Mhubiri mwingine atoa Unabii mzito juu ya Tundu Lissu na Tanzania

Huyo Mhubiri hamuogopi Hangaya??? Maana Hangaya alikataza viongozi wa dini kuongelea siasa.
 
Tundu Lissu anatajwa sana kama Mjumbe wa Mungu. Yule mama ni Mjumbe wa Waarabu wa Dubai
Napenda sana mentality hii ya chadema sababu inarahisisha kazi.......inakuwa nuepesiiiiii. Wakati mnatafuta sifa kama hizi za kijinga humu (dini), Kuna watu wako serious nazo kweli kweli. Nchi hii hakuna atakayefanikiwa abadan kwa kulitenga na kulibagua kundi flani la kidini. Tujifunze hilo kutoka kwa Nyerere.
 
Mtumishi huyu ya Mungu amerejea Unabii alioutoa mwaka jana kuhusu farasi wawili kuwa kwenye mashindano na amesema Watanzania tusimchukulie poa Tundu Lissu maana Mungu amemwambia ni Mtumishi wake na yupo kwa ajili ya kusudi lake.
Kadiri mnavyomtaja kinafiki Mungu, ndivyo anavyozidi kuwapiga laana. Yaani Tundu lissu aliyejaa hila kibao ndani ya moyo wake umuhusoshe na Mungu?!!!! Aisee tuwe serious basi wakuu. Kufeli kwingine tunajitakia.
 
Dah kwa hiyo Tundu n nabii
 
Nani kalibagua kundi gani? Kwani Sheikh Ponda anayemuonya Samia na Utawala wake kila siku ni Mkristo?
 
Nani kalibagua kundi gani? Kwani Sheikh Ponda anayemuonya Samia na Utawala wake kila siku ni Mkristo?
Labda ungerejea, vizuri kabisa, comment ya niliyemquote pamoja na comments nyiiingi tu za watu wa upande wako (nyumbu) Ili ujionee ukweli wa ninayoyasema. Ukweli ni kuwa Kuna udhalilishaji flani mkubwa tu wa viongozi wa dini ya Kiislamu katika comments zao. Ikitokea wameshambulia viongozi tofauti na WA dini ya Kiislamu, unaona kabisa heshima katika mashambuliai yao. Lina itikadi hilo lichama Kwakweli, halitufai Watanzania.
 
Umewahi ona wapi Sheikh Ponda kadhalilishwa na wapenda Demokrasia? Au na Watetezi wa Haki

Viongozi wa Kiislam wanaodhalilisha ni wale wanaojiweka upande wa wanyonyaji hasa Bakwata. Hata kwa Wakristo wapo Viongozi wa Dini wanaosemwa vibaya na Wananchi kwa sababu ya kujiweka upande wa Watawala mfano ni Malasusa.
 

Ngoja akina Tlaatlaah waje kupinga. Lakini umewasilisha vema. Sijui ni kwa nini huko ccm hawapendi uchauguzi huu wa 2025 uwe huru, wa haki- free, fair and credible. Dhulumati hawezi fua dafu kila siku ya Mungu, 40 zake zinakuja tena mbio sana.
 
CCM walishajitenga na Mungu. Wao ukiwaona makanisani au na Viongozi wa dini we jua tu wanafanya maigizo kwa maslahi yao ya kisiasa.
Ngoja akina Tlaatlaah waje kupinga. Lakini umewasilisha vema. Sijui ni kwa nini huko ccm hawapendi uchauguzi huu wa 2025 uwe huru, wa haki- free, fair and credible. Dhulumati hawezi fua dafu kila siku ya Mungu, 40 zake zinakuja tena mbio sana
 
Tanzania ilisha kombolewa na Mwalimu Nyerere
Kama ilishakombolewa wapo wapi Ben Saanane, Mzee Kibao, Aphonce Mawazo, Deus Soka, Kipanya, Amani Manengelo?

Kwa nini mkawateka na kuwaua kama Nchi ilishakombolewa na Nyerere?
 
Ngoja akina Tlaatlaah waje kupinga. Lakini umewasilisha vema. Sijui ni kwa nini huko ccm hawapendi uchauguzi huu wa 2025 uwe huru, wa haki- free, fair and credible. Dhulumati hawezi fua dafu kila siku ya Mungu, 40 zake zinakuja tena mbio sana.
Kwa Neema na Baraka za Mungu, kwasabb ya udhaifu wa kimwili na kiroho, kiburi na kukosa hekima, Tundu Lisu hawezi kua na mamlaka katika serikali za wanadamu ulimwenguni, ispokua ataendelea kua kiongozi wa genge la waropokaji, vibaya na matapeli wa kisiasa tu wenye kibali cha shetani.

Kwa kifupi,
Lisu atakua kiongozi wa makhulukutabu daima, ndio maana ana hulka za akina kasongo yeye mobali nayooo,

huo ni ujumbe wa kinabii ajulishwe pia lisu mwenyewe 🐒
 

Lord denning achana na mchumia tumbo huyo, hakuna nabii hapo..mtu anayetumikia kusudi la Mungu hawezi kupotea, atasemaje tukimpoteza Lissu tutajuta, sisi ndio tuliomtuma Lissu.. au Mungu? tujutie nini km hatukumtuma..? hakuna nabii hapo, nyinyi mnadhani kazi ya Mungu ni mzaha, soma historia ya Mzee Kulola kwa mfano au Mwl. Mwakasege uone mtumishi wa Mungu mule anapita ktk kumtumikia Mungu, mtu hajulikani alizaliwa wapi, lini alianza kazi ya Mungu, ktk mazingira gani..ushuhuda wake kwa kifupi, ghafla tu mtu anajiita nabii ana kanisa tayari..peculiar! mbona haihitaji Roho kumtambua mtu wa aina hii..? Neno kuu kwa mtumishi wa Mungu ni watu waache DHAMBI! siyo kubashiri mambo ya uchaguzi na matukio ya kisiasa..ukiona wa hivyo jua huyo ni tapeli!​

 
Kwa kuwa umelewa uchama huwezi muelewa mtumishi wa Mungu. Kazi ya Watumishi wa kweli ya Mungu ni kufikisha ujumbe kama ulivyo.

Kama mnaona sio mtumishi kweli wa Mungu na kwa sababu Shetani kawapiga upofu muueni Lissu. Alafu Mtajua huyu sio mtumishi wa Mungu au la.

Nimekaa pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…