Mgonjwa kulipia 'Kumuona Daktari' Hospitali si sahihi


Afya usifananishe na upuuzi mwingine,

Hizo Huduma zingine zinaweza zisiwepo na maisha yakaendelea lakini Huduma ya Afya isipokuwepo na maisha hakuna.


Fees uwepo Ila iwe Affordable.

Hizo Huduma zote ulizotaja kuna Watu tangu wazaliwe hawajawahi kuzihitaji lakini hakuna mtu ambaye hajawahi Kuumwa ambaye hajapewa Tiba iwe na Daktari wa miti shamba au Daktari wa madawa ya hospital za Kisasa.

Afya inauhusiano wa moja Kwa moja na kila mtu.
Hivyo vingine havina uhusiano WA ulazima na kila Mtu
 
ni upumbavu mkubwa kumuona daktari pesa. mbona yeye daktari akitoka nje huwa anatuona sisi bure hatumchaji
 
huyo daktari gari lake likiwa na matatizo anampelekea fundi wagari na anapewa ushauri bure na fundi. anamueleza tatizo la gari lako moja mbili tatu. buree
 
Ushauri hautolewi bure. Maana analipwa mshahara..
Kama vipi Better wachaji kwa muda na pia gharama iwe affordable.
Mfano usmbiwe kafanye full blood picture...
Umefanya,umepewa report sasa ukipewa hiyo report utaisoma mwenyewe kujua na kuielewa
Si itabidi umrudishie daktari akakusome

Ova
 
Kwani daktari halipwi mshahara?
 
Wabongo wanataka shortcut mpaka kwenye masuala ya afya zao
Ni vizuri ukamuona daktari akufanyie vipimo,we ujijue kwa undani ni tatizo linalokusibu,alafu hawa maspecialist wakikuandikia dawa hawabahatishi

Ova
 
Kwangu mm sio lazima,kulipa pesa ya daktar kabla ya Huduma.
Kama hospital inamfumo huwo wakumuona daktar mpaka ulipe kwanza,ntaenda hospital nyingine
 
Ndomana kna comment yangu 1 kwenye uzi huu,nlisema consultation fee iko kwenye kila taaluma
Mambo sheria,mambo tax,mambo ya biashara etc
Nashangaa wanaiona hyo ya udaktari tu
Kifupi suala la udaktari,afya naliheshim sana
Juzi juzi hko kigamboni kna namjua tena anauwezo tu,alikuwa anajisikia vibaya kaenda moja kwa moja duka la dawa kachkua dawa za uti
Kameza,jamaa kakata roho
Sasa badala aende hospital au clinic
Ajue ttz jamaa kajifanya mtaalam wa afya anajua
Kafa kindezi kweli

Ova
 
Nchi yetu kila mtu amekuwa kama mtoto kila mtu anataka vya bure bure
Dunia ya leo hakuna cha bure

Kuna dada mmoja alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa alikuwa anakonda sana, mpk watu wakawa wansema Ana ngoma,alipima hadi ngoma alikuwa hana
Ye alikuwa anaenda tibiwa hospital mwananyamala na zakawaida
Huko kila daktar anamuambia lake
Nkamwambia ngj nikiwa sawa ntakufanyia mpngo nkusimamie
Ila utaenda clinic moja adrikallo,pale kuna maspecialist wa kutoka muhimbili na wako vzr tu
Kweli nkamfanyiaga appointment
Tukaenda,dokta akamsikia,akamuandikia vipimo
Mwisho wa siku alionekana Ana gautter
Alimuandikia dozi na alitumia mpk leo
Yule dada kaka vzr mwili umerudi, chura imerudi
Suala la afya linataka umakini sana

Ova
 
Ama iwe ukienda buchani kununua nyama ukiingia tu buchani unalipia kumuona muuza nyama halafu ndio anakata nyama anapima unalipia nyama kilo moja unaondoka
Either hauna akili ama wewe ni mpumbavu.....majibu ni mawili tu.
"Consultation fee" ni huduma sio bidhaa,ni kazi ya daktari kujua upime kipimo kipi na kwa sababu gani?,utumie ama usitumie dawa ipi na kwa nini?,unadhani ni rahisi hio kazi?
Daktari amekaa shule miaka 6 na udaktari ndio degree pekee ambayo mtu analipa ada nyingi kuliko kozi yeyote ile,ada ya MD pale KCMC ya mwaka mmoja unaweza lipia kozi zingine za miaka mitatu na chenji ikabaki.
Ulizia gharama za kusoma MD hata dunia ya kwanza huko,U.S,Canada,Germany etc.
Daktari hana bidhaa,daktari anatoa huduma ya "materials" aliyoyasoma miaka kazaa shule,ile unayolipia ni elimu ya daktari,ni Sheria ya dunia,ukiwa mjinga lazima ulipie elimu ya kitu usichokijua.
Ukienda bar unalipia pombe,ukipanda basi unalipia nauli ufike.
Ukienda kwa daktari unalipia "fee"ya kulipia elimi usiyoijua kuhusu ugonjwa wako,ukienda maabara,unalipia vipimo,ukienda pharmacy unalipia gharama ya dawa.
 
Basi kila sehemu ingekua hivyo tungefika? Mfano ukitaka kusafiri kwenda Morogoro ukiingia tu kwenye abood bus utoe pesa ya kumuona dereva wa basi then ulipie na nauli yako kwa konda
Aisee, ni atai kweikwei!
Bila Shaka uzee ungetukuta tukiwa na umri wa miaka 20 tu,
 
Kama hakuna cha maana kwa nini utoe hio hela?[emoji1787][emoji1787]
 
Waache wafe Wakilalamika. Watanzania ni watu wajinga sana. Hata hawajui wanataka nini. MagufuliJP walimtukana sana ila sasa wanakumbuka, JK the same.
 
Unajua kua kama kuna mashirika ya bima yanafanya biashara?[emoji16][emoji16]
Watu wananunua pombe hadi za milioni usiku mmoja tu,ndio iwe kulipia Bima mwaka mzima milioni,kwa ajili ya kumuona daktari kila anapoumwa?
Hapo utagundua tatizo ni umasikini na si kumuona daktari
 
Na hilo ndio tatizo lenu, hao wanaokufa kwenye uangalizi wenu huko hospitali kutokana na aina za tiba zenu au uzembe wenu hayo hamuyazungumzii ila mkisikia mtu katumia dawa ya kienyeji au kanywa dawa bila ushauri wenu na kafariki au kapata madhara basi hayo ndio mnayaona na kuyaongea.
 
Kama hakuna cha maana kwa
nini utoe hio hela?[emoji1787][emoji1787]
Ingekuwa ni hiayari nisingetoa, sema ndio hivyo madaktari wenyewe wamefundishwa kutengeneza pesa kupitia afya za watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…