Kwenye katiba inasema, maandamano ni haki ya mwananchi, ila ss hawa viongozi vichwa panzi hukutaka tu hata kuongelea swala la maandamano wanakasirika wanataka wakupoteze. Ss hapa picha linaanza hapo tu sehemu kesi ilipofunguliwa, mahakama ya mwanzo, yenyewe Haina uwezo wakusikiliza kesi, mtu unaanza kupiga tarehe
Mi sijui nivigezo gan huwa vinachukuliwa mtu kushtakiwa kesi ya ugaidi, coz lately zimekuwa ndio kesi zinazoongoza ikiwa nipamoja na kuhujumu uchumi. Hii yote ni ile sababu yakutokuruhusu mshtakiwa apewe dhamana
Yaan kila kitu hapa kimetengenezwa ili mtu ateseke kuanzia kisaikolojia, hamna explanation ingine, yaani nikukandamiwa tu hamna explanation ingine.
Ona kituko kingine, unamkumbuka mchimbi amesema mm juzi hapa, na Nini kinaendelea. Ss hapo ndio ujue wananchi tunavyopelekeshwa kama mafala
Kiufupi viongozi wa hii nchi wanatudharau sana sisi wananchi
Kama Waswahili wanavyosema " Mungu si athumani, na wala hanywi chai ya rangi"
Ipo siku tu
#hatujasahau29Oct
#hatusamei29Oct
#backbenchers