Miaka 18 ya upotevu wa maisha ya Yesu Kristo. Je, nini hasa siri yake na wanaficha nini?

Kwanini wachague hivyo 66 na 72 huoni ulakini hapo..?
 
Ni rahisi sana kuandika jambo ukajiona upo sahihi, lakini ni ngumu haswa kukisoma kitu hichohicho ulichoandika na kuona mashudu uliyoyaandika.

Umeandika kwa haraka kwelikweli, hebu kaa kwa kutulia ulete hayo majina yametamkwa ama yameandikwa wapi ili ueleweshwe. Kutokuelewa kunatibika[emoji3166]
 
Hivi hao the storybook kuna siku inaweza kutokea wakaelezea historia ya mtume Muhamad?
Dr Mambosasa Asante
Dr Mambosasa Asante naomba nijibu! Inaweza kutokea kweli?
Yeah nchi hii iko huru kwahyo kila mtu anaweza kujitafutia taarifa na kuziwasilisha kwa Jamii ilimradi anaamini amezipata taarifa hizo katika vyanzo vizuri vya taarifa visivyokuwa na shaka anaweza kueleza na sio Story book hata wewe kama utapata Taarifa yoyote kutoka vyanzo vya kuaminika unaweza ukasimulia
 
Kuna mahali imeshawahi andikwa labda unisaidie nikasome?
 
Natamani kujua neno kristo liliingiaje na lilimaanisha nini na kwanini waislamu hawalikubali
 
Natamani kujua neno kristo liliingiaje na lilimaanisha nini na kwanini waislamu hawalikubali
Dah Hakuna muislam ambae hakubali kwamba yesu ni kristo muislamu ambaye hakubali yesu ni kristo huwa si miongoni mwa waislamu na anakuwa amejitenga na uislamu na huitwa kafiri kwa kuwa amekufuru aya za M/Mungu ambazo humtaja yesu (Issa a.s) kama Kristo (Kiyunani) na Masihi (Kiarabu na kihebrew) ....So for conclusion Hakuna mwislamu asiyekubali ni neno ulojiwekea wewe mwenyew na unajichallenge wewe mwenyeww na unaconclude wewe mwenyewe (Some kind of theological illusion unayojipa na kuwawekea waislamu mipaka wasiokuwa nayo)

Na umesema unataka kujua neno christo liliingiaje ok
Neno Iousous christos au Yesu kristo
.."Ιησούς Ξ§ΟΞΉΟƒΟ„ΟŒΟ‚"...
liliosawa na neno la kiebrania Yehoshua Mashiach "..Χ™Χ”Χ•Χ©Χ’ Χ”ΧžΧ©Χ™Χ—.." au Yesu masihi likiwa linamaanisha Mpakwa mafuta (the anointed one to be the God's chosen for Kingdom like David na kuwa nabii kama kina samweli etc)
BIblia agano jipya imeandikwa kwa lugha ya kiyunani yaani Greek language kama utakuwa unafahamu kuhusu Septuagiant au LXX na baadae kwa kilatin vulgate...
Kwahyo kuna baadhi ya lugha zilikuwa adapted na kuwa changed kutoka kwenye matamshibyake ya awali na kuwa Matamshi mapya kwa mfano kutoka katika masihi na kuwa kristo....
NAFIKIRI UMEELEWA HAPO



 
Wameona wachukue Yale yanayofaa wangechukua yote wasingeyamaliza wala vitabu visingetosha
 
Kuna mahali imeshawahi andikwa labda unisaidie nikasome?
Ukitaka kujua kuhusu Yesu obvious utasoma kwenye Story za injili na Vitabu vya dini vya kanisa...Vilevile ukitaka kujua kuhusu Mtume muhamed kasome kweby Siratul Nabiyu (Vitabu vya sira ya mtume) vinavyoonyesha historria ya mtume...pia vitbu vya hadithi na historia ya dini vipo kibao go and read ..the way you read The history of jesus
 
Wameona wachukue Yale yanayofaa wangechukua yote wasingeyamaliza wala vitabu visingetosha
Sssa kwanini wameacha miaka 18 yote kwanini wasingechukua na yanayofaa kwenye miaka kuanzia 13 mpaka 30 inamaana kwenye miaka hiyo hakukuwa na yanayofaa Kweli?? Bhasi sio yote hata machache tu
 
Kipindi hicho Yesu alikuwa mafunzoni. Unakumbuka wale Mamajusi, waliropoka kwa mfalme Herode kwamba Mfalme amezaliwa. Na ndio hao waliomuonya Yusufu kuwa mtoto yesu hakuwa salama wamtoroshe. Wale mamajusi walikuwa kama kwa nyakati hizi tungewaita ni maprofesa kwani walikuwa wabobezi kwenye elimu ya utabiri na nyota. Tofauti na elimu ya leo ambayo tunasoma ili kushinda vikwazo vya mazingira yanayotizinguka. We study about matters and other living things sorrounding us. Sanasana, tumesoma yanahusu sisi ni nini na ni nani, basi tunasoma juu ya miili yetu, afya zetu na tiba zetu. Elimu ya zamani ili focus zaidi kwenye Roho, Mungu na miujiza (Spirityal knowledge). Walijua uwezo wa Roho ya mtoto Yesu ambayo kama angezaliwa kwao angelikuwa automatic ni kiongozi wao. Kwahiyo walipomwambia Herode kuwa Yesu ni Mfalme hawakukosea. Ila walijua pia lazima Yesu abatizwe( should be initiated) iliajue namna ya kuamsha utukufu aliokuwa nao autumie kuwaonyesha wengine namna kushinda kifo au awaongoze katika ya uzima wa milele. Kwa kuwa walimletea zawadi nyingi mtoto Yesu zikiwemo zile walizopewa na Herode kama mtego wa kumjua mtoto kazaliwa wapi. Wakawashauri Yusufu na mkewe, kwanza waliwafamisha wazazi kwamba mtoto waliomzaa sio wa kawaida na yuko hatarini. Pili kwa zile zawadi Yusufu na mkwewe wanauwezo wa kufanya maisha popote hivyo wamtoroshe mtoto. Lakini pia mtoto Yesu ni lazima akifika umri wa kujifunza basi wakabidhiwe wao jukumu la kumfundisha. Yesu alipofika umri wa miaka 13 na hasa siku alipowapotea wazazi wake wakitoka kusali Jerusalemu, wazazi walimtafuta wakamkuta yuko Sinagogini yuko katika ubishi mkubwa na Rabai(waalimu wa dini ya kiyahudi) wazazi walipomuuliza kwanini alikuwa pale aliwashangaa kwanini wanamtafuka wakati yeye yuko kwenye nyumba ya baba yake. Hilo liliwafanya wazazi wake kukumbuka ushauri wa wale Mamajusi. Yesu akapelekwa mashariki ya mbali kwa masomo kwenye chuo walichokuwa wanafundisha wale Mamajusi (wakufunzi wa utabiri). Elimu ilihusu Roho na Mungu msomi alipembua kwa wenzie kwa kuonyesha level ya juu kiroho(high level of spirual awareness) nguvu za miujiza (spiritual power he has) kumbuka hii sio kwa wakati wa Yesu tuu, ilikuwepo hawakati wa ushindani wa Filauni na Musa. Ili kuwakomboa wana wa Israel Musa alifanya miujiza mbele ya Filauni ambae nae aliamrisha washauri wake kushindana na Musa kimiujiza. Yesu kabla hajarudi alishatambua uhusiano wake na Mungu alipita vyuo mbalimbali kutoa mihadhala kwa Mungu ni nami na anaweza fikiwaje. Mihadhala ya mwisho aliitoa Ugiriki, watu wa mataifa mbalimbali na Wagiriki walimuusudu sana. Ndio maana mwishoni mwa maisha yake Wagiriki wamfuata Yesu Israel na hata maandishi ya kwanza kuhusu maisha ya Yesu yaliandikwa na Wagiri kwa Lugha yao. Ni kweli kuna maandiko kwenye biblia yamefichwa lakini kwenye tempo nyingi mashariki ya kati kuna simulizi za Yesu Mnazaleti. Mafundisho ya Yesu hayafanani na mafundisho ya dini kwa sasa. Mafundisho ya sasa yako kinadhalia wakati yeye alifundisha kwa vitendo. Mfano alitaka watu wamuabudu Mungu kwa njia ya Roho na Kweli. Yesu aliwabatiza wanafunzi wake kwa Roho, nao waliona maono kiroho na kutafukuli kivitendo vya Dunia. Mfano Mt.Yohana katoka visiwa vya Patmo alikuwa Rohoni maono ya Rohoni ameyaandika katika Ufunuo. Yesu alisema iliuuone ufalme wa Mungu ni lazima Uzaliwe mara ya pili. Kwanza, uzaliwe kimwili kwa Baba na Mama yako, lakini pili uzaliwe Kiroho katika Roho. Muulize Askofu au Papa kama wanajua namna ya kumbatiza mtu Kiroho hawezi. Jee hii njia ya Uzima wa Milele ikoje, inatembewaje? Hakuna mtu atakupa jibu. Ni kweli mafundisho yake yamefichwa kwani watu waliona namna ya kutengeneza fulsa. Kwenye kitabu kimoja nilisoma kuwa Yesu akitabiri juu ufichaji wa mafundisho yake, alisema na kuwaambia wanafunzi wake kuwa Mafalisayo watafanya njama ya kuficha mafundisho yangu ili watu wasijue namna ya kuingia Ufalmeni, lakini watakuta hata wao wamejifichia washindwe kuingia pia.

Kwa hiyo ni kweli biblia haonyeshi kipindi cha miaka 18 Yesu akikuwa wapi. Pia haonyeshi kama alikuwa ameoa alipata watoto. Kwa mila za Kiyahudi Yesu alipaswa kuwa na Mke. Ila nachofahamu hakuozwa na wazazi wake mila zinavyotaka. Ila akuwa na mke nae ni yule mwanafunzi wake Mary Magdalane ambaye licha ya kwamba wanafunzi wote walimkimbia Mary na Mama yake Yesu nae akiitwa Mary walikuwa na Yesu mwanzo mpaka mwisho wa mateso na kifo lakini ndie alishiriki mazishi na ndie aliyetokewa na Yesu na kupewa maagizo ya kutaka wanafunzi kuendeleza mafunzo. Inathibitisha kwenye kitabu chake ambacho hakipi kwenye Biblia. "Kwenye mkutano wa kwanza baada ya kuwakusanya wanafunzi, akasimama Peter akasema, Dada yetu Mary sisi sote twajua wewe ulikuwa kipenzi cha Masihi na mtu wa karibu jee ni kitu gani unakijua ambacho Masihi hakuwahi kutufindishe ile wewe alikufundisha. Ndio vingi tuu, Mary alijibu na akasema ...." Kwenye kitabu Mary alitiririsha nondo za kiroho mpaka Luka akaona wizu ikaleta sintofahamu.

Nasema Yesu hakuozwa bali alijitwalia mke kwanini? Yesu alitengua mila na Desturi nyingi za Kiyahudi, ndio maana alitengwa na alioigwa hakurusiwa kusiriki ibada kwenye masinagogi.

Wayahudi walijiona ni watu bora na wateule wa Mungu hivyo waliwabagua wasio Wayahudi hasa wa Israel wanzao wasio amini katika Uyahudi wale wakiitwa Wasamaria. Yesu hakuwatenga, na hata Mary alikuwa Msamaria( yule mwanamke aliyekutananae kisimani) soma Yohana 4:1-24.

Yesu akimwita Mungu kuwa ni Baba yake, wakati kiyahudi ni kufulu "Usilitaje bure Jina...." hasa wakijua amezaliwa na Maria, waliona anamtukana Mungu kwamba anamaana Mungu alizini na Maria. Wakati wao wanajua alikuwa mtoto wa fundi seremala.

Wayahudi walikuwa na mfume dume, walikuwa watengani na wanawake wale huwezi ukafanya maongezi na mwanamke, labda awe Dada, mama au shangazi. Ndoa zilipangwa na wazazi. Yeye marafiki wengi na hata wanafunzi wake walikuwa ni mchanganiko, wanawake, wanaume, wayahudi, wasamaria na mataifa mengine.

Yesu hakuheshi Sabato siku ambayo hakupaswa kufanya kazi yeye alifanya matendo ya Uponyaji.

Yesu hakuamini kwa haki ya kilipana visasi, jino kwa jino, jicho kwa jicho.

Alimuokoa mwanamke mzinifu ambaye kwa mila na desturi alipaswa kupigwa mawe hadi afe.

Wayahudi waliani kwenye extended family value, family always stay together, Yesu aliikana familia yake hadhalani.

Kwa uvunjifuu Yesu hakuozwa kama angeozwa basi ilikuwa ni jukumu la Yusufu na Maria mke. Yeye akuwa na Mary Magdalane mwanamke msamaria waliekutana nae kisimani, kwenye Biblia imeandikwa wanafunzi wake walipo rudi na kumkuta akiongea Mwanamke walishituka.

Uvunjifuu huu wa mila na desturi ndio zilizo mpelekea kupata wafuasi wengi ambao badala ya kwenda kusali masinagogini ambako wangeleka zaka madhehabuni na kuwa ipato cha Makuhani watu waliamua walimfuata Yesu alipo na kusikiliza mafundisho yake.

Pia watu walishawishika kumfuata Yesu kwa tatuzi za kisheria na matatizo ya kijamii. Watu hakwenda kwenye baraza Mafalisayo, hivyo kupelekea upungufu wa kipato cha Mafalisayo.

Makuhani na Mafalisayo baada ya kuona mapinduzi ya yesu katika jamii, na hasa kuwekwa bila kazi na kunyimwa kipato wakajenga chuki dhidi ya Yesu na kumlianjama ya kubambikia keshi ya Uhaini kwa Pirato.

******** Mwisho ******
 
Maandiko matakatifu hayafichi kitu chochote kile kuhusu maisha ya ujana ya manabii, walimu ma mitume wote wanaotambulika ndani yake. Maandiko huanza kuwagusia kidogo walipokuwa katika maisha yao ya utoto, na kisha hufuata simulizi kidogo katika maisha ya ujana wao, na hatimaye sehemu kubwa ya matendo makuu ya Mungu yaliyothibitika ndani yao huzungumzwa kwa kina wanapokuwa vijana wakomavu wenye umri wa miaka 30 ama zaidi umri huo, pale wanapoihesabika kuwa ni watu wazima.

Huu ndio msingi uliowekwa kupitia torati ya Musa na manabii. Labda turejee msingi huo kupitia nukuu ifuatayo hapa chini,

Hesabu 4:30

"Tangu aliyepata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini, utawahesabu, kila atakayeingia katika huo utumishi, ili kufanya kazi ya hema ya kukutania"

Kwa hiyo maandiko matakatifu huangalia muhusika anaanza lini kazi yake ya utumishi ile aliyoitiwa na kupamgiwa na Bwana, na wala haitilii maanani kuhusu simulizi za kina za maisha yao ya awali, hasa yale ya ujana wao. Yenyewe huangalia aina ya huduma, na muhusika ameitwa na Bwana kufanya nini, na kwa wakati gani, na nini ni matokeo ya kile alichoitiwa kwa wahusika waliokusudiwa.
 
Aah kumbe ni wakati wa kuutafuta ukweli katika hiyo miaka iliyopotea
Yesu aliianza rasmi kazi iliomleta Duniani akiwa na miaka 30. Maandiko katika bible ni muongozo wa Mungu mwenyewe. Wahusika hawakulazimika kuandika taarifa kipindi hiko ambacho kazi haijaanza. Utotoni pia ukifuatilia haikuelezewa sana kwa sababu hiyo hiyo. Kilichoelezwa utotoni ni kuonyesha ujio wake na utofauti wake. Baada ya hapo ni ripoti ya kazi.
 
Kwahiyo utakubaliana na mimi kwamba yesu ameanza kuwa masihi(Kristo) Baada ga kufikisha Miaka 30 na miaka mingine yoyote ya nyuma alikuwa kama mwanadamu mwingine...?
 
ok Sawa kwahyo Yesu alikuwa Anointed "Masihi" ama kristo sio kwa kuzaliwa bali kwa kuteuliwa na Bwana kipindi cha kuanzia miaka 30 ya uhai wake...kama sijakunote vibaya...
 
Perfect Comments ever πŸ‘πŸ‘πŸ‘ Nidai Soda
 

Mkuuu yesu kaingia kanisani??! Bibilia gani inasema ivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…