Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

....acha kuishi kwa hisia, na kusikiasikia! Hizo hela kama hajakupa wewe unauhakika gani ndiye anazitoa
 
Haya yote yanapikwa na Timu ya Membe kwa kutumia mapesa ya Marehemu Gadafi na madili mengine ya Pembe za ndovu na wale wawekezaji walioletwa na Membe Kimagumashi nao wanakamuliwa vijicent na Zote kawekeza kwenye kupambana na Lowasa baada ya kubaini ndiye Tishio kwa wale wote wanaowania kuingia ikulu, Membe yupo Tayari ashinde njaa siku nzima lakini Pesa yake ya siku hiyo itumike kumchafua Lowasa hapo roho yake hujisikia rahaa.......

Nyerere amekuwa akisingiziwa Kuwa alimkataa Lowasa wakati si kweli ikumbukwe Kuwa Majungu juu ya Lowasa hayajaanza Leo hata kipindi cha Nyerere yalikuwa yakipenyezwa Pia.

Nchi hii Hakuna Kiongozi aliyekuwa Msafi kiasi cha kumnyooshea mwenzake kidole, wale wote wanaowania kuingia ikulu kila mmoja ana madhambi na mapungufu yake ambayo yanajulikana, Lakini Membe kaamua kuwaacha kakomaa na Lowasa tu kisa eti ndiye Tishio miongoni mwao.
 
Siasa upumbavu mtupu, n wasaa wa vijana kuwaza namna ya kutoka kimaisha Lowassa na Membe hawawasaidii. Mnabshana nyny wenzu wanacheka na kula pamoja!
 
Richmond alipikiwa na nani?

Kwa nini hataki kusema chanzo cha utajiri wake kama ni halali?

Nini malengo yake ya kulazimisha kwenda ikulu, anachokitafuta ni nini? Kama ana nia njema na nchi kwa nini hatuoni lolote analolifanya kwa Watanzania zaidi ya propaganda na rushwa?

Kwa raiis anayetumia nguvu ya rushwa, unategemea atajenga taifa la aina gani?

By the way, hakuna mtu mwadilifu ccm. Hakuna kiongozi bora atatoka ccm. Mtegemee maafa zaidi ya haya yalilyopo.

Lowasa hafai hata kusimama na kuongea haki wala uadilifu. Ni mwizi na fisadi asiye na uzalendo hata chembe.

Ccm bye bye.

Ccm rest in pieces.
 
Mkuu mwana kampeni mpya wa ...Njenga Karume, kwanza karibu jf, pili asante, kuliingiza hili jina Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, mara 14, sio promo ndogo, asante kwa hili!.

Tatu na hili ndilo kubwa kuliko, "maneno huumba!", kama uliotuletea hapa ni kweli tuu, basi asante na utabarikiwa sana!. Lakini kama maneno haya ni uongo, na uzushi, ambao wewe umelishwa tuu na kuja kututapikia hapa, nakushauri, japo umeandika humu, tubu ndani ya nafsi yako, kuepuka adhabu ya kitu kinaichoitwa "karma!".

Una hiari kuufanya moyo wako mgumu, ila kiukweli kabisa, niko very sure 100% sure, "karma!" is real!.

Take it or leave it!.


Kwa wengine msioijua "karma", kama mnamjua huyu
N
jenga Karume in real life, na haswa hawa watu wanaokuja na majina bandi ya wafu waliokuwa in real life, (James njenga karume (1929 – 24 February 2012)) angalieni kitu kitakachomsibu in a near future, mje tuu mtushuhudie ni nini kilimpata!.

Wasifu wa huyu Njenga Karume wetu humu jf,
Alijiunga jf tarehe 26 September, 2014. Tangu amejiunga, ameposti mara 5 tuu, kati ya hizo, 4 ni kuanzisha thread, na hachangii hata neno moja!.

Kwanini lowassa anatumia fedha nyingi kwenda ikulu Started by njenga karume, Today 01:41

Kwanini Kikwete hana imani na Lowassa? Started by njenga karume, 2nd November 2014 10:17

News Alert: Nyerere kumkataa lowassa Started by njenga karume, 1st November 2014 16:51

Lowassa ni timu losser, haifai kuongoza nchiStarted by njenga karume, 26th September 2014 19:48




Pasco
 
Membe Team mtapiga kelele hata lini ? Mnajua membe hana huo ubavu, mtabaki kumwabudu humu JF huku mkipishana na ukweli .
 
Membe is no longer an agenda for consideration in our contemporary CCM politics. We have only two contestants in this holy race these are, Mizengo Kayanza Peter and Edward Ngoyai Lowassa. Plus two anonymous young men whose network within the ruling party is still weak to offer anything for their success
 
Membe Team mtapiga kelele hata lini ? Mnajua membe hana huo ubavu, mtabaki kumwabudu humu JF huku mkipishana na ukweli .

Membe kila akibuni njia mpya wana JF wanamshitukia ! Hivi ni kwa nini Membe asizitumie hizo pesa za Marehemu Gadafi kujenga miundo mbinu kijijini kwao kisha akawapatia Mitaji wana Ukoo wake wote na wale wanakijiji masikini akawawezesha kwa kuwapia mitaji angalau itamsaidia kupata Mvuto wa kisiasa, kuliko kutumia Pesa nyingi kumchafua Lowasa ambaye inaelekea hamwezi Maana kila akimchafua watu wanampigia mayowe kwani wanajua Kuwa yy Membe si msafi kiasi cha kumyoshea Lowasa kidole.
 
Membe is no longer an agenda for consideration in our contemporary CCM politics. We have only two contestants in this holy race these are, Mizengo Kayanza Peter and Edward Ngoyai Lowassa. Plus two anonymous young men whose network within the ruling party is still weak to offer anything for their success
Mkuu Nedese, kiukweli Pinda hautaki urais wala alikuwa hana mpango nao kabisa!, ule tuu u PM kwake ni mzigo, uje umeongezee, si tutamuua bure baba wa watu?!.

Kilichomfanya Pinda asiufikirie kabisa urais, ni kwa sababu yeye by nature ni cleam man na very humble!, anazijua how dirty JK played!, anajua how dirty and crook one has to be ili kuupata urais!, kwa vile yeye sio mtu wa makuu, ameishajitayarisha na kujipanga kujistaafia na pensheni yake, na mashamba yake, na asali yake!.

Baada ya CCM kushuhudia nguvu ya EL, Pinda ameombwa tuu ili kumtumia kuhala,lisha kulikata jina la EL katika hatua za awali kabisa, ndani ya CC ili lisiingie NEC!.

Baada ya kumchinjia baharini EL, kuna watu wengine wawili watalazimishwa kuingia kwenye race, ambao ni "The choosen one", na "the Zanzibar pace maker!", yaani yule ambaye wamemdhamiria ndio awe rais wa 2015, na mgombea mmoja weak kutoka Zanzibar prefarably Gharib Bilal, ila majina hayo matatu, Pinda, The Choosen One and boya la Zanzibar, no yatatinga Mkutano Mkuu wa CCM. Huko amini usiamini Pinda atajitoa na kusema kura zangu mpeni "the choosen one!. Na Gharib pia atajitoa vyivyo hivyo!. Pia wanaweza kubaki, ili kuithibitishia jumuiya ya kimataifa kuwa CCM ni chama cha kidemokrasia!, lakini kura za ushindi ni kwa the choosen one!.

EL akishakatwa, atakuwa under survailance 24/7 asije ku defect na kuimiza CCM!, na wakiona kuna dalili yoyote ya defection, "watamaliza kazi!", kwani Dr. Omar Ali Juma, ilikuwaje?!, tena Jumbe ana bahati sana, alifanya upuuzi ule chini ya Nyerere, mcha Mungu na mtu wa Imani, EL asipojiangalia kwa makini, kufika kwake October 2015 ni majaaliwa sana!.

Haya ni maoni yangu tuu, "no inside trading yoyote!".

Pasco.
 
Lowasa ndo kiongozi maana yeye si fisadi wa nchi hii,usimchafue kwa vile wewe hajakuhusisha
 
kwanini wewe hupendi lowasa awe rais?una roho ya kishetani
 
CCM inapita katika tanuru la moto. Ikitokea kwamba Lowassa hajapitishwa sijui nini kitatokea, amekamata kila mahala kuanzia makanisani, misikitini, ndani ya CCM hadi wapinzani.

Si asipopitishwa na CCM mtampitisha UKAWA?
 
hafai hata robo kuwa rais na ammiri jeshi wa tanzania. Hafai hafai hafai hata robo.
Ile clip aloitoa makonda ndo itakuwa kampeni ya ukawa. Na ile clip kila mtu anayo na itapeperushwa nchi nzima wala ukawa hawatapiga kampeni
 
LAKINI JE? ALIMKATAA LOWASSA PEKEE "wakati ule lowassa na kikwete walipopanda ndege moja kwenda dodoma 1995" mwl jk ktk utawala wake aliwahi kusema ktk awamu yake kuna mazuri na mabaya shikeni mazuri acheni mabaya! pia haiwezi kuwa ajabu ktk mabaya aliyoyakosea ni kauli @yake! kwa LOWASSA, mwl alikuwa ni mwanadamu hakuwa mungu!
 
Last edited by a moderator:
"Mtanzania wa leo hawezi kununua watu kabla ya yeye hajanunuliwa!!!". Mwl JK Nyerere.

JE, NGOYAI ANANUNUA WATU ILI KWENDA IKULU? KAMA ANUNUA WATU ATALIPAJE HIZO PESA ANAZOGAWA?

"Ikulu ni mahali patakatifu, anaye kimbilia ikulu niwa kuogopwa kama ukoma" "Kwa mtu mwaminifu kabisa, Ikulu ni mzigo, si mahali pa kukimbilia hata kidogo". "Mimi nimekaa Ikulu miaka 21, kuna biashara gani pale Ikulu?. Mwl JK Nyerere"

" Mara hii tu mmetajirika kiasi hicho? Kama mmeweza kutajirika kiasi hicho katika muda mfupi, fanyeni basi wote tutajirike, kwa nini mtajirike peke yenu?!". Mwl JK Nyerere.

JE KUNA WATU WANAPAKIMBILIA, JE KUNA WATU WAMETAJITIRIKA MUDA MFUPI BAADA YA KUINGIA MADARAKANI? KAMA NI KWELI BASI HATA SISI TUNAHITAJI MAISHA MNAYOISHI.


"Kiongozi atakayepokea rushwa, tukimkamata tutamfunga miaka miwili na atapigwa viboko 24; 12 akiingia na kumi nambili akitoka, aende akamwonyeshe mkewe. Mwl JK Nyerere.

JE, AKINA MLAMBA, YONA, CHENGE, MAMA TIBAIJUKA WACHAPWE VIBOKO?
"Katika nchi kama yetu, ambayo Waafrika ni maskini na wageni ni matajiri, kuna uwezekano mkubwa kwamba Mwafrika akiruhusiwa kuiuza ardhi, katika miaka themanini au miaka ijayo, ardhi yote ya Tanganyika itamilikiwa na matajiri wageni, na wenyeji watakuwa watwana. Lakini hata kama wageni wasingekuwa matajiri, litaibuka tabaka la Watanganyika matajiri wajanja. Tukiruhusu ardhi iuzwe kama kanzu, katika muda mchache, kutakuwa na kundi dogo la Waafrika wakiwa na ardhi na walio wengi watakuwa watwana." NYERERE, 1958

JE ARDHI INAUZWA KWA WAGENI? NI NANI ANAUZA HIYO ARDHI?

"Watanzania wanataka mabadiliko; wakiyakosa ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM"
Julius Nyerere, Dodoma, 1995. . Mwl JK Nyerere.

NI KWELI WATANZANIA WANATAKA MABADIRIKO? KAMA NDIYO NANI ANAYASIMAMIA?
"Nang'atuka, lakini bado nasisitiza kuwa, bila CCM imara nchi yetu itayumba" 1990s. . Mwl JK Nyerere.

JE, CCM NI IMARA? KAMA SIYO IMARA NANI ANAIYUMBISHA?

"Serikali ikitawaliwa na rushwa haiwezi kukusanya kodi, itabakia kukimbizana na watu wadogo wadogo tu". Mwl JK Nyerere.

JE? NI KWELI SERIKALI INAKIMBIZANA NA WATU WADOGO WADOGO? SETH WA IPTL NA WENZAKE WAMELIPA KODI?
 
Ulikuwa na hoja isipokuwa umechanganya mambo mengi
 
Nyerere angekuwa hai angeshaitosa CCM,mengi aliyoyasema yametokea kabla hajafa ingawa sasa ndo yametamalaki.
 
Back
Top Bottom