Uchunguzi wa kifo cha Martha Towo ni rahisi sana na si chini ya watu 20 wanaweza kuhusishwa nacho, ambapo watachujwa mpaka watabaki si chini ya watano .
Na ni uchunguzi rahisi kutokana na makosa mengi waliyofanya wauaji.. Hawakuwa wajuzi maana wajuzi huwa hawaachi alama! Japo kuna kosa moja dogo sana hufanya na kufumua mpango wote.
Uchunguzi wake utaanzia kazini kwake, maisha yake nje ya kazi, marafiki zake, wateja wake, mishe na dili zake, mawasiliano yake pamoja na mahusiano.. Hapa ni kwa ajili ya ku 'establish' Msingi wa kesi na 'motive' ya muuaji/wauaji.
Uchunguzi wa pili ni eneo lilikofanyika tukio.. Pori la Mitamba linalosifika kwa matukio ya mauaji, Mitamba halina tofauti sana na Mabwepande na kama linaweza kuchunguzwa vizuri kuna maiti nyingi mule zinaweza kuwa zimezikwa.
Mitamba liko Kibaha njia ya kwenda Bagamoyo eneo linaitwa Pangani.. Sehemu kubwa ya pori la Mitamba ni eneo la wizara ya mifugo na uvuvi na kuna kipindi matapeli wa viwanja Kibaha walilivamia na kuwauzia watu viwanja mpaka serikali ikaingilia kati.
Marehemu ni mkazi mwenyeji wa Kibaha Kwambonde kakulia hapo, kosoma Tumbi nknk. Wazazi wake wanaishi hapo mpaka sasa na ni watu unaoweza kuwaita maarufu eneo hilo na hata kanisani kwao Tumbi. Kwanini muuaji/wauaji wakachagua kuja kummaliza 'nyumbani kwao'?
Marehemu alisafiri salama salimini toka kituo chake cha kazi Shinyanga mpaka nyumbani Kwambonde Kibaha. Pengine alitumia ndege, usafiri binafsi au wa jumuiya lakini alifika salama.
Je, wauaji walikuwa wanamfuatilia kote huko?
Je, wauaji ndio walimuita aje Kibaha?
Je, lengo lake la kuja nyumbani Kibaha lilikuwa ninini?
Je, mpango wa kummaliza Kibaha pori la Mitamba ulikuwa mpango plan A au B?
Marehemu siku ya tukio alikuwa kanisani na ndugu zake.. Ni wazi alipata wito wa kuitwa nje mara moja ama kwa ishara ya mtu alikuwa ndani ya kanisa ama kwa simu kwa kuwa mikoba yake aliacha alipokuwa kaketi. Hakurudi!
Ni wazi walimuita walikuwa nje kabisa ya kanisa barabarani! Kanisa la KKKT Tumbi liko pembezoni mwa barabara ya kuelekea Tumbi hospital. Ni wazi kulikuwa na gari ambalo ama alipanda kwa hiari ama kwa lazima/Kutekwa.
Ni wazi safari ilianza kuelekea Pangani pori la Mitamba.. Macho ya marehemu yata 'reveal' kilichotokea ndani ya gari kwa hicho kipindi chote mpaka kufika Mitamba kumwagiwa Petrol na kuchomwa moto!