wanajidai kwamba kulitokea mkamganyiko.., kidogo niwapeleke mahakamani.., ila jikaona niache tu , maana ipo siku utahitaji msaada wao, hivyo si vyema kukorofishana na hopsitali.

Kuja kucheki, wamekata Bima milioni 2, for nothing!!!
 
Hili la dr ku-google siyo ukilaza wala jambo geni. Nimeliona mpaka majuu. Anakuwa anatafuta kutaka kujua zaidi na siyo kwamba anategemea google kumtibu mgonjwa. Tusiwe kama watu wasio na shule ukimwambia kuwa umesomea computer anategema ujue kila kitu kwenye computer kichwani mwako. Halfu kuna nchi nyingine matibabu yanaaongozwa na protocal fulani walizojiwekea na ziko kwenye database ambayo dr yoyote anaweza kui-access kwa mwongozo zaidi wakati anatibu. Hata ma-pilot wanatembea na reference zinazoelezea hatua za kutatua changamoto fulani na hawatakiwi wazikariri zote.
 
Minister of Health unasisitiza Nyungu ambayo since std 1- University level hujawahi kubukua sehemu... badala ya watu wawe Vaccinated..
Haya ndio mambo yenu ya utoto yanayo wa cost watanzania in everyday life.

Mimi na wewe wote tunajua nchi nzima anti-vaccine alikuwa Magufuli na hakuna mtaalamu wa afya aliepinga kutokana na nidhamu ya uwoga wa kukosa mkate wako au kutembelewa na wanyofoa kucha.

Ukitaka kumjadili Dr Gwajima ongelea uwezo wa ‘managing quality in health services’ sasa kuna rules na regulations za assessment, intervention and medical procedures.

Mambo yote hayo yapo wizarani if you ask me hizo info zinatakiwa kuwa kwenye public maana ata sijui wanafunzi wa health management wanafanya vipi research zao kuelezea what went ata kwa kuchukua ili sakata la hii mada kama case study na kupendekeza nini cha kufanya kuzuia huu uzembe in the future.

Sasa Dr Gwajima mwenzako anajua miongozo yote ya hiyo wizara medical intervention, maabara, inventory control ya dawa, ward duties, usafi; ni kila nyanja ya hiyo wizara umuongopei tatizo kilaza kama wewe ukimsikiliza unaweza dhani anaropoka alikadhalika kwa wenye ufahamu wa health management wanaona she is always referring to existing regulation au policies.

Trust me Dr Gwajima ni level nyingine kwenye health management.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…