Mayor Quimby
JF-Expert Member
- Mar 13, 2021
- 6,750
- 14,529
Shida yenyewe 90% ya viongozi wetu kuanzia kwa rahisi wametoka familia hizo hizo ‘hoe hae’, sasa sijui nani anamuandaa mwenzake kumtumikisha.N
Nchi karibu zote za Africa kuondoa Egypt, Morocco Libya na Tunisia may be, wana sera za makusudi kuwafanya wananchi mafukara wakubwa ili wawatawale kwa urahisi. Ufukara kwa wananchi ni nyenzo muhimu kuwasaidia kutawala bila bughudha au kero. Maskini hawezi kununua silaha, kuendesha mgomo au kudai haki anaogopa kufa njaa. Inabidi akubali kulamba viatu vya mkubwa, kusifu kuabudu ili aweze kuishi.
Tatizi ninaloliona kwa upande wangu ni mfumo ambao unaotaka ili hudumu kwenye nafasi yako kutokana na mamlaka ya wakuu wako inabidi uwe mlamba miguu.
Tatizo lingine serikali inatumia muda mwingi kutengeneza vijana kama viongozi wa kesho na kuwapa special skills lakini ukiwasikiliza not technical at all kwenye hizo area walizopewa pamoja na exposure za upendeleo,
Labda tatizo ni mentors na wenyewe hawana uwezo pia, ndio maana nchi inatumia muda mwingi kuzalisha viongozi magarasha.