13 August 2021
Miradi ya Miundo-mbinu Tanzania kama SGR, NHPP Stiegler's Gorge , Air Tanzania yajadiliwa kwa kina.
Jopo hilo lina jumuisha Dr. Bravious Kahyoza, Prof. Abdul Shareef, Aisha , Rosemary Mwakitwange, Zitto Kabwe, Haidery, J R Nkomo, Sheikh Salim Amar, Joseph Cyril James.
Asilimia 7% ya ukuaji uchumi, Public spending, Kodi, Uwekezaji, State capture, asilimia 26 ya watu wote ni kundi la masikini hohehahe limeongezeka ( yaani watu 15 milioni)
Je majenzi ya miradi hii mikubwa ni kweli yanabebwa na fedha zetu za ndani sisi waTanzania ?
Public spending review inaonesha ktk miaka 5 inaonesha matumizi ya serikali yameongezeka na matumizi ya serikali ni huduma na siyo uzalishaji kama ingekuwa ongezeko la matumizi yangekuwa ktk sekta binafsi ambao ndiyo wazalishaji halisi.
Nini madhara yake, serikali inakosa mapato toka sekta binafsi na ndiyo maana serikali inakwenda kuwakaba zaidi wananchi masikini kwa kodi kama za kodi za miamala , kodi ktk mafuta ya uendeshaji vyombo vya usafiri n.k
Hili linazidi kuifanya serikali kuwa ktk mbinyo mkubwa wa kutafuta fedha kujaribu kukamilisha majenzi ya miradi mikubwa ya miundo-mbinu mingi iliyoanzishwa kwa wakati mmoja ktk miaka mitano ya hayati John Magufuli.
Serikali haikutafakari sana kwa kuwekeza ktk miradi hii mikubwa inayojengwa na makampuni ya nje na kufanya Asilimia 77% ya matumizi hayo ya matrilioni yanakwenda kunufaisha nje yaani nchi za Turkey na China na vifaa vya gharama kubwa hutoka nje huku cement ya ndani ya Tanzania inapata asilimia 7 % tu ya matrilioni ya miradi hii.
Maana yake Tanzania inachochea chumi za nje na siyo uchumi wetu wa ndani. Na ndiyo maana fedha imepotea mikononi mwa wananchi mmoja mmoja na hata serikalini kupelekea nchi kwenda nje kukopa na kuwabana wananchi kwa tozo za miamala.
Source : Nadj Media Center