Mhasibu, Afisa TEHAMA wa Kanisa la SDA wapandishwa kizimbani kwa Wizi wa Tsh. Milioni 717


Ukiwaona wanavyosimuliana jinsi wakatoliki wanavyoabudu sanamu unaweza kufikiria kila mtu yuko serious. Kumbe binadamu ni wale wale. Na mambo yetu yale yale. Na kibaya, tuna share hata namna yadhambi zinazoendelea.
Tuache kujihesabia haki tukiwa tunaishi duniani
 
Wakati waumini wanajikamua pesa za sadaka kwa ajili ya maendeleo ya kanisa, kuna wajanja wachache wanazivizia na kuzitafuna kisawasawa. Kuna mhasibu mmoja wa SDA ambaye ni jamaa yangu yaani anazikula sana hizo hela za sasaka, hadi raha!


MKUU Sadaka humpi mtu au kanisa, unaitoa kwa MUNGU wako kwa Njia ya IMANI

We Kama unajua NDANI yako huwa unaoelekea MTU au kanisa sadaka na Sio MUNGU wako bora uache kutoa izo sadaka b'se hakuna mavuno B'se tunamuendea MUNGU kwa IMANI tu pekee yake

Hao watu waibe, wasiibe ni wao wenyewe na nafsi zao ila Kama umetoa sadaka yako kwa IMANI hiyo ni hadhina kubwa Sana mbele za MUNGU wako

Note: Kuna tofauti kubwa kati ya MUNGU na dini

Dini ilimkataa na kumpinga hata kumsulubisha YESU Kwaiyo chunguza NDANI yako wewe ni muumini wa dini au muumini wa MUNGU?🤔
 
Sitoi Sitoi sadaka kanisani tena,wataomba na kaomba lkn nitakuwa mpenzi msikilizaji na mtazamaji.
 
Dini ilimkataa na kumpinga hata kumsulubisha YESU Kwaiyo chunguza NDANI yako wewe ni muumini wa dini au muumini wa MUNGU?🤔
Mkuu kama ni hivyo basi hakuna haja ya kwenda kanisani bali unaweza ukamuabudu Mungu yako ukiwa nyumbani na kumtolea dhabihu badala ya kwenda kanisani kukamuliwa sadaka na wafuata dini.
 
Hapo kesi ni moja tu kutakatisha pesa japo sidhani kama ni kweli hii wamepewa kama kifungashio tu wasichomoe (Kanisa limewasingizia kupitia Wakili wao)

Swala la wizi wa Pesa za Kanisa kama kweli Sadaka huwa ni ya Mungu basi aachiwe mwenyewe sidhani kama Mungu anahitaji mtetez binadamu na kila Sabatho wanafundisha Mungu haibiwi twajiibia wenyewe. Shida iko wapi sasa?

Kimsing wameupiga mwingi waendelee kusafisha Mitaa, Conference na Union zote mpaka GC.

#Biashara ya dini inaimaliza Afrika yetu.
 

Hata kama umeamua kuwa mwizi, huu ni wizi wa kipumbavu.

Auditor wa kawaida hata wa for four angeweza gundua huo wizi ndani ya mwezi.
 
Mkuu kama ni hivyo basi hakuna haja ya kwenda kanisani bali unaweza ukamuabudu Mungu yako ukiwa nyumbani na kumtolea dhabihu badala ya kwenda kanisani kukamuliwa sadaka na wafuata dini.


MUNGU haabudiwi kanisani mkuu, MUNGU anaabudiwa katika Roho na katika kweli


Yohana


4.20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.
4.21 Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.


MWANAMKE msamaria alimwambia YESU 👉 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.

Hapa alikuwa akimaanisha kumuabudu MUNGU ni Mahali/SEHEMU fulani


katika mlima huu 👉 sehemu


huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia 👉 sehemu


Tazama jibu la YESU kwa mwanamke Msamaria👇
 Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.


Yohana 4.24


"Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli"


Kumuabudu MUNGU ni katika Roho na katika Kweli na Sio kama dini inavyosema Kwamba kumuabudu MUNGU ni mahali au sehemu fulani hiyo hali ilikuwa katika Agano la kale kabda ya MUNGU kutupatanisha na yeye kwa njia ya YESU KRISTO, Ndio maana YESU alimjibu MWANAMKE kwamba ninyi mnaabudu msichokijua 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…