Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika

Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika

Halafu issue ya " technical compatibility" inashughulikiwa vipi? Hivi vipande vitatu vitaoanishwa vipi mbele ya safari?
Umeliweka kwa kingereza ili lionekane ni swali fikirishi ila umeuliza issue ya kitoto sana.. Kwamba reli itashindwa kuunganishwa kisa imejengwa vipande vipande! So ujenzi wa reli ni lazima ujenge moja kwa moja?
 
Ili iwe Rais kufikia Nchi jirani haraka

Sent using Jamii Forums mobile app
..hebu angalia ramani ya sgr hapo chini.

..tutafikia nchi gani jirani ikiwa tumeruka kujenga kipande cha Dodoma -- Tabora -- Isaka?

.
1611244723654.png
 
..hebu angalia ramani ya sgr hapo chini.

..tutafikia nchi gani jirani ikiwa tumeruka kujenga kipande cha Dodoma -- Tabora -- Isaka?

.
View attachment 1682748
Kwa sasa Kenya na Tanzania zinashinda speed ya kuyafikia masoko yao.

Uganda ilishindwa kukamilisha reli yao na Kenya kwa sababu Kenya walishindwa kujenga reli yao hadi Malaba.

Hadi Sasa Isaka Kuna Dry Port inayolisha Rwanda, Burundi, Congo, na Uganda.

Kwa sasa Tanzania inafanya miradi mingine sambamba na SGR
1. Upanuzi wa Bandari ya Dar Es Salaam
2. Ujenzi wa Bandari Kavu Pwani
3. Ujenzi wa Bandari kavu Dodoma.
4. Ujenzi wa Meli Ziwa Victoria

Kwa sasa Tuna Phases 2 moja Dar hadi Moro na Moro hadi Singida...

Maana yake chini ya Masaa 6 tutaweza kusafirisha mizigo ya Nchi hizo hadi Dodoma kwenye Bandari Kavu Baada ya hapo tutasafirisha mizigo kwa mabasi au MGR hadi Mwanza na Isaka tayari kuelekea Nchi wateja wa Bandari yetu.
Kwa maana nyingine ndani ya Siku moja tutakuwa tumefika Rwanda na Burundi.

Usafiri wa Bei nafuu yaani Meli kutoka Mwanza hadi port Bell ni wastani wa masaa 17 kama sijakosea kwa sasa... Ila kipindi cha hivi karibuni Serikali imewekeza sana kwenye Ujenzi wa Meli Kubwa ndani ya Ziwa Victoria.

Kama Tanzania itakuwa na Kipande Cha Mwanza to Isaka kabla ya Naivasha to Malaba maana yake Uganda kuchukua Mizigo kupitia Bandari ya Dar Es salaam itakuwa haraka, nafuu na effecient. Na kuwashawishi kuanza kujenga Reli kutokea Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sasa Kenya na Tanzania zinashinda speed ya kuyafikia masoko yao.

Uganda ilishindwa kukamilisha reli yao na Kenya kwa sababu Kenya walishindwa kujenga reli yao hadi Malaba.

Hadi Sasa Isaka Kuna Dry Port inayolisha Rwanda, Burundi, Congo, na Uganda.

Kwa sasa Tanzania inafanya miradi mingine sambamba na SGR
1. Upanuzi wa Bandari ya Dar Es Salaam
2. Ujenzi wa Bandari Kavu Pwani
3. Ujenzi wa Bandari kavu Dodoma.
4. Ujenzi wa Meli Ziwa Victoria

Kwa sasa Tuna Phases 2 moja Dar hadi Moro na Moro hadi Singida...

Maana yake chini ya Masaa 6 tutaweza kusafirisha mizigo ya Nchi hizo hadi Dodoma kwenye Bandari Kavu Baada ya hapo tutasafirisha mizigo kwa mabasi au MGR hadi Mwanza na Isaka tayari kuelekea Nchi wateja wa Bandari yetu.
Kwa maana nyingine ndani ya Siku moja tutakuwa tumefika Rwanda na Burundi.

Usafiri wa Bei nafuu yaani Meli kutoka Mwanza hadi port Bell ni wastani wa masaa 17 kama sijakosea kwa sasa... Ila kipindi cha hivi karibuni Serikali imewekeza sana kwenye Ujenzi wa Meli Kubwa ndani ya Ziwa Victoria.

Kama Tanzania itakuwa na Kipande Cha Mwanza to Isaka kabla ya Naivasha to Malaba maana yake Uganda kuchukua Mizigo kupitia Bandari ya Dar Es salaam itakuwa haraka, nafuu na effecient. Na kuwashawishi kuanza kujenga Reli kutokea Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app

..nadhani tungejitahidi walau kujenga sgr toka Dar mpaka Isaka dry port.

..kwa jinsi ulivyoelezea hapo juu siamini kama kutakuwa na efficiency ktk kusafirisha mizigo.
 
21 Jan 2021
Kisarawe, Pwani
Tanzania

SERIKALI YA KIJIJI KISARAWE YAZUIA MAGARI YA UJENZI SGR “TUNADAI BILIONI SITA”


Mara ya mwisho kijiji kililipwa Oktoba 2018.
Serikali ya Kijiji cha Kibwemwenda imeyazuia kufanya kazi magari ya Kampuni ya Yapi Merkezi ambayo inahusika na ujenzi wa SGR kwa kile wanachodai kuwa hawajalipwa Bilion 6 za ushuru kutokana na mawe, kokoto na kifusi kuchimbwa kijijini kwao. “Wanachukua hapa mawe, kokoto na kifusi, walilipa ushuru tukapata Mil 92 tukajenga Zahanati na nyumba ya Mganga, material ya kutengenezea Reli wanayachukua hapa, Rais kama anasikia kama wanachukua bure aseme ni bure ila kama wanapaswa kulipa walipe” - Idi Zanga, Mwenyekiti wa Kijiji “Tunawadai sio chini ya Bilioni 5 ni Bajeti ya miaka miwili ya Halmashauri yetu, tu nataka tuipate ili tufanye shughuli za kimaendeleo” -Mkurugenzi wa Halmshauri
Source : millard ayo

Mrema, Natumai serikali kuu itawasikia wananchi hawa wa Kijiji cha Kibomwenda ili wapate haki yao stahiki. Ni haki yao wanufaike na mradi mkubwa wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railways🚂🚃. Kampuni ya YAPI MERKEZ toeni fungu la fedha ili mlipe ushuru wa mapato ya madini ya Ujenzi katika Halmashauri ya Kisarawe ili asilimia 20% iende kwenye Kijiji hicho itasaidia kujenga miradi mbalimbali kama Shule, Hospital, Maji, Umeme na barabara kama kumbukumbu ya mradi huo mkubwa kabisa Afrika.
 

January 30, 2021​

Mwanza, Tanzania

SEKTA BINAFSI TANZANIA KUPITIA KONGAMANO LA FURSA ZA MRADI WA SGR MWANZA ISAKA KILOMITA 341, WAJITOKEZA KUSHIRIKI KTK MRADI HUU KIPANDE CHA SGR MWANZA - ISAKA


Wafanyabiashara waTanzania wajadili fursa ktk mradi wa SGR reli kipande cha kutoka Mwanza mpaka Isaka utakaogharimu dola za Kimarekani U$ 1.32 bilioni sawa na shilingi trilioni za kiTanzania 3.06 .

Wadau hao wa Maendeleo wa Ndani hawataki tena kubakia watazamaji wakichungulia kwa mbali na kuachwa nyuma kufaidi na kushiriki ktk fursa zinazoletwa wakati wa utekelezaji wa miradi mikubwa ya ujenzi wa miundo-mbinu. Kongamano hilo linafanyika ktk ukumbi wa Benki Kuu wa jijini Mwanza, Tanzania.

Kongamano hilo ni la aina yake ili kuhakikisha wadau wa maendeleo wa ndani kupitia makampuni yao ujuzi wao kushiriki moja kwa moja toka spedi/chepeo la kwanza linakita ardhini kuashiria mwanzo wa ujenzi wa reli ya SGR kipande cha Mwanza mpaka Isaka.

Wadau wa sekta binafsi Tanzania kupitia shirikisho lao la TPSF, wasafirishaji na mabenki ya ndani watajadiliana namna ya kutumia fursa hiyo Mpya ya kipande cha reli ya SGR itapoanza kujengwa na wao kushiriki kufaidika kuingiza pesa wakati ujenzi huo utakapokuwa unaendelea ambapo wadau wa nje yaani makampuni mawili ya China Civil Engineering Construction (CCEC) na China Railway Construction Corporation (CRCC) toka China yameshinda tenda ya Sh trilioni 3.06 ya ujenzi wa kipande hicho kama waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi alipobainisha alipofika mwanzoni wa mwezi January 2021 mjini Chato, Geita Tanzania.

Chinese companies win $1.32bn Tanzanian rail contract​

8 January 2021 (Last Updated January 8th, 2021 16:23)
The Tanzanian Government has awarded a $1.32bn contract to two Chinese companies for the construction of a 341km rail line : Read more source : Chinese companies win $1.32bn Tanzanian rail contract

Source : TRC RELI TV

Soma zaidi kuhusu mradi huo wa SGR reli kipande cha Mwanza - Isaka kilivyowasukuma sekta binafsi Tanzania kuhakikisha nao wanashiriki :


Yametimia: Mkataba ujenzi wa SGR Mwanza- Isaka wasainiwa​

jamvilahabari
jamvilahabari
3 weeks ago
AADB15DD-0D7F-4035-89DA-56831E3BCDBB-871x1024.jpeg

NA JONAS MUSHI, DAR ES SALAAM
Tanzania na China zimetiliana saini ya mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) katoka Mwanza hadi Isaka yenye urefu wa kilometa 341 ambayo itajengwa na kampuni kutoka China.

Hafla ya utiaji saini wa mkataba huo ilifanyika jana wilayani Chato mkoani Geita na kuhudhuriwa na Rais wa Tanzania Dk John Magufuli na Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi.

Akizungumzia kuhusu mradi huo Rais Magufuli aliwataka wakandarasi wa China kuujenga kwa haraka na kuiomba Serikali ya China kutoa mkopo nafuu kwaajili ya kipande cha Isaka-Makutupora.

Ujenzi SGR kipande cha Mwanza hadi Isaka utatekelezwa kwa miezi 36 kwa gharama ya shilingi trilioni 3.0617. Kwa kusainiwa kwa mkataba huu, Serikali itakua inatekeleza mradi wa SGR katika eneo lenye urefu wa KM 1,063.

Kwa upande wake Waziri Yi alisema uwepo wa Rais Magufuli katika tukio hili la utiaji saini wa mkataba huo unaonesha umuhimu mkubwa ambao Rais anaupa ushirikiano na urafiki uliopo kati ya nchi hizi mbili.

“Nachukua fursa hii kuyaagiza makampuni ya China yanayotekeleza miradi hapa nchini Tanzania kutekeleza miradi hiyo kwa kuzingatia kwanza maslahi ya Tanzania,” alisema Yi.

Awali akielezea kuhusu mradi huo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk. Leonard Chamuriho, alisema Serikali inatekeleza kipande cha tatu cha ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza .
Chamuriho alisema mkataba huu utatekeleza kwa muda wa miezi 36 kwa gharama ya Sh trilioni 3.06 ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/25 na mpango wa maendeleo ya Taifa wa miaka mitano.

“Ni jambo la faraja kwamba utiaji saini huu unafanyika ikiwa kuna ugeni wa Waziri wa Mambo ya Nje ya China.

“Huu ni ushahidi mwingine wa mahusiano ya kiuchumi kati yetu na China tunawakaribisha kampuni zao kushiriki katika ujenzi wa vipabde viwili vilivyobaki vya reli ya kisasa vya Makutopora hadi Tabora na Tabora hadi Isaka,” alisema Chamuriho.

Pia aliiomba Serikali ya China kuunga mkono katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuridhia taasisi za Serikali ya China kutoa mkopo nafuu ili reli nzima kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza iweze kufanya kazi mapema.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania, (TRC), Masanja Kadogosa, alisema makampuni ya kimataifa yaliyojitokeza kwa ajili ya kujenga reli ya kisasa kipande cha Mwanza – Isaka ni 108, baada ya kufanya mchakato kampuni za CCECC zilishinda zabuni.

“Tulitangaza kipande hiki cha tano mwezi Agosti 25 na Novemba 25 na kampuni za kimataifa zaidi ya 108 ziliomba tenda. Bada ya kufanya mchakato kwa mujibu wa sheria za nchi yetu kuna kampuni mbili zilishinda,” alisema Kadogosa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CCECC, Mhandisi Jiang Yigao alisema; “Kampuni hii imekua Tanzania kwa zaidi ya miaka 50, kwa miaka 10 iliyopita tumetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo daraja la Busisi- Kigongo, Ubungo interchange na ujenzi wa reli ya Tazara.

“Kama tulivyofanya ujenzi wa TAZARA tutafanya hivyo hivyo kwa kujenga reli hii ya kisasa tukitumia raslimali zilizopo na kujenga mradi huu kwa wakati na kwa viwango vya kimataifa.”
D5F51C12-EEFC-4579-8E9E-F85460B93EAE-300x161.jpeg

WALIYOZUNGUMZA RAIS MAGUFULI NA WANG YI
Kabla ya utiliaji saini wa Mkatba wa ujenzi wa Reli Rais Magufuli alifanya mazungumzo na Waziri Wang Yi kuhusu mambo mablimbali ya kimahusiano na uchumi baina ya TANZNAIA NA China.

Katika hotuba yake Rais magufuli alidokeza mambo makubwa matatu waliyozungumza ikiwemo kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa miradi.
“Nimemuomba atusaidie miradi mitatu mikubwa ya umeme ukiwemo wa maji ya mkoani Njombe, Lumakali na Luhuji pamoja na ujenzi wa KM 148 za barabara kwa kiwango cha lami Zanzibar,” alisema Rais Magufuli.

Pia alisema ameiomba Serikali ya China kutoa msamaha wa madeni mbalimbali yakiwemo ya muda mrefu ambayo China iliikopesha Tanzania.

“ Nimewaomba watusamehe madeni yetu tuliyokuwa tumekopa ikiwemo la Dola za Marekani Mil. 15.7 za ujenzi wa reli ya TAZARA, deni la Dola za Marekani Mil.137 la nyumba za askari pamoja na deni la kiwanda cha Urafiki la Dola za Marekani Mil.15,” alisema Rais Magufuli.

Alibainisha kuwa China imejipatia fedha nyingi kupitia utekelezaji wa miradi hapa nchi ambapo kwa miaka 10 wamevuna zaidi ya Trilioni 21 sawa na Dola za Marekani Bilioni 10 ambazo ni fedha za walipa kodi wetu; “Ndiyo maana kwenye maombi yangu niliomba mtusamehe maana na nyie mmevuna mengi kwetu.”

Alisema walizungumzia pia suala la fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania na fursa ya soko la China kwa bidhaa za kitanzania.
“China ni nchi tajiri duniani na sisi Tanzania tuna mazao mengi ambayo tunaweza kuyapeleka nchini humo hivyo natoa wito kwa Watanzania kuwa huu ndio wakati wa kulishika soko la China kwa kuwapelekea mazao yetu.

“Nimemuhakikishia Waziri Wang Yi kuwa kufanya biashara na Tanzania kuna faida kwani kupitia nchi yetu watakuwa na uwezo kufanya biashara na nchi zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye watu milioni 165 na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi zilizo Kusini mwa Afrika yenye watu milioni 500 kwa sababu Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya hizo.

“Mazungumzo tuliyofanya yalikuwa mazuri na nimemuhakikishia Waziri Wang Yi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na China kwa sababu ni ndugu zetu,” alisema Rais Magufuli.

Pamoja na ushirikiano uliopo kwenye sekta nyingine ikiwemo sekta ya miundombinu, uhusiano baina ya Tanzania na China umezidi kuimarika zaidi katika sekta ya TEHAMA. Kupitia kampuni ya Huawei, China imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika kufanikisha miradi mbalimbali inayolenga kuboresha sekta ya TEHAMA sambamba na kukuza na kuibua vipaji vya sekta hiyo muhimu hapa nchini.

Matunda ya ushirikiano huo yalijidhihirisha hivi karibuni ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikabidhi tuzo kwa washindi wa shindano la TEHAMA duniani lililoandaliwa na kampuni ya Huawei ambapo wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walishika nafasi ya pili Ulimwenguni.

FEC80344-E90B-44AE-A097-B553E89658B5-300x200.jpeg
Habari ya kina kuhusu kipande cha Mwanza - Isaka kwa hisani kubwa: Source/ Chanzo : Yametimia: Mkataba ujenzi wa SGR Mwanza- Isaka wasainiwa
 
January 30, 2021

TRC na Kongamano la SGR reli Mwanza-Isaka



Mkurugenzi Mkuu wa TRC Bw. Masanja Kungu Kadogosa ategemea makubwa kuhusu Kongomano la SGR reli kipande cha Mwanza - Isaka.
Source : TRC reli tv
 
Wakati wa ukaguzi wa uharibifu wa njia ya reli ya kati sehemu za Gulwe na Kilosa, wataalamu wa ujenzi wa reli wamebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuitumia reli ya mkoloni kwa miaka zaidi ya 10 ijayo.


Kweli nchi nzima haina mwenye kipaji cha kutabiri majanga!!! au wote ni wachumia tumbo
 
9 Feb 2021

Why Tanzania is building THE LONGEST SGR RAILWAY IN AFRICA. Tanzania SGR


The Tanzania Standard Gauge Railway is a railway system, under construction, linking the country to the neighboring countries of Rwanda and Uganda, and through these two, to Burundi and the Democratic Republic of the Congo, as part of the East African Railway Master Plan. In this video, We take at this mega project in detail. On how this SGR railway is being, why it is being built, it is economic significance to Tanzania and Africa at large. We also look at the motive for the construction of this massive project.

00:00 Prior Information about the project
01:38 Tanzania, Kenya SGR
02:14 Tanzania SGR
08:01 Economic Significance of the Project
Source : SAFARI TALK TV
 
2 March 2021
Kilosa, Morogoro
Tanzania

HATUA YA UJENZI ILIPOFIKIA , DARAJA LA MTO MKONDOA KUUNGANISHA MAHANDAKI MAWILI RELI MPYA YA SGR


Daraja toka handaki moja kwenda la pili lina Urefu mita 487 kukatisha juu ya Mto Mkondoa ili kuunganisha mahandaki hayo mawili.

Nguzo za daraja bado zinaendelea kujengwa ili kumalizia ujenzi wa daraja hilo katika kipande cha reli mpya ya SGR baina ya Morogoro na Makutupora Dodoma.
Source : TRC RELI TV
30 December 2019 Diamond asimama kuangalia maendeleo ya ujenzi wa reli Mpya SGR
 
2 March 2021
Kilosa, Morogoro
Tanzania

HATUA YA UJENZI ILIPOFIKIA , DARAJA LA MTO MKONDOA KUUNGANISHA MAHANDAKI MAWILI RELI MPYA YA SGR


Daraja toka handaki moja kwenda la pili lina Urefu mita 487 kukatisha juu ya Mto Mkondoa ili kuunganisha mahandaki hayo mawili.

Nguzo za daraja bado zinaendelea kujengwa ili kumalizia ujenzi wa daraja hilo katika kipande cha reli mpya ya SGR baina ya Morogoro na Makutupora Dodoma.
Source : TRC RELI TV

Mkuu vipi kwa kipande cha isaka to mwanza naona kimya kimeanza au bado??
 
Mkuu vipi kwa kipande cha isaka to mwanza naona kimya kimeanza au bado??
Watakuwa wanajipanga "kutafuta pesa ya ndani" kugharamia kipande hicho cha SGR.

Maana siku zote wamesema wameweza kutumia fedha za ndani kipande cha SGR reli ya Dar - Moro, pia kipande cha SGR Reli Morogoro - Makutupora yote ni pesa za ndani.

Hivyo tutegemee tutabanwa wananchi kodi ilipwe kwa wingi na vyanzo vipya kubuniwa kazi imalizike ndani ya miaka 15.
 
14 March 2021

SAFARI ZA TRENI (SGR) KUANZA MWEZI WA NANE MWAKA HUU 2021

Waziri wa Ujenzi awapa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Reli ya SGR wajumbe wa Kamati ya Bunge. Urefu wa reli hiyo Dar -Mwanza ikikamilika ni kilometa 1,216

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dk Leonard Chamuriho amesema safari ya reli ya Kisasa (SGR) zinatarajiwa kuanza August mwaka huu katika kipande cha Dar es salaam – Morogoro.

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ya kukagua mradi huo kutoka Dodoma hadi Dar es salaam , Dk Chamuriho alisema baada ya vichwa na mabehewa ya treni kuwasili July 2021 watafanya majaribirio ya safari. Alisema ujenzi wa kipande hicho umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 huku na maeneo yaliyobaki yatakamilishwa ndani ya muda mfupi.

Hata hivyo amesema katika Afrika reli ya SGR inayojengwa nchini Tanzania ndiyo bora na inaweza kuhimili mzigo mzito wa tani 35 na kubeba mabehewa mawili kwenda juu huku nchi nyingine reli yao ikiwa na uwezo wa kuhimili uzito wa tani 25.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu Mh. Selemani Kakoso alisema wameridhishwa na ujenzi wa mradi wa treni ya mwendo kasi (SGR). Mh. Kakoso ambaye ni Mbunge wa Mpanda vijijini alisema yapo mambo ambayo wamekuwa wameishauri Serikali na tayari yamefanyiwa kazi. Alisema walikuwa wamesisitiza kuwa maeneo ambayo reli inapita wananchi walipwe haraka iwezekanavyo fidia zao ambayo jambo hilo limeshafanyiwa kazi.
Source: millard ayo
 
February 5, 2020
Kilosa, Tanzania

Wahandisi : Reli ya kati ihamishwe toka eneo la mafuriko na pia SGR kuchukua miaka 15 kukamilisha

Wakati wa ukaguzi wa uharibifu wa njia ya reli ya kati sehemu za Gulwe na Kilosa, wataalamu wa ujenzi wa reli wamebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuitumia reli ya mkoloni kwa miaka zaidi ya 10 ijayo.




Pia Reli mpya ya SGR itachukua takriban miaka 15 kumalizwa kujengwa hilo limebainishwa ktk eneo la reli ya kati lililokumbwa na mafuriko yasiyo ya kawaida wakati jopo la wahandisi na mkurugenzi mkuu walipokuwa wanajadili athari za mafuriko na changamoto za reli ya mkoloni na reli mpya ya SGR.

TRC inapoteza zaidi ya milioni 100 kwa siku kutokana na kusitisha safari reli ya kati. Na ili kukabiliana na mafuriko inabidi reli ya kati ihamishiwe mlimani na mlima huo unahitaji kuchongwa pia .

Uharibifu ktk eneo la mto Mkondoa ni mkubwa sana na ingawa eneo hilo la Gulwe Kilosa hakuna mvua lakini mvua kubwa zinazonyesha mikoa ya Iringa na Dodoma inaingiza kiasi kikubwa cha maji mto Mkondoa.

Source: TRC Reli TV

Mbongo akisema 15 ujue hapo ni miaka 50
 
2 March 2021
Kilosa, Morogoro
Tanzania

HATUA YA UJENZI ILIPOFIKIA , DARAJA LA MTO MKONDOA KUUNGANISHA MAHANDAKI MAWILI RELI MPYA YA SGR


Daraja toka handaki moja kwenda la pili lina Urefu mita 487 kukatisha juu ya Mto Mkondoa ili kuunganisha mahandaki hayo mawili.

Nguzo za daraja bado zinaendelea kujengwa ili kumalizia ujenzi wa daraja hilo katika kipande cha reli mpya ya SGR baina ya Morogoro na Makutupora Dodoma.
Source : TRC RELI TV
Hivi aliyewaambia Makutupora ipo Dodoma ni nani? Makutupora ipo Manyoni, Singida na ipo kilomita 82.7 (magharibi) kutoka Dodoma Jiji.
 
Reli hii inaanza kutumika mapema kabla ya miaka hiyo 15. Uzuri ujenzi uko kwenye mgawanyiko. Sio contractor mmoja mwanzo mwisho
 
Maguli anawatesa sana waombezi wa mabaya kwa matokeo ya miradi.

Nchi imeabadilika na mengi mazuri yanakuja.
 
Back
Top Bottom