Mi natoa ONYO: Kuna Member wa Humu JF ana mahusiano na mchumba wangu. Tusije Kulaumiana Bure

Wewe umesema upo na huyo mchumba wako huu ni mwezi wa tano sasa inakuwaje unasema ulimsomesha chuo akamaliza???? Muongo wewe sema ushampenda mschana wa humu JF ila unasikia wivu alivyo karibu na member mwingine
 
Wambie mazee wakileta za kuleta radi ninayo njooo
 
Ina maana 2015 ulikuwa na demu mwingine???? Maana huyu umesema mwenyewe uko nae sasa mwezi wa tano!!!!!! Hata wewe ni muhuni tu kubali hivyo!!!
 
Hii story ya kutunga au jamaa alivyo kuwa anaandika alikuwa kajawa na hasira.....

Kwanza amesema yupo na Mchumba wake huyo sasa ni miezi 5 ..........
Sehem nyingine anasema Mchumba wake huyo muda mwingi yupo nyumbani kwani alisha maliza chuo miaka 2 iliyo pita.............
Sehem nyingine anasema ametumia gharama nyingi kumsaidia kwenye Elimu yake.

Kwahiyo kuwa na Mchumba kwa Miezi 5 unaweza fanya yote hayo.
 
Usijidanganye!!!! Gharama haziwezi kulipwa hata mahakamani utaulizwa UNADAI GHARAMA JE ULIOA, ONYESHA CHETI CHA NDOA" Kama huna wewe ni sawa na watu wanaohonga pesa michepuko huko nje ambapo ukitoa sahau kurudishiwa.
 
acha kulialia sasa unaishi na malaya hapo unapaswa ujue
 
nmegundua nyie watu mnaniombea mabaya sana..hamwoni kwua sasa ndo mnampa uthibitisho kabisa????????????????????????? nmewakosea nini mimi jamani mpaka mnaniombea mabaya hivi.......................
Anayeshikwa na ngozi ndio mla nyama sikuzote. Wanakuhisi wewe maana ndio bingwa wa kuleta story za kipuuzi na matusi. Lazima utakuwa wewe na utakoma ubishi ngoja akutie mikononi mwake.
 
Mkuu hapo huna mchumba. Piga chini tafuta mwingine coz mchumba anayecheka cheka kwenye social media sio mchumba huyo ni kahaba tu.Miez 5 imetosha kabisa kujua huyo sio mwanamke hafai. Piga Windows chini
Hawezi kukuelewa kushtaki tu anaashiria kafa kaoza sioni sababu ya kumlaumu mshikaji na dem wako unae
 
Ninavoina mimi mtoa mada wa uzi huu alikuwa anataka kupiga soga tu maana sijaona hoja zenye mashiko kwa kumtishia huyu anaemsumbua mwenza wako.
Watoto wa mtaani wanasema demu kama bahari we ukilinda KIGAMBONI wenzio BEACH KOKO wanogelea.


viWaNdA
 
Pole sana mkuu,haya mambo ya mahusiano ukikosea kuchagua utaumia sana,Anyway naamini huyo mchumba wako ndio anamakosa kama anajua ana mtu wake kwa nini ajilegeze na kujilengesha kwa mwanaume mwingine? Kama kweli unaushahidi wa kutosha nakushauri mpige chini huyo uendelee na maisha yako.
 
Unazunguka mbuyu wakati njia iko wazi!
Mwaga mchele kuku wapate chakula chao.
Na inaonesha hujiamini
Umesema umemsomesha chuo kwa kumlipia mpaka tuition fee wakati uchumba wenu una miezi 5 how comes??
Au kipindi unamsomesha chuo alikua Dada yako baada ya kumaliza chuo ndio amekua mchumba?
Since amemaliza chuo huu ni mwaka wa pili na nyinyi uchumba wenu una miezi mi5 huoni kama kuwa na jamaa mwingine ni very possible?
Bed performance is very important for strong relationship!
 
Jamaa kashindwa kabisa kuelewa kama kapata bahati mbaya

Yani agungwe kwa kuchekeshwa tu bado unamganda???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…