Hivi kuchaji hizi EV inaweza kutumia muda gani hadi kujaa ?
Kutegemea vitu viwili, system charge ya gari lako na charging station unayotumia.
Fanya mfano, una simu unataka ijae haraka. Kwahiyo simu itatengenezwa iweze kupokea power harakaharaka na pia lazima uwe na chaja yenye kutoa power kubwa.
Sasa kwenye magari ivo ivo. System charge zipo za kisasa siku hizi za 400kW architecture na za kisasa zaidi ni 800kW.
Za 400kW ukikutana na Fast charger inachaji kwa 0-80% kwa dakika 30 hivi wakati za 800kW kutoka 0-80% haizidi dakika 8.
Pia charging system zipo:
Level I ni slow charge AC, (hizi zina 2-3kW ni charger za home) kama unavyochomeka pasi home unachaji gari lako, itachukua karibia masaa 8-20 kujaa full charge.
Level II tunaiita fast charge AC, kwenye viwanda na unaweza funga home au maofisini ni 8-22kW zenyewe masaa 3-6 full charge.
Level III ndio fast charger DC ndio zinakua kwenye charging stations. Hizi zina 50-350kW na zinazidi kuboreshwa. Chini ya dk 20 ushafika full charge.