Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Ukisoma vitabu vitakatifu vya Biblia na Quran tukufu, utajionea mwenyewe kuwa Mungu alikuwa anawasilisha ujumbe wake kwa watu kabla ya kufanya jambo.
Ni bahati mbaya sana kwa upofu waliopewa watu na Shetani huwa ni wagumu sana kupata ujumbe wa Mungu pale unapowasilishwa kwao.
Mimi Lord denning wa JF sio Nabii ila kwa kumjua kwangu Mungu kidogo sana niliweza kulinganisha mateso aliyokuwa anayapata Yesu kuelekea kuhukumiwwa kwake kwa Makosa ya Uongo, Kuuwawa na Kufufuka na matukio yanayompata hivi karibuni Tundu Lissu. Uzi wenyewe huu hapa chini👇
www.jamiiforums.com
Kwenye uzi huu, nilielezea vizuri vitu ambavyo nimeviona na mambo niliyoona yanaashiriwa na matukio haya.
Leo kwenye pitapita zangu za YouTube nimekutana na ujumbe mzito alioutoa mtumishi wa Mungu anayejulikana kwa Jina la Prophet Edmund Mystic.
Kilichonishangaza, ujumbe alioutoa mtumishi huyu hautofautiani sana na mambo niliyoona yanahusiana na Tundu Lissu hivi sasa.
Mtumishi huyu wa Mungu amerejea Unabii alioutoa mwaka jana kuhusu farasi wawili kuwa kwenye mashindano na amesema Watanzania tusimchukulie poa Tundu Lissu maana Mungu amemwambia ni Mtumishi wake na yupo kwa ajili ya kusudi lake.
Mwisho Mtumishi kamaliza kwa kusema Tukimpoteza Lissu tutajuta sana.
Rai yangu kwa Watanzania ambao at least mnaamini kuwa Mungu yupo, tumuombee sana Tundu Lissu kusudi la Mungu kwake katika kuikomboa Tanzania likapate timia.
Muwe na usiku mwema

Watanzania tusali sana: Kukamatwa na Kushtakiwa Tundu Lissu Kuelekea Pasaka ni tukio lingine lenye Unabii Mzito kwa Tanzania
Leo tukiwa tunaelekea Alhamis Kuu, Ijumaa Kuu pamoja na na Pasaka, Mwanasiasa Mashuhuri nchini Tanzania, Tundu Antipas Lissu amefikishwa Mahakamani Jijiji Dar es Salaam na kushtakiwa kwa Makosa ya Uongo na Kutunga ya Uhaini pamoja na Uchochezi. Tundu Lissu ameshtakiwa kutenda makosa haya na...