Mgonjwa kulipia 'Kumuona Daktari' Hospitali si sahihi

Ni dhuluma ya wazi kabisa , hata ukisahau documents kwenye chumba cha daktari kesho yake ukataka kurudi kuchukua huwezi kuruhusiwa kuingia lazima ulipe hela ya kumuona daktari.
Siku nyingine mtu na wewe unageuza kibao unamdai daktari hela kwakua na yeye amekuona wewe pia hivyo alipie kama wewe ulivyolipia kwa kumuona yeye
 
Kazi ya daktari ni kuokoa maisha ya watu chumba cha dakitari sio duka la mangi!
 
Naona wangepunguza au iwe sawa hospital zote ukitoa kabisa kutatokea usumbufu kila mmoja atataka kumuona daktar mwingine Hana ugonjwa ambao n serious lakin atataka kumuona Dr
Sipati picha pale agha khan ni tsh ngapi kumuona dr wa kihindi
 
Hospitali zingine wana option ya kupitiliza maabara moja kwa moja which makes sense. Story yeyote utakayompa daktari mwisho lazma atakutuma ukapime mkojo au upeleke sample ya mavi maabara na kutobolewa kidole kwa ajili ya damu.
 
Ushauri hautolewi bure. Maana analipwa mshahara..
Kama vipi Better wachaji kwa muda na pia gharama iwe affordable.
 
mkuu hapo hamn kbx we mtu amesoma miaka mitano af unataka kumuona bure acha zako ww
 
mkiongezewa Kodi mnalia tenah
 
Kusoma kila mtu kasoma tunazidiana vyumba tu
tayar sasa Apo ushaona mnAzidiana vyumba broo udakttar ni risk ya maisha ya watu kufa au kupona wanafanya hvo ili kubalance mxhahara wao mkuu hizo hela wanazozitoa m nazan zinasaidia serikali hata kuongeza vituo vingine m naona wako sahihi kbxa
 
Labda useme kuwe na kiwango kimoja kwa nchi nzima...

Ukiondoa hiyo fee, mahospitali yatafurika wakati bado uwiano wa daktari mmoja kwa wagonjwa ni mkubwa...
Kwamba hii fee imewekwa ili kupunguza Jam Hospitalini mkuu?

Hoja ya kuwekwa kiwango kimoja imekaa poa sana hata hivyo.
 
Nani kamlazimisha, si aachane na udaktari ajichimbie Sumbawanga akalime maparachichi au mahindi pia ni maisha?
nani sasa wa kuachana na mwenzake,
ww ndio uachane na kwenda kumuona kama hautaki kulipa.. uumwe hadi ufe
 
Kwa hospital za serikali ambazo ni za umma ni sawa kuweka hela ndogo lakini kwa private inakuwa ngumu,kumbuka hospital za serikali zinapewa ruzuku ila private hela yako ndio huduma yako
 
tayar sasa Apo ushaona mnAzidiana vyumba broo udakttar ni risk ya maisha ya watu kufa au kupona wanafanya hvo ili kubalance mxhahara wao mkuu hizo hela wanazozitoa m nazan zinasaidia serikali hata kuongeza vituo vingine m naona wako sahihi kbxa
Unajua bora wangefuta huo msemo halafu hiyo gharama ichanganywe kwenye bili kuu ya vipimo ..kama serikali ilivyoua kulipia kadi ya gari pale TRA
 
Nenda JKCI Muhimbili
Kumuona daktari ni 35000. kwa consultansion isiyo zidi dk 10
Dawa ni balaa
Dawa ya gout 45000 mtaani 22000
Elenopril ya BP 15000 mtaani 7500
Huo ni mfano mdogo tuu na hospital inapewa ruzuku na mishahara inalipwa na serikali
Ukienda kwenye vipimo Kama huna bima katafute dawa mbadala ni balaa tupu
 

Acha kuziingilia Private Hospitals, Hujalazimishwa kwenda kwao, Elekezeni shutuma zeni kwenye Goverment mana hao ndio wajibu wao kukutizameni nyinyi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…