Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika

Mhandisi: Reli ya SGR mpya kuchukua miaka 15 kumalizika

14 March 2021
Morogoro, Tanzania

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU WAFURAHISWA NA KAZI ZA WAHANDISI WAZAWA KATIKA KARAKANA YA RELI MOROGORO


Source : TRC RELI TV
 
Upo uwezekano JPM akitoka madarakani baadhi ya miradi itashindwa kuendelea...
Meko kaharibu nchi kwa sababu ya kuwa one man show. Nafuu Mungu ameamua kuchukua roho yake mapema kabla hajaharibu sana.

Kama unaamini Magufuli yuko hai shauri yako. Mimi najua ukifa ubongo (brain damage) hata moyo usaidiwe na mashine huamki
 
March 27, 2021
Chato, Geita
Tanzania

CHAMURIHO: TUTASIMAMIA VIZURI MRADI WA UJENZI WA RELI YA SGR KUTIMIZA NDOTO YA JPM


Source : TRC RELI TV

Zawadi aliyoacha Magufuli kwa waTanzania : Reli ya kisasa (SGR)

Tarehe 14 mwaka 2018 Rais John Magufuli aliasisi ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa kwa kuweka jiwe la msingi la kipande cha pili cha mradi huo kilichoanzia mkoani Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma.
Reli ya Kisasa nchini Tanzania SGR

CHANZO CHA PICHA,MICHAEL KHATELI
Maelezo ya picha,
Reli ya Kisasa nchini Tanzania SGR
Kipande hicho chenye urefu wa kilometa 422 kitagharimu kiasi cha shilingi trilioni4.3, ambapo ni sehemu ya mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kati wa kuanzia Dar es salaam hadi Mwanza yenye urefu wa kilomita 1,219. Ujenzi wa kipande cha kutoka Dar es salaam hadi Morogoro unaelezwa kuwa umekamilika kwa asilimia 80. Hii ni zawadi aliyoacha Magufuli kwa Watanzania. Source : Zawadi aliyoacha Magufuli kwa Watanzania - BBC News Swahili
 
8 April 2021

RIPOTI YA CAG KUHUSU MRADI WA SGR RELI MPYA KIPANDE CHA DAR - MOROGORO
  • Wafanyakazi 952 wa kigeni hawana vibali vya kufanya kazi na hivyo kuikosesha serikali mapato ya dola million 2
  • Mradi kipande cha Dar Moro kimechelewa kukamilika kwa miezi 18
  • Ucheleweshaji wa kukamilika kipande cha Dar Moro kimesababisha Gharama za Mhandisi msimamizi kuongezeka kwa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 11.2 sawa na bilioni 26.3 shilingi za kitanzania
 
8 April 2021
Kaliua, Mpanda

RELI YAKATIKA ABIRIA WAKWAMA


Kufuatia mvua kubwa zilizonyesha kwa siku tatu mfululizo na kusababisha tuta la reli kusombwa na maji na kuharibu miundombinu ya Reli ya Tabora – Mpanda kwa umbali wa kilomita 5 kati ya eneo la Lumbe na Usinga umesababisha abiria waliokuwa wakitoka Tabora kwenda Mpanda kukwama kwa takribani siku mbili na kulazimika kulala stesheni ya Kaliua Mkuu wa wilaya ya Kaliua Abel Busalama amefika eneo hilo ambapo amepiga marufuku wananchi kuendesha shughuli za kilimo kando ya reli huku akiliomba shirika kutafuta usafiri mbadala kwa abiria waliokwama.
Source : millard ayo

..................................................................
...
Kumbukumbu za changamoto ktk reli ya Tabora Kaliua mpaka Mpanda

21 May 2020
Maeneo ya mto Ugalla mkoani Tabora ambapo TRC na wahandisi wake walivyoweza kukatisha mto huu mkybwa
tazama mto Ugalla ulivyo mkubwa
 
13 May 2019
Spika Job Y Ndugai mradi wa SGR Reli mpya usingeanza kwanza. Bali bandari ya kisasa ndiyo ingejengwa kwanza ikimalizika ndiyo ujenzi wa SGR reli ungefuata. Kuanza ujenzi wa SGR reli bila bandari ya kisasa Bagamoyo ni sawa na kuweka rikwama / mkokoteni mbele ya punda ausukume.

Tazama maelezo na mapendekezo ya Spika wa Bunge kuhusu uamuzi wa Serikali kusitisha mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo


Spika Ndugai Aishangaa Serikali Kusitisha Mradi wa Bandari Bagamoyo

 
April 2021

WANAJESHI KUTOKA NCHI ZA ULAYA, INDIA NA AFRIKA WATEMBELEA MRADI WA SGR.


Ziara hiyo inayoratibiwa na TPDF, maofisa hao wa kijeshi wamekuja kujifunza na kubadilishana uzoefu wa miradi ujenzi wa miradi mikubwa amesema Mkurugenzi wa uhandisi TRC.
Source : TRC RELI TV
 
Hii sgr hadi ikamilike mpaka kigoma au mwanza ni mwaka 2040


Huu mradi unajengwa mwendo wa kobe sana


Hii ya Dar morogoro yenyewe siasa nyingi bado sanaah
 
Mradi huu ulichukuliwa kisiasa sana na mwendazake bila kufanyiwa upembuzi yakinifu na changamoto zake huku ulikuwa umebinafsishwa kuwa ni wa Mh. Hayati John Pombe Joseph Magufuli badala ya serikali ya Tanzania.

Ni matumaini yetu awamu hii ya sita itakuja na upembuzi yakinifu wa mradi huu mzima na kwa kuwa utatumia zaidi ya miaka 15 kukamilika basi mradi huu mkubwa uwe wa serikali ya Tanzania na kuanzia awamu hii ya sita uwazi zaidi utumike kuwafahamisha waTanzania wauenzi kama ni mradi wao na siyo kuubwaga kwakuwa ulikuwa wa mwendazake.
 
21 MAY 2021

WAHANDISI “WAKITEST” MITAMBO, VITUO VYA UMEME 100% SGR MPYA RELI KIPANDE DSM - MOROGORO



Source: TRC RELI TV
 
22 May 2021
Dar es Salaam, Tanzania

Mkurugezi wa TRC, Bw. Masanja Kadogosa aelezea changamoto za nguzo za kubeba daraja mradi wa SGR Reli kati ya Dsm na Pugu

Nguzo mbili za kubeba reli ya juu kwa juu mradi wa SGR Mpya reli pale Nkrumah jijini Dar es Salaam zilileta changamoto na kubidi kurekebishwa huku ujenzi wa sehemu hiyo marekebisho yake kumalizika November 2021, abainisha mkurugenzi mkuu wa TRC

Mkurugenzi pia anatufahamisha masuala ya umeme kukamilika baada ya miezi 6 kwani inahusisha pia wakandarasi kupasisha mfumo upo salama na unafaa kwa matumizi ya reli. Pia mabehewa na vichwa kuchelewa kufika kutokana na nchi zilizopewa kazi ya kuyaunda kukumbwa na gonjwa la korona.
 
10 Juni 2021
Dodoma, Tanzania

Waziri wa Fedha Dr. Mwigulu Nchemba : Miradi mikubwa ikiwemo SGR RELI MPYA ni ya waTanzania wote lazima ikamilike

 
14 Juni 2021

UCHAMBUZI WA BAJETI NA KODI MPYA

Zitto Kabwe aainisha changamoto ya mradi wa SGR RELI kwa uongozi wa awamu ya 6 ulioshika hatamu ya uongozi wa serikali kupata pesa za mradi huu wa SGR RELI MPYA

Mradi huu wa SGR RELI MPYA ulikuwa una nadiwa wa Mh. Rais John Magufuli , sasa ni wajibu wa serikali mpya kuurudisha kwa wananchi kuwa ni mradi wao na washawishiwe kukubali kulipa kodi zaidi kwa kuwa SGR RELI Mpya ni mradi wao wananchi na watafaidika nao, tofauti na ilivyokuwa wakati wa awamu ya 5 ambapo kila kitu kilionekana na kupigiwa chapuo kuwa ni (mradi) cha Magufuli mwenyewe.
Source : E Digital
 
26 June 2021

MADA : SIKU 100 ZA UONGOZI WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, MKURUGENZI TRC AZUNGUMZA

Masanja Kungu Kadogosa, mkurugenzi Mkuu wa shirika la reli nchini Tanzania TRC azungumzia siku 100 za Mh. rais Samia Suluhu Hassan na picha kubwa ya sekta ya reli baada uwekezaji wa dola za Kimarekani US$ 7 bilioni itavyokuwa miaka 10 ijayo.
 
13 August 2021

Miradi ya Miundo-mbinu Tanzania kama SGR, NHPP Stiegler's Gorge , Air Tanzania yajadiliwa kwa kina.


Jopo hilo lina jumuisha Dr. Bravious Kahyoza, Prof. Abdul Shareef, Aisha , Rosemary Mwakitwange, Zitto Kabwe, Haidery, J R Nkomo, Sheikh Salim Amar, Joseph Cyril James.

Asilimia 7% ya ukuaji uchumi, Public spending, Kodi, Uwekezaji, State capture, asilimia 26 ya watu wote ni kundi la masikini hohehahe limeongezeka ( yaani watu 15 milioni)

Je majenzi ya miradi hii mikubwa ni kweli yanabebwa na fedha zetu za ndani sisi waTanzania ?

Public spending review inaonesha ktk miaka 5 inaonesha matumizi ya serikali yameongezeka na matumizi ya serikali ni huduma na siyo uzalishaji kama ingekuwa ongezeko la matumizi yangekuwa ktk sekta binafsi ambao ndiyo wazalishaji halisi.

Nini madhara yake, serikali inakosa mapato toka sekta binafsi na ndiyo maana serikali inakwenda kuwakaba zaidi wananchi masikini kwa kodi kama za kodi za miamala , kodi ktk mafuta ya uendeshaji vyombo vya usafiri n.k

Hili linazidi kuifanya serikali kuwa ktk mbinyo mkubwa wa kutafuta fedha kujaribu kukamilisha majenzi ya miradi mikubwa ya miundo-mbinu mingi iliyoanzishwa kwa wakati mmoja ktk miaka mitano ya hayati John Magufuli.

Serikali haikutafakari sana kwa kuwekeza ktk miradi hii mikubwa inayojengwa na makampuni ya nje na kufanya Asilimia 77% ya matumizi hayo ya matrilioni yanakwenda kunufaisha nje yaani nchi za Turkey na China na vifaa vya gharama kubwa hutoka nje huku cement ya ndani ya Tanzania inapata asilimia 7 % tu ya matrilioni ya miradi hii.

Maana yake Tanzania inachochea chumi za nje na siyo uchumi wetu wa ndani. Na ndiyo maana fedha imepotea mikononi mwa wananchi mmoja mmoja na hata serikalini kupelekea nchi kwenda nje kukopa na kuwabana wananchi kwa tozo za miamala.

Source : Nadj Media Center
 
Back
Top Bottom