Mgonjwa kulipia 'Kumuona Daktari' Hospitali si sahihi

Waache wafe Wakilalamika.
Watanzania ni watu wajinga sana. Hata hawajui wanataka
nini. MagufuliJP walimtukana
sana ila sasa wanakumbuka, JK
the same.
Kufa kupo tu ndio maana wengi wanakufa kwa maradhi ambayo madaktari hamjui tiba zake au hamkubaliani na tiba zake ambazo ni nje ya mlichofundishwa na matokeo mgonjwa anawafia hospitali bila kujaribu njia nyengine mbadala.
 
Ni kweli upo sahihi mwanchi kulipia hiyo ghalama ya kumuona daktali kwa sababu

Huyu mgonjwa tayari analipa makodi kibao
 
Ni kweli upo sahihi mwanchi kulipia hiyo ghalama ya kumuona daktali kwa sababu

Huyu mgonjwa tayari analipa makodi kibao
HELA YA CONSULTATION HACHUKUI DAKTARI ILE NI KWA AJILI YA HOSPITAL KUWEZA KUJIENDESHA NA KUMLIPA MSHAHARA YULE DAKTARI ANAYEKUHUDUMIA .

Sent from my Redmi Note 8 using JamiiForums mobile app
 

Wewe ni daktari sio!! Naona unatumia nguvu kujitetea
 
Suala la afya liko kwenye jukumu lako mwenyewe.....
Ukiona unahisi unatofauti mwilini,au unajisikia ndivyo sivyo muone daktari
Aliyebobea kwenye kazi yake
Ova
 
Ingekuwa ni hiayari nisingetoa, sema ndio hivyo madaktari wenyewe wamefundishwa kutengeneza pesa kupitia afya za watu.
Dunia ya sasa ndiyo ilivyo
Bila pesa hupati kitu

Ova
 
Labda useme kuwe na kiwango kimoja kwa nchi nzima...

Ukiondoa hiyo fee, mahospitali yatafurika wakati bado uwiano wa daktari mmoja kwa wagonjwa ni mkubwa...
Unaonaje pia kama watakuwa wanawajibishwa severely wakimsababishia mtu/mgonjwa kufanya irrelevant diagnosis au hata kumpa dawa zisizotakiwa?

Maana kama ni usumbufu kumuona, vipi kuhusu kufanyia mafunzo mwili wa mtu?

Wengi wanaotea!
 
Sasa daktari atalipwaje,
Gharama za kumlipa daktari ziwekwe kwenye vipimo au kwenye madawa, au kwenye getini kama get pass ukiingia tu utoe hela?
 
Hahahaha

Sio education.

Ila sielewi bado. Hujanishawishi.

Health care ni basic needs.

Inatakiwa itolewe for free au kwa very minimal cost ambayo kila mtu anaweza afford. Over
 
Mfano usmbiwe kafanye full blood picture...
Umefanya,umepewa report sasa ukipewa hiyo report utaisoma mwenyewe kujua na kuielewa
Si itabidi umrudishie daktari akakusome

Ova
Bwana wewe si anapokea mshahara kutokana na kodi za wananchi.

Private its okay hata consultation fee ikiwa milioni.
 
Kwenye ada umepuyanga. Na wanaosoma Aerospace au aircraft engineering wasemeje.
Mnakurupuka tu.

Fee hio ifutwe.
 
Kupitia uzi huu..
Nmegundua kuwa wabongo wengi hawaelewi vitu vingi kuhusu madaktari na udaktari..

Kubwa kuliko ni kuwa mtoa uzi ulitakiwa ku moderate uzi na kuwarudisha kwenye njia wanao potosha kuhusu mnufaika wa hizo gharama...

Inabidi ieleweke kwamba.

1. CONSULTATION FEE = (gharama ya kumuona daktari) haichukuliwi na Daktari.. Hata madaktari wengi wanaon siyo fair kuwa na amount kubwa hivo. Na mara nyingi utakuta daktari anajitolea hela yake ya mfukoni kumlipia mgonjwa maskini...

2. KUMUONA DAKTARI.. siyo sawa na kumuona mkiwa mna piga gambe, ama kumuona padre ukienda kuungama.. Ile ni sehemu ya Matibabu.. Kama ni kuchangia basi Ni lazima kuchagia sawa na unavyo changia dawa.

3. Kama unaona consultation services siyo muhimu kuchangia.. Basi hata dawa ziwe bure.. Kwa mantiki hiyo hiyo. Kwa maana zote ni aina za Matibabu..

4. Elimu elimu elimu itolewe kwa wagonjwa kuhusu huduma wanazo changia.

Kwa sehemu kubwa mfumo wetu wa afya ni kuchangia na siyo kulipia huduma.


Tujifunze kupitia kisa hiki:

Kuna mgonjwa yeye mwnyewe alijiona kama ana uvimbe usio uma tumboni akijishika.

Aka amua kwenda Hospital ya wilaya. Akalipia gharama za kumuona dokta.. Dokta kambinya binya Ikaonekana ni kweli ana uvimbe tumboni.. Ile hospital haikuwa na ultrasound machine. Ikabidi aandikiwe barua kwenda hospital ya mkoa "for further evaluations and managements"


Kufika hospital ya mkoa, napo akalipia gharama ya kumuona daktari, dokta akamuandikia alipie kipimo cha ultrasound.. Bada ya majibu ya ultrasound akamuandikia barua ya rufaa kwenda hospital ya kanda.


Hospital ya kanda akalipishwa tena gharama ya kumuona daktari.. Na Daktari alipomuona akasema haamini kipimo kutoka hospital ya chini, hata hivyo kuna details hazijatajwa kwenye report hiyo.. Hivyo apime upya kipimo cha ultrasound aongezee na CT - Scan.

Mgonjwa aka hamaki, hela zime isha, uvimbe upo vile vile, na anaona kama hajatibiwa..
Akaanzisha varangati eti arudishiwe hela zake za kumuona daktari.. Kwani daktari haja fanya chochote.

**************
 
Hahahaha

Sio education.

Ila sielewi bado. Hujanishawishi.

Health care ni basic needs.

Inatakiwa itolewe for free au kwa very minimal cost ambayo kila mtu anaweza afford. Over
Kwa sheria ipi Tanzania, unatakiwa kutoa huduma bure. Ukinipa basi naacha ubishi hapa
 
Hii ishu Isikusumbue Sana mkuu hakuna mabadiliko yoyote yatakayotokea. Hili ni suala la cost sharing.. Limeanzia miaka y 80s huko. Sio zuri Kwa wenye kipato kidog zaidi kama mm n wew Lakin tayar lishakuwa zuri Kwa sabb ni kesi y kupata mapato Kwa Serikali.
 
Mkuu, daktari anapokuwa ofisini (wodini) pale ile ndio ofisi yake, kama ilivyo kwa accountant na kada nyingine! ambao wanalipwa mashahara kupitia kodi,
Je, nao wawe wanalipisha wananchi wanao enda kupata huduma za kiuhasibu?
 
Mtu aliyetakiwa apate hela nyingi katika hii dunia, ni daktari;kwa sababu anaokoa maisha yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…