Mh. Pinda; Mbunge wa CCM atakayetetea kura ya siri atanyang'anywa kadi!

Mh. Pinda; Mbunge wa CCM atakayetetea kura ya siri atanyang'anywa kadi!

Finally viongozi wa CCM wameamua kulinda misimamo yao, taasisi zipo kwa sababu ya malengo fulani haiwezekani taasisi ambayo hipo kwa sababu ya kutoa elimu kuhusu uzazi wa mpango, elimu kama hiyo inaendana na vitu kama contraception nakadhilika halafu atokee member ambae kwa imani zake za kidini anapinga mbinu hizo na kutaka wazazi wajiamulie wenyewe. Swali la kujiuliza alienda kujiunga na kundi kufanya nini wakati anaelewa kabisa wapo kwa makusudi ya kuzuia uzazi usio na mpango in the first place na precautions ni njia moja wapo ya kutoa somo.

CCM kama chama cha siasa pia kina misimamo yake haiwezekani wanachama waone misimamo ya chama haifai unajiuliza walijiunga kwa sababu gani kama hawakubali foundation za chama ambacho ni zao la TANU na ASP mpaka leo watake vingine. Watu hawawezi kukurupuka na matatizo yao ya maisha waingie siasa bila ya kuvielewa vyama vya siasa na kutotaka kuheshimu misingi ya chama, na kama CCM wakiendelea kulea wanachama wa design hiyo ujue misuguano na malumbano haitoisha lazima kuwe na discipline within na wanachama kufuata misimamo ya chama navyojua mimi si tu vyama vya siasa bali taasisi zote sheria/kanuni/misimamo lazima zieshimiwe duniaini kote si Tanzania tu.

Wajumbe la bunge la katiba waache akili za kitoto kura ya siri ni akili za mimi nachotaka na kusimamia, wakati wajumbe wanaulamzima wakuwafahamisha wapiga kura wao na wanamakundi wenzao wamechagua nini na si nafsi zao zinataka nini ndio siasa zenyewe ppl have to compromise for the good of many ie political party.

wewe bongo lala kwani katiba ya nchi inaandikwa na vyama?
=============you are a diplomatic fool=============
 
Kikwete aliwahi kujinasibu kuwa atawaachia Watanzania katiba mpya itakayotumika kwa miaka 50 - 100 ijayo lakini kwa hali ilivyo ni wazi kuwa hata hili limeshamdodea kama alivyoshindwa pia kutatua kero za muungano mbali na majigambo aliyoingia nayo mwaka 2005 juu ya kero hizo.
 
WITO KWA WABUNGE WA BUNGE MAALUMU WAPENDA MABADILIKO YA KATIBA,CCM WAKIPITISHA KURA YA WAZI BASI MMUONDOKE BUNGENI MUWAACHE CCM WAJITENGENEZEE KATIBA YAO YA CHAMA.full stop ni kupotezeana muda kama niya thabiti ya kuwa na katiba mpya
Hizi ni hoja nyepesi zinazoonyesha ni jinsi gani hamkujipanga na hamfahamu hata utaratibu wa ulioko katika bunge la katiba.

Kama mnadhani kura ya siri ndiyo dawa ya tatizo lililopo basi inafaa tu kurudi majumbani kwao.

CCM inaweza ikawapa hilo dai lenu la kura ya wazi ili mjikaange wenyewe kama ilivyowapa kuhusu uchaguzi mwenyekiti wa bunge, Mh. Sitta.

CCM kila wakiweka ndoana ya kisiasa mnaikimbilia na kuimeza. Unapokaa mpaka swala linapitiswa ndiyo unaanza kulalamika ni dalili mbaya kisiasa ya kuonyesha kuwa hafamu hata kinachoelekea kufanyika.

Haya ni mawazo yaliyojisimika kwenye reactive mentality badala ya proactive mentality.
 
Tunataka kura ya wazi kila mtu atusikie tunafanya nini kwenye bunge la katiba hakuna cha usiri hapa mambo yote wazi.

Nyie Mamburula wa ccm kama mnataka kura ya wazi kwenye Katiba na uchaguzi mkuu nao mpitishe kura ya wazi pia,
 
Kikwete aliwahi kujinasibu kuwa atawaachia Watanzania katiba mpya itakayotumika kwa miaka 50 - 100 ijayo lakini kwa hali ilivyo ni wazi kuwa hata hili limeshamdodea kama alivyoshindwa pia kutatua kero za muungano mbali na majigambo aliyoingia nayo mwaka 2005 juu ya kero hizo.
Kwani hii nchi ya jk peke yake kwa akili yako wewe hata kama ungemwagiwa mafuta ya taa kichwani na kuwashwa kwa kiberiti usingeweza kubadilika kabisa make wewe unaamini kuwa jk anapaswa kufanya kila kitu kumbe mambo mengine yanahusu jamii yote kwa pamoja.
 
Nyie Mamburula wa ccm kama mnataka kura ya wazi kwenye Katiba na uchaguzi mkuu nao mpitishe kura ya wazi pia,
We kitasa kweli hapa tunapiga kura kupigia katiba hatumpigii mtu wewe kwa vile hunaakili unadhani hii ni kura udiwani au ubunge kwa nini bavicha hamna akili?
 
Mheshimiwa waziri mkuu, Mizengo Pinda ametangaza kwenye kikao kilichowashirikisha baadh ya wabunge wa ccm kuwa atakayetetea kura ya siri atanyanganywa kadi ya chama! Vigezo na masharti yazingatiwe.

Ha haaa ni mnkwara tu hawana ubavu huo.., waziri mkuu wetu tunamjua hana historia hio...
 
wewe bongo lala kwani katiba ya nchi inaandikwa na vyama
Chama cha siasa ni mkusanyiko wa watu wenye nia ya kuongoza taifa (na ambapo wananchi wana matakwa mengi na yanayotofautiana), kwa hivyo vyama vinachaguliwa na wananchi kwa kuelewa misimamo yao na sera zao. Waliopo bungeni wapo pale kwa niaba ya mimi na wewe kupitia chama, inachofanya CCM si kwamba inalinda maslahi ya chama tu bali na wapiga kura wao waliowachagua kwa kukielewa chama.

Kama mpiga kura kwakuwa sikupata kura ya maoni wala kuhojiwa kuhusu katiba, ni vyema chama nilichokipigia kura kilinde kilichonifanya kukipigia kura chaguzi zilizopita na popote maslahi yangu yanapo zungumziwa including kwenye bunge la katiba. Sasa wasitokee wanachama wenye misimamo tofauti ambayo aikuwa kigezo changu cha kumpa kura mwanachama wao hili aende kuniwakilisha, maana kuna vyama vingine vinavyojinada kwa mwendo mwengine ningeweza wapa kura yangu. Kwa maana hiyo kura ya siri ni kunilaghai mpiga kura nataka kujua umechagua nini kwa niaba yangu na kama ni zile sababu zilizonifanya nikipe kura chama chao na mwakilishi wangu. Vilevile chama cha siasa kina haki ya kulazimisha wanachama wake kulinda kanuni na misingi yao inayojinadi nayo kwa wananchi.
 
WITO KWA WABUNGE WA BUNGE MAALUMU WAPENDA MABADILIKO YA KATIBA,CCM WAKIPITISHA KURA YA WAZI BASI MMUONDOKE BUNGENI MUWAACHE CCM WAJITENGENEZEE KATIBA YAO YA CHAMA.full stop ni kupotezeana muda kama niya thabiti ya kuwa na katiba mpya

Tatizo ni kuacha posho Mkuu. Kusingekuwa na mambo ya posho, hilo unalolisema mbona linawezekana tu.
 
Tunataka kura ya wazi kila mtu atusikie tunafanya nini kwenye bunge la katiba hakuna cha usiri hapa mambo yote wazi.

ccm sera ya uwazi wameitoa wapi? mpaka macho yanawatoka wanataka kura za wazi, ili twende vizuri tunaomba mikata yote ya madini iliyopita iwekwe wazi.
 
Mheshimiwa waziri mkuu, Mizengo Pinda ametangaza kwenye kikao kilichowashirikisha baadh ya wabunge wa CCM kuwa atakayetetea kura ya siri atanyanganywa kadi ya chama! Vigezo na masharti yazingatiwe.
Hebu tuambie hapa jukwaani msimamo wako ni nini na utupe sababu za huo msimamo wako. Nitafurahi sana nikipata jibu ambalo sio la jazba wala kejeli.
 
Hebu tuambie hapa jukwaani msimamo wako ni nini na utupe sababu za huo msimamo wako. Nitafurahi sana nikipata jibu ambalo sio la jazba wala kejeli.

kura ya wazi. Kwa7bu hyo katiba siyo ya siri.
 
kura ya wazi ndo mpango maana katiba ni ya watz. Hiyo mikataba mnayozungumzia ni mambo mengine.

Kama katiba ni swala la wazi mbona hamtaki
Waandishi wa habari waingie kwenye ukumbi
Wa kamati mnaficha. Nini Kama ninyi ni waumini
Wa uwazi mtajibeba watanzania sio tena mabwege.
 
Back
Top Bottom