Mhasibu afungwa miaka 76 kwa kufoji risiti na kujipatia tsh. mil. 97

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Bernald Mnyilenda aliyekuwa Mhasibu wa Shule ya Southern Highlands amehukumiwa kifungo hicho baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa kumkuta na hatia ya kutumia kitabu ghushi cha Risiti na kupokea ada kiasi cha Tsh. milioni 97.

Mahakama hiyo imemkuta na makosa 22 baada ya kusikiliza Mashahidi 7 wakiwemo wakaguzi wawili, mmiliki wa shule hiyo, Marry Joseph Mungai na baadhi ya wazazi waliothibitisha kulipa ada na kupewa risiti zilizokwisha muda wa matumizi.

Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa, alikataa utetezi wa Mtuhumiwa aliyeomba kupunguziwa adhabu na kusema hajaona ushawishi, hivyo anastahili hukumu ya miaka 76 na kutakiwa kurejesha Tsh. Milioni 116.3.
 
Anarejeshaje wakati kutoka tu kwa hiyo miaka,sidhani.
 
Dah! Jamaa sijui watampeleka Gereza la Isupilo! Amewatapeli Mabepari wa Kimataifa! Pole yake. Na kama alitumia hiyo hela kujongea, ndiyo basi tena.

Jina la Mkurugenzi tu wa hiyo English Medium linaogopesha! Marry Joseph Mungai!!
 
Hii dunia haiko fair!!nchi ingekuwa huru na mahakama ziko huru sasa hivi mwi*lu,mwezi wa kwanza, nope no uyo na majambazi wengine wa kijan wangekuwa jela kwa kuwahujumu mamilioni ya watanzania wanaoishi kwenye ufukara wa kutisha kwa sababu yao.Mungai hili jina is untouchable pengine mmiliki wa shule kala hasara afu jumba bovu kaangushiwa mnyonge wa nchi hii,nimewaza tu msije nifunga kwenye kiroba
 
Vipi wale wanaofisadi matrilioni kwenye sirikali na wanajulikana hadi na watoto wadogo, wenyewe hawastahili mvua hadi huyo mhasibu apigwe mvua yote hiyo kwa pesa ya kashata, aka. pesa ya ubuyu, aka. pesa ya mboga, aka. vijisenti....the world is not fair.​
 
Wizi hayo huwa ndio matokeo yake.

Southern highland kule mbeya inamilikiwa na Philipo Mulugo, mzee wa Tanganyika na Zimbabwe.
Hii shule ni ya English medium. Iko katika Mji wa Mafinga. Ni ya marehemu Joseph Mungai, Bepari wa Kimataifa. Pake Mafinga ni shuke maarufu na ya muda mrefu. Ada yake si haba! Maana watoto wanaosoma hapo, wazazi wao lazima wajimudu.

Alishawahi kuwa Mbunge wa Mugindi kwa miaka mingi, na pia Waziti katika serikali ya Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na JK! Alipoingia Magufuli alimpiga zengwe, na historia yake ikavurugika kuanzia hapo.

Ni tofauti na hiyo shule ya sekondari ya Mbeya ambayo huyo Philipo Mugo aliwatapeli Wahindi wa watu.
 
Philipo mlugo ni mtu, aliwapiga changa akina kanjibai wakaingia kingi wakapigwa kanyaboya shule mbili kwa bei ya suti na tai ya lameck Wa nchemba
 
Bernald Mnyilenda aliyekuwa Mhasibu wa Shule ya Southern Highlands amehukumiwa kifungo hicho baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa kumkuta na hatia ya kutumia kitabu ghushi cha Risiti na kupokea ada kiasi cha Tsh. milioni 97.

Mahakama hiyo imemkuta na makosa 22 baada ya kusikiliza Mashahidi 7 wakiwemo wakaguzi wawili, mmiliki wa shule hiyo, Marry Joseph Mungai na baadhi ya wazazi waliothibitisha kulipa ada na kupewa risiti zilizokwisha muda wa matumizi.

Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa, alikataa utetezi wa Mtuhumiwa aliyeomba kupunguziwa adhabu na kusema hajaona ushawishi, hivyo anastahili hukumu ya miaka 76 na kutakiwa kurejesha Tsh. Milioni 116.3.
Huyo jamaa mjinga vihela vya shule vidogo sana ni rahisi kujulikana. Sasa mtu kalipa na mwanaye yuko hapo.Mkuu wa Shule hela hazioni ila wewe unadai wamelipa. Ni alilo hizo au matope.

Alijaribu kamba yake sasa imekatika.
 
Vipi wale wanaofisadi matrilioni kwenye sirikali na wanajulikana hadi na watoto wadogo, wenyewe hawastahili mvua hadi huyo mhasibu apigwe mvua yote hiyo kwa pesa ya kashata, aka. pesa ya ubuyu, aka. pesa ya mboga, aka. vijisenti....the world is not fair.​
Aliyepatikana na nyama ndio mwizi wa mg'ombe
 
Duuh..miaka mingi sana asee..hii sio adhabu bali kukomoana au alitembea na demu wa hakimu akaona akomeshee kupitia hiyo kesi.

Wizi sio mzuri...ukitaka kuiba iba za umma pia kula na wengi...sasa unaiba ada za wazazi sio poa.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom