Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaama ajirusha kutoka ghorofani na kufa kutokana na kukosa ajira

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Police wamesomba waliokuwa wanapiga picha.

Habari kamili inakuja. Picha zimekataa kuupload. Ila nimeattach kwenye comment no 6 na 7.
Kuna mdogo wangu mmoja nae alipitia kipindi kigumu sana cha kutokua na ajira, na pia yeye alikua pia na tatizo la kiafya ambalo lilikua linsumbua sana. Siku moja nimempigia naongea nae, analia machozi anasema yeye anataka kujiua.
Nikapanga kesho kutwa nae nikaonana nae; Siku ya kwanza nikampitisha pale Ocean road hospital, tukazunguka mawodini, sikuongea neno lolote bali nilimwambia kuna jamaa yangu kalazwa hapo namtafuta, ila sijui yupo wodi gani. Hali za wagonjwa aliokutana nao mule ndani, alibaki mdomo wazi. Tukatoka pale, nikamwambia twende muhimbili, inaonekana jamaa wamemuhamishia muhimbili... Nikapita nae mule pia kama wodi mbili hivi... Halafu kutoka pale nikaagana nae, kila mtu akarudi kwake.
Kesho yake akanitumia meseji akaniambia kaka nimekuelewa sana, upuuzi wa kufikiria kujiua siwezi kufanya tena, nitapambana so long as ninaishi na nina uwezo wa kutafuta.
Anyways, aende kwa amani.
 
Katiba mpya na time huru vijana piganieni Sana Sana.Kama mtabaki hivyo hali itakuwa mbaya kupita kifani.Wana jeuri sn CCM hasa hawa wa sasa wakiongozwa na huyu hopeless
 
Uchambuzi mzuri uliotukuka
 
Ndio ujiue jamani? Usomi wake umemsaidia nini, alikuwa anatambua kabisa kuwa ajira ni ngumu..ameshindwa kujiajiri mwanaume mzima?

Ulimpa huo ' Mtaji ' akashindwa ' Kujiajiri ' huko? Mlioshiba ( Matajiri ) acheni kuwa na ' dhihaka ' kwa Watu Masikini / Makapuku. Watanzania wengi wasio na Ajira wana ' Business / Project Ideas ' nyingi mno tu ila wengi Wao kinachowaumiza tu ni upatikanaji wa ' Mitaji ' na ndiyo Watu wengine kama huyu Mwenzetu aliathirika ' Kisaikolojia ' akaamua kukifanya alichokifanya. Binafsi sijafurahishwa na huku ' Kujiua ' Kwake japo kwa Mazingira aliyokuwa nayo na hali ilivyo ilikuwa ni rahisi sana kwa Shetani kumuingia na ' Kushawishika ' katika ' Kujimaliza ' huko.
 
Kiongozi nadhani hawalijui hili kama sehemu tu ya kufanyia field practical/ ya kujitolea tu inakuwa ni shida kuipata sembuse hiyo ya kujishikiza? hivi wadau wanapolalamika kwamba ajira zimekuwa ngumu wenzetu hawa sijuwi hawaoni hali halisi ilivyo.
Mambo yako live sana kitaani huku!
 
Nyinyi mliobakia ambao mmemaliza hadi leo hamjapata kazi msiwe na fikira potofu kama za mwenzenu
Naigeria watu wana mastaz na wanauza nyanya sokoni
Mtakuwa nyinyi na vidigrii vyenu tena hata kingereza hamjui nani awape kazi
 
Mkuu,hakika una hekima za mfalme Suleiman, yaani hekima yako haifanani kabisa na CCM,Nakushauri uhame CCM mkuu,umeongea maneno mazito yamenigusa sana.
Hakuna mwana CCM zaidi ya Nyerere,Kikwete na wewe GENTAMYCINE BIN ANTIBIOTIQUE pekee ndo wenye hekima.
Yaliyobakia ni mapopoma tupu
 

Shukran na Akhsante sana Mkuu. Nimezipokea pongezi / kongole zako kwa mikono miwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…