Mh. Zitto kuna ukweli gani katika ripoti hii?


Honestly. Nimesoma hiyo habari yote hapo juu sikuona pabovu. Nilidhani Zitto alipata faida binafsi kuoka Barrick kumbe ni msaada, tena wa mabati ya shule ya sekondari. Hivi Watanzania wanajua hawa jamaa wanatuibia kiasi gani? Sembuse huo msaada kidogo? Na msaada unapelekwa kwenye halmashauri ya Wilaya, si kwa ofisi ya mbunge.

Zitto kaza buti mwanangu....Maana mti wenye matunda ndio utupiwao mawe!
 
Nasubiri tuu majibu ya Zitto kwenye post hii ndipo nijilalie, namuona yuko on line.
Mhe. Zitto semo neno moja tuu roho zetu zitulie! Angalau sema ulizisambaza hizo proporsals sehemu kadhaa ABG wakiwemo, ila waliojibu ni ABG.
Mkuu wangu hata kama... Kwa Usd 10,000 sidhani kama Zitto mwenyewe alishindwa kuzipata. Hata kwa kupitia Mabillioni ya JK mbunge unaweza kucheza nazo zikaenda kuboresha shule zako. na ikija julikana ulifuja fedha ya JK, wananchi watakupa support zaidi kwa ujasiri uloufanya kuwekeza fedha hizo ktk elimu, lakini hii ya Barrick kusema kweli wakati mwingine mkuu wangu Zitto hufanya maamuzi ya ajabu sana hasa naposikia kwamba ni yeye aliyekwenda kuomba msaada Barrick..Ni kwa njia hizi za misaada Kina Jeetu Patel na Rostam huwakaweka mfukoni viongozi wa serikali..Na Zitto kama anategemea kuwa rais huko mbele ni muhimu afahamu hata nchi za magharibi hutumia misaada kama hii kuwaweka kibindoni marais wa nchi maskini.
 
Kilicho na kinachomponza Zitto ni umaarufu na ufisadi. Mtu anayepiga kelele ili aunganishwe kwenye ulaji ni mbaya sana. Na kwa hili na mengine yaliyojificha Zitto hana tofauti na walafi wengine, pengine tu yeye amekosa channel ya uhakika. Kuna dalili zote kuwa akipata nafasi huyu kijana hawezi kuiachia hata kidogo.

Baada ya kuanzisha ule mpambano wa madini na kupata umaarufu mkubwa Rais alipo amua kumpa nafasi na yeye kula kupitia ile kamati jamaa hakubisha, aliporudi bungeni kutoa ripoti tone yake ikabadilika kabisa. Akaanza kuonekana kuzungumza zaidi kwa busara kwa kuwa alishakula chake cha juu.

Alipoenda Rais kufungua barabara huko kijijini Kigoma jamaa ndo akawa amekwisha kabisa utafikiri barabara ilikuwa ni favour wakati yeye anatambua hilo ni jukumu la serikali na hata hivyo kwa wale wapiga kula bongo lala ikaonekana kuwa ni juhudi zake binafsi zilizofanya hilo.

Nikielekea upande wa ndani wa chama chetu cha CDM mambo ni yale yale. Ukikuta mtu mnaye kwenye chama kimoja na yeye kila siku anakuwa na mawazo tofauti na chama ujue hilo ni tatizo. Mimi nijuavyo mtu unakubaliana na chama kwa kufuata itikadi na upambavu wake wote. Kama hukubaliani nacho then achana nacho either unahamia kingine au unaanzisha chako ambacho unajua kinakubaliana na malengo yako.

Ukirejea siku aliyotamka Bungeni kuwa Spika Makinda anaendesha bunge vizuri sana hiyo ilikuwa ni dharau kwa wenzake kama kina Lema, Lissu, Msigwa na wengineo ambao wamekwaruzana mara kadhaa na Spika huyo. Kwa ufupi ni kusema kuwa wenzake wa CDM ni wahuni bingeni kwa kuwa ndo wanaomkorofiisha Makinda.

Sasa lipo wazi kwa nini wabunge wa CDM wanapingana kuhusu posho za vikao. Yeye hataki kuchukua kwa kuwa kuna wengine wanao muwezesha wakati wenzake Bungeni ni sehemu ya kujipatia kipato.

Kijana think twice!
 
Lakini kama barrick walipeleka maendeleo ya elimu kigoma nazani waliisaidia serikali, kibaya hapo ni uwazi. je huyo mbunge wa huko buzwagi hafahamu au naye kala murungura?
 

Kweli mimi ninakushangaa sana FOXY. Je hizo hela alizichukua yeye akaweka mfukoni au zilipelekwa kwa watoto wa masikini? Pili Kuna ubaya gani msaada wa barrick kwenda kigoma. Mbona kuna misaada ya watu mbalimbali inakwenda mpaka Somalia wakati wamechuma Tanzania. Hili tunaliona tatizo kusaidia watanzania wenzetu. Wewe FOXY una matatizo sana kila wakati nikisoma maelezo yako ninaona umetumwa kupinga kila kitu kinacho tolewa na upinzani. Angalia usije ukawa kama lilivyo jina lako maana kwetu FOXY ni malaya.
 

Na wewe una matatizo kumtwe. Hivi unamlaumu hizo fedha alitumia yeye na familia yake au walipewa watanzania kama ambavyo akina Mengi na Bahrasa waanapeleka misaaada kwa watu mbalimbali ndani na nje ya nchi? Poleni sana.
 
Wabunge wanapotaka kuwa tendaji ni kosa kubwa.
  • Mbunge akiwa mtendaji lazima kutakuwa na conflict of interest
  • Mbunge akinzisha na kumanage NGO hata kama nia yake ni nzuri tayari atajikuta kwenye mamtatizo sababu NG zinahitaji misaada
  • Mbunge kupewa Fund ya CDF na serikali n kuimanage ni kosa. Subirini labda CAG afunike funike akiazna kukagua pesa za hiyo mifuko
Nawachowashauri wabunge wakizidi kujisahu watajikuta wao ni version B ya sirikali.
 
Reactions: EMT
Bila kuwa na Tanganyika haya hayawezi kwisha, Natamani nimsikie Zitto kwa hili lakini moyo wangu unaogopa maana zitto ni mwanasiasa na atakuja kisiasa... Hivi kweli wanasiasa huwa wanalala kwa amani usiku huku wakijua kuwa mchana kutwa wameongea uongo hata kwa mtu ambae hata hana chakula?
Ni bora kupokea posho zilizofanyiwa kazi na masaburi kuliko hili
 
Miongoni mwa mbinu wanazotumia CCM kuwanyamazisha Wabunge wanaopiga sana kelele ni kuwapa ulaji e.g. Uwaziri,uenyekiti wa bodi,kuongoza kamati na kadha wa kadha,sasa ndugu yetu,mbunge wetu mpendwa ameisoma vizuri hiyo teknik na kuifanyia kazi ya kulipua mabomu mjengoni na kupiga sana kelele mpaka jamaa wakamwona na sasa anakula kuku kwa gharama ya jasho na damu za Wadanganyika,hata hiyo nafasi ya uenyekiti wa kamati anayoiongoza jamaa pale magogoni alitoa amri kwamba lazima jamaa apate kamati.
 
Mheshimiwa Zitto, ahsante kwa majibu yako. Jana nilisema kuwa utakapokuja kujibu lazima utajibu kifasaha kabisa, na ndivyo ulivyofanya. Nadhani ni vyema Wanajamvi tukaweka maslahi ya Taifa na uzalendo mbele kwanza kuliko chama cha siasa. Ikiwa kama Kampuni binafsi ikampenda mwakilishi mmoja pale mjengoni, na wakasema tutakujengea barabara jimboni kwako au tutakuchimbia visima au tutaleta mashine za irrigation au vitanda vya hospitali, kwakweli hakuna tatizo lolote kama vinakwenda kwa watanzania wenzetu. UZALENDO.
 
Na kwa akili hizi kina Mandela wasingeweza kuikomboa South Afrika maanake walijengewa kuliko hata hizo barabara za vumbi..Halafu basi mnosema haya ni Wapinzani wakubwa wa Ghadafi ambaye kayafanya mengi sana mazuri Libya, lakini kitu ambacho wote hapa hatukubaliani ni uongozi wa kimaguvu na kwa miaka 42. Ukiweza kulitazama swal hili kwa jicho hilo utaelewa sisi wapenzi wa Zitto tunalalamika kitu gani?
 
Mkandara

Wakumbushe kuwa kina Mandela walikataa ku appeal kifungo cha maisha kwa kuhofia kuonekana wanaupinga utawala wa kaburu kisha wanauomba favor ya appeal (ambayo kimsingi ni haki yao) Itakuwa msaada Wa dola elfu kumi?
 
Hao wa pande za huko wamelala tuu!!!!!!!!!
Sasa zito afanyaje wao wanakazi ya ndiooooo
kwani wapo bungeni kwa ajili gani sasa?
Kama zitto kaweza na hao wa pande za huko wanafanya nini bungeni sasa?
Maendeleo hayakufwati unayatafuta mwenyewe alaa
 
Mkandara<br />
<br />
Wakumbushe kuwa kina Mandela walikataa ku appeal kifungo cha maisha kwa kuhofia kuonekana wanaupinga utawala wa kaburu kisha wanauomba favor ya appeal (ambayo kimsingi ni haki yao) Itakuwa msaada Wa dola elfu kumi?
<br />
<br />
ngoja wajisahulishe historia wakati ndo'itakayo wahukumu!
 
Hapa inavyoonekana barrick walimzunguka zitto, zitto akawa naive kwa motives zao akadhani ni wema , sijui kwa nini hakujiuliza why kigoma? Na si ibwera bukoba?- jibu ni simple, kwamba kigoma kuna mbunge anayehatarisha maslahi yao, na kwa kwa hivyo basi "penye udhia, penyeza rupia"- sisi third world countries tuko so naive inapokuja katika namna ya kudeal na international corporates,international ngo's, diplomatic entities, n.k.
Ni vizuri wanasiasa wetu na watu kiujumla wakafahamu principle hii. "kwa kila jambo ambalo international institution zinalolifanya, the ulterior motive ni kwamba wao watanufaika vipi, suala la wewe utanufaika vipi ni juu yako, kwa hiyo inabidi ucheze smart". Vijimsaada vingine ni chambo tu, kama vile ambavyo unahitaji ka chambo kadogo kulivua lisamaki likubwa basi ndivyo hawa majamaa yanavyofanya kututeka na kutuibia rasilimali zetu".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…