Miaka 18 ya upotevu wa maisha ya Yesu Kristo. Je, nini hasa siri yake na wanaficha nini?

Miaka 18 ya upotevu wa maisha ya Yesu Kristo. Je, nini hasa siri yake na wanaficha nini?

Kama wewe ni mkristo/ umezaliwa familia ya kikristo au uko interested na mambo ya kikrsto kuna maandiko matatu,,,,1..Walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu nami niko kati yao 2..Lolote mtakalolifunga duniani na mbinguni limefungwa na lolote mtakalolifungua duniani na mbinguni limefungwa. 3...Kuzimu na uharibifu vi wazi mbele za BWANA; si zaidi basi,mioyo ya wanadamu??? Kama unasoma biblia sahihi utajua hayo yameandikwa wapi... Maana yangu ni hii :-

Kwamba vitabu vilivyopitishwa na hao unaowaita wazee wetu walikuwa na lengo na hawakuwa wenyewe,,zaidi hawakufanya chochote kumfurahisha mtu au kwa manufaa binafsi ila walikuwa na lengo la kumfanya mtu kumjua MUNGU na malengo yake dhidi ya binadamu...Na ndio maana watu wasiotaka imani iwe ndio centre ya maisha yao kwa ujumla wanaona wale wazee makini walikosea compilation ya vitabu vilivyokubaliwa kwa pamoja kuwa mwongozo wa IMANI.....Old Testament 39....New Testament 27 Lakini walikaa pamoja na wakakaa kamati ilioongozwa na ROHO MTAKATIFU ili wasije wakafanya jambo ambalo lipo kwa ajili ya kumfurahisha binadamu na sio kumsaidia binadamu...

Katika pseudepigrapha kuna vitabu kama the book of Adam and Eve,,Enock,,Melchizedek,,jubilee ,,, testament of solomon nk nk.

Apocrypha kuna esdras,,bel and dragon,,tobith,,judith,,book of tomas nk

Hapo juu umevielezea vizuri kabisa as falsely atributed works na established copies or transcripts of certain text,,,kwamba ni vyenye mapungufu....Maana yake havitoshi na sio tu kwamba havina uvuvio wa Roho mtakatifu pia mengi yalioandikwa humo sio maneno ya MUNGU.Kweli kuna vitabu kama waamuzi na samuel kumetajwa kitabu cha Yashari...Lakini pameandikwa kwamba '''Mambo yaliosalia ya mfalme ahabu hayakuandikwa kwenye kitabu cha Yashari???"""lakini hakujatolewa ulazima wa kukisoma au kukijumuisha kwa sababu hio yashari ilikuwa kama kitabu cha tarehe na kumbukumbu ya matukio,,,,

Zaidi sana hiki kitabu cha Yashari nilicho nacho mimi naamini sio Yashari original kimejaa hizo (falsely atributed works) na sio kitabu cha kiimani (ndio nathubutu kusema kinawafaa watu wa FACTS zaidi) same kwa Enock,,melkizedeck tomas na vitabu vingine ambavyo vimeandikwa kwa ajili ya biashara na mashindano ya bestselling zaidi ya kumsaidia mtu kumjua NA kumfanya MUNGU kuwa centre ya maisha yake...Au naweza kusema walioviandika walikuwa na lengo la distraction ili mtu asijue lengo hasa la MUNGU kwa mwanadamu lilikuwa ni nini.

Mimi siamini kama kuna mtu wa IMANI atasoma yashari apate kitu au Enock au melkizedech vimeandikwa uwongo ambao haujajificha... Mfano eti! Musa alienda kuomba ushauri kwa Nuhu au Tera alikuwa mkuu wa majeshi ya Nimrodi,,,Huu si tunaweza sema ni upumbavu mtupu na kupoteza mda(total wasting of time).

Kitabu cha biblia,,mimi ni mprotestant kina vitabu 66 na iko na lengo moja tu kumfanya mtu yeyote aliemwamwini YESU KRISTO kama njia,,kweli na Uzima kuwa karibu na MUNGU,,kumjua na kuwa maisha ya haki na mategemeo ya kiimani kuishi maisha mapya baada ya haya tunayoishi,, kama WAFALME NA MAKUHANI...Kwa hio tukiitafuta FACTS tunaitafuta katika lipi lililo jema na lipi lililo baya,,,na zaidi katika Maisha ya kiimani kuna kuamini neno la MUNGU kupractise imani ili iwe Reality..

Wewe ukiwa ni MKRISTO maandiko yako huwa yanakuelezea na haihitaji forensic science kujua huu uzi ni wa mkristo au asie mkristo mtu akiusoma uzi wako ataiona chuki yako iliojificha dhidi ya maandiko na imani ya kikristo,, kwa hio,, reaction imesemwa huwa equal and opposite. kwa hio action yako ya kuleta kuwaambia wakristo wanatakiwa wautafute ukweli pengine as if hawaujui kila mmoja atakuja na mtazamo wake,,kama mimi nilivyokuona kwamba huujui ukweli na hutaki kuujua na unadhani kila mmoja anafikiri kama wewe.

Kumtaja Roho mtakatifu kuwa kuna maandiko kayafanya sacred na yakawa mwongozo haimake sense(ambapo ni kwako tu hakuna hio sense) na unajaribu kutafuta fact kwenye vitabu vingine.

Naweza kusema Fact is inversily proportional to faith,,mfano Musa aliambiwa apige fimbo yake kwenye maji na bahari ikagawanyika(FAITH) Kama MUSA angekuwa mtu wa fact asingepiga ile fimbo kwenye maji,,,Elisha alitupa tawi la mti kwenye maji na shoka (chuma) kikaelea juu ya maji(FAITH) Daniel,,azaria na mishael walitupwa kwenye Furnace yenye uwezo wa kuyeyusha chuma hata Tungsten carbide lakini hawakuungua wala harufu ya moto au moshi haikuwapata(FAITH) Mwanamke Sara ambae alikuwa amepita hata menopouse stage BIBI mkongwe alizaa mtoto (FAITH) YESU KRISTO kafanya mambo yasiohesabika mpaka kumfufua mfu(FAITH) kwa hio swala la facts lipo kwenye vitabu vya phisycs labda kidogo na mathematics..Faith ni gate la mahusiano ya MUNGU NA MWANADAMU...Huwezi kumpata MUNGU kwenye fact,,,,hata YESU amesema ukiijua kweli sio ukiijua fact,,,na hio kweli pia huwezi ipata bila mwongozo wa ROHO MTAKATIFU.Na HOLY SPIRIT Ni real,,yupo na anaongea.....
Kwanini wachague hivyo 66 na 72 huoni ulakini hapo..?
 
Utata unakuja hapo walipoanza kumuita Yesu/jesus mbadala wa jina lake halisi.

Huo uhuni wa kubadiri majina ya manabii na wahusika wa matukio upo ktk biblia tu ni maajabu haya, hata Qur'an na vitabu vingine ama dini zingine na hata historia za kawaida hutoona kubadirika kwa majina ya wahusika kwa visingizio kuwa wametafsiri kutoka ktk lugha fulan,

Kwanini wahindu ama waislam wasimbadiri muhamad ama Allah asiitwe kwa majina ya uswahili ama huko uzunguni wasiwabadiri mitume wa uislamu kwa lugha zao wanazoelewa?

Je inawezekana vipi mtu anaeitwa Juma hapa Tanzania akienda china abadiri jina eti aitwe kichina, na akienda uingereza aitwe kwa lugha wanayoitafsiri jina la Juma? Na akienda uturuki wabadiri tena hamuoni kuwa huo ni mchezo mchafu wa kuficha jambo hapo?

Huyo yesu ni aina ya kiumbe chenye majina meengi hapa dunian na ktk dini kulko kiumbe chochote, maana wanadini wanataka kutuaminisha mambo yasiyowezekana.

Ni kweli maisha ya huyo yesu ni mengi hayajulikani, na sio kujulikana tu bali kutafsirika.

Kikawaida ukiisoma biblia kwa macho ya upembuzi utagundua kuwa kuna wakina yesu zaid ya mmoja humo wamechanganywa,

Kwa mission aliyotumwa hapa dunian haikuwa ya kuja kuishi kwa miaka 33 bali zaidi ya 55, maana kikawaida cheo chake ama mission yake ya Utume ilikuwa aanze baada ya kufikisha miaka 25 na kustaafu miaka55, lkn maajabu ya watafsiri wakaweka maneno yao ya uongo.

Pia kuna mengi hayajawekwa wazi kuhusu wale mitume wake kuwa walikuwa 13 kutoka ktk kabila 13 za waisraeli[emoji23][emoji23].

Ni mengi yamefichwa ktk biblia kwa kujua ama kutokujua sababu kuu ya kutokujua ni kuchakachua kitu walichoshindwa kukichakachua.

Biblia ukiisoma nje ya mahaba ya dini na vifungo vya mashetani ya kidini basi utagundua mengi sana.

Hakukuwa na haja ya kubadiri majina ya huyo mwana wa Mungu na kumuita Yesu sjui jesus mala yeshua, wangeacha tumuite majina yake halali.

Jiulizen kama maandiko yalikataza kubadiri ama kuongeza lolote kwanini hawa wafia dini waliongeza upuuzi wao waliouona ni bora? Kutafsiri maana ya sentensi na historia sio mbaya, lkn kubadiri majina ya wahusika huo ni uhuni na ushenzi kama sio ujambazi.

Yesu ama jesus hajawai kuwepo, hajawai kuwepo maana ilo jina halina muhusika kutoka historia yoyote hapa dunian ndiomaana hata uwepo wake unamikanganyiko kuanzia ktk biblia yenyewe, mpaka kwa walioicopy biblia hao wanaomuita issa bin mariam, wote waongo wakubwa.

Historia za watu wa kale, imechezewa mno, imeharibiwa sana, Yesu hatorudi mtamsubiri sana, maana haiwezekani kitu kilichoundwa kwa kufananisha na mtu mwingine mseme kiumbe hiki kiwepo haiwezekani.

Someni sana maandiko nje ya dini zenu mtaelewa hili jambo, View attachment 2459327
Ni rahisi sana kuandika jambo ukajiona upo sahihi, lakini ni ngumu haswa kukisoma kitu hichohicho ulichoandika na kuona mashudu uliyoyaandika.

Umeandika kwa haraka kwelikweli, hebu kaa kwa kutulia ulete hayo majina yametamkwa ama yameandikwa wapi ili ueleweshwe. Kutokuelewa kunatibika[emoji3166]
 
Hivi hao the storybook kuna siku inaweza kutokea wakaelezea historia ya mtume Muhamad?
Dr Mambosasa Asante
Dr Mambosasa Asante naomba nijibu! Inaweza kutokea kweli?
Yeah nchi hii iko huru kwahyo kila mtu anaweza kujitafutia taarifa na kuziwasilisha kwa Jamii ilimradi anaamini amezipata taarifa hizo katika vyanzo vizuri vya taarifa visivyokuwa na shaka anaweza kueleza na sio Story book hata wewe kama utapata Taarifa yoyote kutoka vyanzo vya kuaminika unaweza ukasimulia
 
Kuna mahali imeshawahi andikwa labda unisaidie nikasome?
 
Ililichukua kanisa miaka isiyopungua 500 kujadili mambo mbalimbali kuhusu Yesu, na kipi kiwemo kwenye biblia na kipi kisiwemo na kipi kiandikwe na kiandikwe vipi na kipi kiachwe kabisa na kisizungumzwe tena Na wengi hawajui kuwa kuandikwa kwa biblia ya sasa kulichukua miaka mingi sana ,Huku pia kanisa likijadili Yesu anatakiwa kuonekana vipi mbele za jamii...
Natamani kujua neno kristo liliingiaje na lilimaanisha nini na kwanini waislamu hawalikubali
 
Natamani kujua neno kristo liliingiaje na lilimaanisha nini na kwanini waislamu hawalikubali
Dah Hakuna muislam ambae hakubali kwamba yesu ni kristo muislamu ambaye hakubali yesu ni kristo huwa si miongoni mwa waislamu na anakuwa amejitenga na uislamu na huitwa kafiri kwa kuwa amekufuru aya za M/Mungu ambazo humtaja yesu (Issa a.s) kama Kristo (Kiyunani) na Masihi (Kiarabu na kihebrew) ....So for conclusion Hakuna mwislamu asiyekubali ni neno ulojiwekea wewe mwenyew na unajichallenge wewe mwenyeww na unaconclude wewe mwenyewe (Some kind of theological illusion unayojipa na kuwawekea waislamu mipaka wasiokuwa nayo)

Na umesema unataka kujua neno christo liliingiaje ok
Neno Iousous christos au Yesu kristo
.."Ιησούς Χριστός"...
liliosawa na neno la kiebrania Yehoshua Mashiach "..יהושע המשיח.." au Yesu masihi likiwa linamaanisha Mpakwa mafuta (the anointed one to be the God's chosen for Kingdom like David na kuwa nabii kama kina samweli etc)
BIblia agano jipya imeandikwa kwa lugha ya kiyunani yaani Greek language kama utakuwa unafahamu kuhusu Septuagiant au LXX na baadae kwa kilatin vulgate...
Kwahyo kuna baadhi ya lugha zilikuwa adapted na kuwa changed kutoka kwenye matamshibyake ya awali na kuwa Matamshi mapya kwa mfano kutoka katika masihi na kuwa kristo....
NAFIKIRI UMEELEWA HAPO

Wameona wachukue Yale yanayofaa wangechukua yote wasingeyamaliza wala vitabu visingetosha
 
Kuna mahali imeshawahi andikwa labda unisaidie nikasome?
Ukitaka kujua kuhusu Yesu obvious utasoma kwenye Story za injili na Vitabu vya dini vya kanisa...Vilevile ukitaka kujua kuhusu Mtume muhamed kasome kweby Siratul Nabiyu (Vitabu vya sira ya mtume) vinavyoonyesha historria ya mtume...pia vitbu vya hadithi na historia ya dini vipo kibao go and read ..the way you read The history of jesus
 
Wameona wachukue Yale yanayofaa wangechukua yote wasingeyamaliza wala vitabu visingetosha
Sssa kwanini wameacha miaka 18 yote kwanini wasingechukua na yanayofaa kwenye miaka kuanzia 13 mpaka 30 inamaana kwenye miaka hiyo hakukuwa na yanayofaa Kweli?? Bhasi sio yote hata machache tu
 
Kipindi hicho Yesu alikuwa mafunzoni. Unakumbuka wale Mamajusi, waliropoka kwa mfalme Herode kwamba Mfalme amezaliwa. Na ndio hao waliomuonya Yusufu kuwa mtoto yesu hakuwa salama wamtoroshe. Wale mamajusi walikuwa kama kwa nyakati hizi tungewaita ni maprofesa kwani walikuwa wabobezi kwenye elimu ya utabiri na nyota. Tofauti na elimu ya leo ambayo tunasoma ili kushinda vikwazo vya mazingira yanayotizinguka. We study about matters and other living things sorrounding us. Sanasana, tumesoma yanahusu sisi ni nini na ni nani, basi tunasoma juu ya miili yetu, afya zetu na tiba zetu. Elimu ya zamani ili focus zaidi kwenye Roho, Mungu na miujiza (Spirityal knowledge). Walijua uwezo wa Roho ya mtoto Yesu ambayo kama angezaliwa kwao angelikuwa automatic ni kiongozi wao. Kwahiyo walipomwambia Herode kuwa Yesu ni Mfalme hawakukosea. Ila walijua pia lazima Yesu abatizwe( should be initiated) iliajue namna ya kuamsha utukufu aliokuwa nao autumie kuwaonyesha wengine namna kushinda kifo au awaongoze katika ya uzima wa milele. Kwa kuwa walimletea zawadi nyingi mtoto Yesu zikiwemo zile walizopewa na Herode kama mtego wa kumjua mtoto kazaliwa wapi. Wakawashauri Yusufu na mkewe, kwanza waliwafamisha wazazi kwamba mtoto waliomzaa sio wa kawaida na yuko hatarini. Pili kwa zile zawadi Yusufu na mkwewe wanauwezo wa kufanya maisha popote hivyo wamtoroshe mtoto. Lakini pia mtoto Yesu ni lazima akifika umri wa kujifunza basi wakabidhiwe wao jukumu la kumfundisha. Yesu alipofika umri wa miaka 13 na hasa siku alipowapotea wazazi wake wakitoka kusali Jerusalemu, wazazi walimtafuta wakamkuta yuko Sinagogini yuko katika ubishi mkubwa na Rabai(waalimu wa dini ya kiyahudi) wazazi walipomuuliza kwanini alikuwa pale aliwashangaa kwanini wanamtafuka wakati yeye yuko kwenye nyumba ya baba yake. Hilo liliwafanya wazazi wake kukumbuka ushauri wa wale Mamajusi. Yesu akapelekwa mashariki ya mbali kwa masomo kwenye chuo walichokuwa wanafundisha wale Mamajusi (wakufunzi wa utabiri). Elimu ilihusu Roho na Mungu msomi alipembua kwa wenzie kwa kuonyesha level ya juu kiroho(high level of spirual awareness) nguvu za miujiza (spiritual power he has) kumbuka hii sio kwa wakati wa Yesu tuu, ilikuwepo hawakati wa ushindani wa Filauni na Musa. Ili kuwakomboa wana wa Israel Musa alifanya miujiza mbele ya Filauni ambae nae aliamrisha washauri wake kushindana na Musa kimiujiza. Yesu kabla hajarudi alishatambua uhusiano wake na Mungu alipita vyuo mbalimbali kutoa mihadhala kwa Mungu ni nami na anaweza fikiwaje. Mihadhala ya mwisho aliitoa Ugiriki, watu wa mataifa mbalimbali na Wagiriki walimuusudu sana. Ndio maana mwishoni mwa maisha yake Wagiriki wamfuata Yesu Israel na hata maandishi ya kwanza kuhusu maisha ya Yesu yaliandikwa na Wagiri kwa Lugha yao. Ni kweli kuna maandiko kwenye biblia yamefichwa lakini kwenye tempo nyingi mashariki ya kati kuna simulizi za Yesu Mnazaleti. Mafundisho ya Yesu hayafanani na mafundisho ya dini kwa sasa. Mafundisho ya sasa yako kinadhalia wakati yeye alifundisha kwa vitendo. Mfano alitaka watu wamuabudu Mungu kwa njia ya Roho na Kweli. Yesu aliwabatiza wanafunzi wake kwa Roho, nao waliona maono kiroho na kutafukuli kivitendo vya Dunia. Mfano Mt.Yohana katoka visiwa vya Patmo alikuwa Rohoni maono ya Rohoni ameyaandika katika Ufunuo. Yesu alisema iliuuone ufalme wa Mungu ni lazima Uzaliwe mara ya pili. Kwanza, uzaliwe kimwili kwa Baba na Mama yako, lakini pili uzaliwe Kiroho katika Roho. Muulize Askofu au Papa kama wanajua namna ya kumbatiza mtu Kiroho hawezi. Jee hii njia ya Uzima wa Milele ikoje, inatembewaje? Hakuna mtu atakupa jibu. Ni kweli mafundisho yake yamefichwa kwani watu waliona namna ya kutengeneza fulsa. Kwenye kitabu kimoja nilisoma kuwa Yesu akitabiri juu ufichaji wa mafundisho yake, alisema na kuwaambia wanafunzi wake kuwa Mafalisayo watafanya njama ya kuficha mafundisho yangu ili watu wasijue namna ya kuingia Ufalmeni, lakini watakuta hata wao wamejifichia washindwe kuingia pia.

Kwa hiyo ni kweli biblia haonyeshi kipindi cha miaka 18 Yesu akikuwa wapi. Pia haonyeshi kama alikuwa ameoa alipata watoto. Kwa mila za Kiyahudi Yesu alipaswa kuwa na Mke. Ila nachofahamu hakuozwa na wazazi wake mila zinavyotaka. Ila akuwa na mke nae ni yule mwanafunzi wake Mary Magdalane ambaye licha ya kwamba wanafunzi wote walimkimbia Mary na Mama yake Yesu nae akiitwa Mary walikuwa na Yesu mwanzo mpaka mwisho wa mateso na kifo lakini ndie alishiriki mazishi na ndie aliyetokewa na Yesu na kupewa maagizo ya kutaka wanafunzi kuendeleza mafunzo. Inathibitisha kwenye kitabu chake ambacho hakipi kwenye Biblia. "Kwenye mkutano wa kwanza baada ya kuwakusanya wanafunzi, akasimama Peter akasema, Dada yetu Mary sisi sote twajua wewe ulikuwa kipenzi cha Masihi na mtu wa karibu jee ni kitu gani unakijua ambacho Masihi hakuwahi kutufindishe ile wewe alikufundisha. Ndio vingi tuu, Mary alijibu na akasema ...." Kwenye kitabu Mary alitiririsha nondo za kiroho mpaka Luka akaona wizu ikaleta sintofahamu.

Nasema Yesu hakuozwa bali alijitwalia mke kwanini? Yesu alitengua mila na Desturi nyingi za Kiyahudi, ndio maana alitengwa na alioigwa hakurusiwa kusiriki ibada kwenye masinagogi.

Wayahudi walijiona ni watu bora na wateule wa Mungu hivyo waliwabagua wasio Wayahudi hasa wa Israel wanzao wasio amini katika Uyahudi wale wakiitwa Wasamaria. Yesu hakuwatenga, na hata Mary alikuwa Msamaria( yule mwanamke aliyekutananae kisimani) soma Yohana 4:1-24.

Yesu akimwita Mungu kuwa ni Baba yake, wakati kiyahudi ni kufulu "Usilitaje bure Jina...." hasa wakijua amezaliwa na Maria, waliona anamtukana Mungu kwamba anamaana Mungu alizini na Maria. Wakati wao wanajua alikuwa mtoto wa fundi seremala.

Wayahudi walikuwa na mfume dume, walikuwa watengani na wanawake wale huwezi ukafanya maongezi na mwanamke, labda awe Dada, mama au shangazi. Ndoa zilipangwa na wazazi. Yeye marafiki wengi na hata wanafunzi wake walikuwa ni mchanganiko, wanawake, wanaume, wayahudi, wasamaria na mataifa mengine.

Yesu hakuheshi Sabato siku ambayo hakupaswa kufanya kazi yeye alifanya matendo ya Uponyaji.

Yesu hakuamini kwa haki ya kilipana visasi, jino kwa jino, jicho kwa jicho.

Alimuokoa mwanamke mzinifu ambaye kwa mila na desturi alipaswa kupigwa mawe hadi afe.

Wayahudi waliani kwenye extended family value, family always stay together, Yesu aliikana familia yake hadhalani.

Kwa uvunjifuu Yesu hakuozwa kama angeozwa basi ilikuwa ni jukumu la Yusufu na Maria mke. Yeye akuwa na Mary Magdalane mwanamke msamaria waliekutana nae kisimani, kwenye Biblia imeandikwa wanafunzi wake walipo rudi na kumkuta akiongea Mwanamke walishituka.

Uvunjifuu huu wa mila na desturi ndio zilizo mpelekea kupata wafuasi wengi ambao badala ya kwenda kusali masinagogini ambako wangeleka zaka madhehabuni na kuwa ipato cha Makuhani watu waliamua walimfuata Yesu alipo na kusikiliza mafundisho yake.

Pia watu walishawishika kumfuata Yesu kwa tatuzi za kisheria na matatizo ya kijamii. Watu hakwenda kwenye baraza Mafalisayo, hivyo kupelekea upungufu wa kipato cha Mafalisayo.

Makuhani na Mafalisayo baada ya kuona mapinduzi ya yesu katika jamii, na hasa kuwekwa bila kazi na kunyimwa kipato wakajenga chuki dhidi ya Yesu na kumlianjama ya kubambikia keshi ya Uhaini kwa Pirato.

******** Mwisho ******
 
Habari za Mida hii Ndugu Zangu Naomba kuanza kwa kuwatakia Sikukuu njema ya Kuzaliwa kwa Yesu kwa wale wote wafuasi wa imani ya Kikristo na hope mnaenjoy sana Happy noela

Kabla ya yote ningependa kurejea Luka 1:1-3 Kama inavyosema;
..."Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu,kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo,nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu,.........,"

Miaka 2000 iliyopita katika Mji wa bathelehem ya Uyahudi Alizaliwa Mtoto Aliyepewa Jina la Yeshua/Yehoshua ama yesu au Issa unaweza kumuita utakavyoweza kuita kwa lugha yako ilimradi imani ibaki kuwa alizaliwa Mtoto Ambaye ni Mtu muhimu sana katika historia ya ukombozi wa Wakristo duniani,

Na maandiko yote Yameandika kuhusu yesu kuzaliwa kwake,Miujiza yake mafundisho yake kuishi kwake ,Kusulubiwa kwake na kufufuka kwake na hata kupaa kwake kwenda mbinguni.

Maandiko yote ya biblia yaliyopo yanaanza kuzungumzia yesu kuanzia alipokuwa anazaliwa mpaka akiwa na umri wa miaka 12 (Soma luka 2 yote,pia soma mathayo 2)

Lakini baada ya miaka hiyo 12 Biblia ikawa kimya mpaka tena pale ambapo yesu anatimiza miaka 30 ya maisha yake ndo tunaona yesu anaanza kutajwa tena,kipindi anabatizwa na yohana Mbatizaji..(luka 3:23,Marco 1;9 ,Mathayo 3 kuanzia aya ya 14 na kuendelea)

Lakini miaka yake yote kuanzia umri wa miaka 13 mpaka 29 hakuna sehemu yoyote ya biblia inayotaja maisha yake alikuwa wapi? Alifanya nini? Aliishi wapi? na ilikuwaje?
basi nitajaribu kupitia baadhi ya theory na nakala za vitabu ili tuende sawa katika kujibu haya

HOJA KWA UFUPI

Maisha ya yesu kipindi Akiwa hai hakuna aliyekuwa anayanakili ama kuandika maisha yake kwakuwa Maisha yake na injili hii imekuja kuandikwa Miaka 70 mpaka 140 baada ya kifo chake.
Japo inasemekana historia ya yesu ilikuwa inaelezwa kuwa Masimulizi kumhusu yesu yalikuwa yakifahamika kwa watu wengi Sana kwa muda mchache.
kulingana na Injili ya yohana Yesu alifanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja tu na kulingana na injili za ki"synoptikia" (synoptic gospels) Yaani Luka matayo na marko alifanya kazi kwa muda wa miaka 2 mpaka mitatu kabla ya kifo chake...
Japo kuliandikwa Vitabu vingi sana zaidi ya 100 kuhusu maisha ya Yesu lakini vitabu 4 tu vya injili ndiyo vilivyokubaliwa kuingia katika biblia rasmi iliyoamriwa kutumika...

Mengi tunayoyajua kuhusu yesu Tunayatoa katika vitabu vinne tu vya injili yaani marko,mathayo luka na yohana,japo vitabu vingine ambavyo havikuingizwa kwenye biblia bado vipo na vingi viko maktaba vimehifadhiwa kwa na unaweza ukaviita APOKRIFA GOSPELS na vina mambo mengi sana ambayo huwezi kuyakuta kwenye biblia na mara nyingi huwa hayaruhusiwi kuzungumzwa kwa uwazi na mengine utayakuta kwenye biblia..
Kwanini hawakutaka kuviingiiza kwa kisingizio cha KUVUVIWA ama canonical views ?.....
Baadhi ya Vitabu Hivyo vingine huzungumzia Maisha ya yesu akiwa na umri wa miaka 13 mpaka 29 kama kitabu cha The Gospel of Mary, Injili ya mtoto yesu na vinginevyo....

UCHAMBUZI

Dr.Elizabeth McNamer,Proffesor of theology and religious history wa rocky Mountain college Huko Billings Montana,
ambaye kwa Miaka 14 Amekuwa Mkurugenzi mkuu wa Bethsaida Biblical Archaeological Excavations in Israel ( Machimbo ya Kiakiolojia ya kiblia huko Israel) Pia ni proffesor maarufu kwa ufundishaji wake wa Maandiko huko Asia Na anaposcast yake kuhus Historia ya Biblia.Katika moja ya mahojiano yake aliwahi kunukuliwa akisema
"Ililichukua kanisa miaka isiyopungua 500 kujadili mambo mbalimbali kuhusu Yesu, na kipi kiwemo kwenye biblia na kipi kisiwemo na kipi kiandikwe na kiandikwe vipi na kipi kiachwe kabisa na kisizungumzwe tena Na wengi hawajui kuwa kuandikwa kwa biblia ya sasa kulichukua miaka mingi sana ,Huku pia kanisa likijadili Yesu anatakiwa kuonekana vipi mbele za jamii..."

Hiyo ni wakati akijibu moja ya maswali kuhusu kitabu chake cha Jesus and First-Century Christianity in Jerusalem by Elizabeth McNamer,

View attachment 2457658

Kutokana na kutokuonekana kwa historia ya Yesu Katika miaka 18, hii ni kuanzia miaka 13 mpaka miaka 29 kwenye biblia kumezua mijadala mingi sana katika Jukwaa la wana theolojia na wasomi wa dini wabobezi wa kikristo mpaka ikafika hatua Wakaunda theory zao ama hypothetical Views zao na Wote wakaipa majina miaka hii kama.. The lost years of Jesus Christ "Miaka iliyopotea ya Hostori ya Yesu kristo" na wengine waliita "The unaccounted years of Jesus Christ" Pia huitwa the silent years au the missing years ...

MILA NA DESTULI ZA KIYAHUDI KUHUSU MIAKA ILIYOPOTEA YA YESU NA CHANZO CHA NADHARIA

Hapa tutaangalia mila na desturi za kiyahudi kuhusu miaka hiyo inayosemekana kutokupatikana historia ya yesu Kama wewe ni mfatiliaji wa mila na desturi za kiyahudi na kiAramaiki utakuwa si mgeni wa maneno kama Bar-Mitzvah au Bat-Mitzvah..

Hizi ni mila kama mila za kwetu africa au kwetu huko uziguani,Au huko kwetu uzaramoni au umasaini na kwingineko...
Kwakuwa yesu alikuwa ni mmoja wa Wayahudi katika kabila la kiAramaic hivo alifata Tamaduni zote..

"Bar Mitzvah" maana yake halisi ni "mwana (wa kiume) mwenye amri." "Bar" ni "mwana wa kiume" katika Kiaramu, ambayo ilikuwa ni lugha ya watu wa Kiyahudi.
"Mitzvah" ni "amri" katika Kiebrania na Kiaramu.

"Bat" ni binti katika Kiebrania na Kiaramu. (Matamshi ya Ashkenazic ni "bas").

Kitaalamu,Maneno hayo humaanisha mtoto anayekua, na ni sahihi kabisa kwa mila za kiyahudi kumuita mtu kama "kuwa bar (au bat) mitzvah.

"Hata hivyo, neno hili linatumika zaidi ku sherehe za ukuaji zenyewe, na kuna uwezekano mkubwa wa kusikia kwamba mtu "ana bar mitzvah" au "alialikwa kwenye bar mitzvah."

Sasa sherehe hizi zikuwaje na zilimaanisha nini
Mtoto wa kiyahudi zamani hizo mpaka leo kwa kufata sheria za Musa (zilizopo kwenye talmud) Anapofikisha umri wa miaka 13 (kwa mtoto wa kiume) na miak 12 (kwa mtoto wa kike) huhesabika kama amekuwa na hufanyiwa sherehe hiyo ya Mitzvah ili ayavae majukumu yake mapya na ieleweke kwamba mtoto akishafanyiwa sherehe hii hawi tena chini ya uangalizi wa wazazi hiyo umaanisha kwamba hawi chini ya amri ya wazazi na ndo maana ikaitwa Bar/Bat mitzvah..

Na ni mujibu baba kufurahi na kumpa maneno mazuri ya wosia mtoto huyo kwani Baba amejitoa katika responsibikity za mtoto huyo kwahyo dhambi zake na maamuzi huwa yapo chini ya mtoto (hapo mwanzo kabla ya miaka 13 mtoto huwa chini ya kifungo cha miaka na wazazi wake hivyo dhambi na malezi yote huwa chini ya wazazi wake) sherehe hizi hufanyika siku ya sabato....

Na mtoto huwa na ruksa ya kwenda mahali popote atakapo..

(Rejea ya Tamaduni hii ipo katika kitabu cha Talmud na inafanywa na wayahudi mpaka leo)..

Mila hizi zinahusianaje sasa na upotevu wa maisha ya yesu kuanzia miaka 13-29?

Inasemekana kwamba baada ya yesu kuwa tayari amekuwa Bar-Mitzvah akiamua kwenda sehemu mbalimbali kutafuta Elimu huku akiiacha Yerusalem na kurafuta elimu sehemu mbalimbali za nchi zote duniani na Hatimae kurudi Akiwa na miaka 30
(Ambayo pia ni miaka ya Kuhubiri na utume kwa mujibu wa Talmud)

Katika miaka ya 1800-1900 kuliibuka nadharia "Hypothetical views" nyingi sana kuhusu the lost years of jesus christ,Japo wanatheolojia wengi wa kisasa yaani morden theologists wanasema kuwa Yesu aliishi Nazareth na alikuwa akifanya kazi na baba ake kama fundi selemala Japo hili linakosa ushahidi zaidi wa moja kwa moja wa kimaandiko kwenye biblia zaidi ya ushahidi wa mathayo 13:55 na Marko 6:3 japo ukiangalia vizur utagundua ni andiko moja lenye sentensi moja na lenye maana tofauti huku kwwnye mathayo limetajwa tofauti na kwenye marko limetajwa tofauti labda ni katika zile njama Dr Elizabeth McNamer alizokuwa akitueleza..sasa twende kwwnye nadharia hizo kuhusu miaka iliyopotea .....

1.EARLY THORIES (about early as possible as 70-1600 Ad)

Nadharia za awali Kuwa kuna uthibitisho gani unaounga mkono imani kwamba Yesu alisafiri maelfu ya maili kutoka Yudea hadi nchi nyingine?
Vyanzo vya kwanza kabisa vinatoka katika maandiko ya Injili ya Mathayo, Marko, Luka na Yohana. Bethlehemu ni mahali ambapo inaaminika kuwa Kristo alizaliwa, lakini Injili zinasema familia yake iliondoka mara baada ya hapo na kukaa katika mji wa Nazareti, kutimiza yale ambayo manabii katika Biblia walitabiri; kwamba Yesu ataitwa Mnazareti. Nazareti lilikuwa eneo tulivu, la kilimo na la uvuvi ambapo jamii iliishi maisha yasiyofaa, ikidokeza kwamba hadhi ya Yesu ilikuwa ‘Blue collar’ huku yeye na baba yake seremala

Yusufu wakipata riziki zao duni kama mafundi. Huku kukiwa na matarajio machache ya kazi, nadharia moja ni kwamba huenda Yesu alitafuta kazi fulani umbali wa maili tatu katika mji wenye shughuli nyingi wa Sepphoris katika eneo la kati la Galilaya katika Israeli ya leo, mji uliojulikana wakati huo kwa michoro yake maridadi sana iliyotengenezwa na Waruma. Kukiwa na fursa nyingi za kujenga nyumba na kuta,

Huenda mji huu ukawa ndio hatua ya kwanza kuelekea mahali panapoaminika kuwa mahali pa kuanzia kwa jitihada ya Yesu ya kupata nuru ya kiroho. Ikiwa kama vile wasomi fulani Wakristo wanavyoamini kwamba Yesu alitumia muda mwingi wa miaka hii ya kati akifanya kazi ya seremala katika Galilaya, kuna marejezo machache kuhusu hilo katika Biblia. Pengo la miaka kumi na minane katika maandiko limetokeza nadharia kadhaa za kushangaza, lakini hadi sasa hakuna iliyothibitishwa na ushahidi wa kutegemewa.

2.WALKABOUT (MATEMBEZI)

Nadharia nyingine ni kuhusu Yesu na miaka yake iliyopotea ni kwamba alienda ‘kutembea’ kutoka nyumbani kwao Nazareti. Ikiwa tukio hili linatokea Yesu alikuwa mvulana wa miaka 12, kwa hiyo kijana kama huyo anaonekana alikuwa na uwezo upi wa kihisia-moyo na ujuzi gani ili kuchukua safari kubwa na inayoweza kuwa hatari? Sawa endelea
Yaelekea zaidi alipokuwa akiishi Sepphoris, Kijana Yesu anaweza kuwa alipata ujuzi wake wa mapema wa ulimwengu kupitia lugha ya Kiaramu na kujifunza kusoma. Andiko moja linalodokeza hilo linapatikana katika Injili ya Luka, inayosema kwamba Yesu aliingia katika sinagogi na kusoma kitabu cha kukunjwa cha manabii. Wakati huu akiwa kijana, angepitia moja kwa moja unyanyasaji wa kijamii na kiuchumi wa wakulima wa Kiyahudi wa Kipalestina wa wakati wake, ambao alikuwa sehemu yao. Huenda ujuzi huo ndio uliomtia moyo Yesu kutafuta majibu katika ulimwengu wa nje na huenda ukawa na uvutano juu ya uamuzi wenye utata wa kuacha familia yake.

Wasomi wa elimu ya Historia ya kidini wanaamini kwamba
Yosefu baba wa Yesu alikufa alipokuwa na umri wa miaka 12 hivi na kwamba tukio hilo lenye kuhuzunisha ndio lilikuwa kichocheo kwake, akiwa bado mvulana mdogo, kuanza jitihada ya kibinafsi ya kupata nuru ya kiroho. 'Matembezi' haya yaliyodumu kwa takriban miongo miwili yanaweza kuwa yalianza muda mfupi baada ya kuwa na umri wa miaka 13. Ni katika umri huu hatari ambapo madai ya ‘mengi ya miaka 18 uya upotevu wa historia ya yesu’ huanza na nadharia nyingi za mahali ambapo Yesu alitumia miaka yake ya malezi kukua na kuwa mtu mzima ziko wazi kwa tafsiri nyingi.

Haidhuru Kijana yesu alikuwa na jukumu gani kwa mama yake na jamaa zake huko Nazareti,
ulikuwa uamuzi wenye kutatanisha kuwaacha watu wake wa karibu katika umri mdogo kama huo, alipokuwa akianza safari ya ajabu na hatari kwa miguu. Hata hivyo, baadhi ya Wakristo wanaamini kuwa miaka iliyokosekana haina matokeo madogo na ufunuo wowote kuihusu hauwezi kuleta mabadililko yoyote...

3.VATICAN'S SECRETS (Siri za Vatikani)

Kumekuwa na uvumi kwa miaka mingi kwamba Vatican ina ushiikilia ukweli huu kuhusu maisha ya Yesu na miaka kumi na minane iliyopotea,kwa madai kuwa Habari hizo zinaweza kubadilisha sana imani ya dini ya kikristo ya leo,
Hata hivyo hakuna kilichofichuliwa kuhusu kuwepo kwa hati hizo na kile ambacho Yesu alikuwa akifanya na mahali alipokuwa kuanzia umri wa miaka 13 hadi 30. Baadhi ya watafiti wanaamini kwamba alitumia miaka hii isiyo andikwa kusafiri kwenda Uingereza akiwa na 'Yosefu wa Arimathaya', huku wengine wanaamini alisafiri hadi India na Uajemi. Mwishoni mwa karne ya 19 msafiri Mrusi Aitwaye Nicolas Notovitch alidai kwamba aligundua maandishi ya kweli katika nyumba ya watawa huko India ambayo yalithibitisha kwamba Yesu alisafiri na kufundisha huko na kwingineko Mashariki.

ZIKO THEORY NYINGI SANA NITAENDELEA KUZINDIKA KADRI NIPATAVYO UWEZO

CLARIFICATION
To declare interest "Part of the story was done on wasafi Tv the "storybook"
Maandiko matakatifu hayafichi kitu chochote kile kuhusu maisha ya ujana ya manabii, walimu ma mitume wote wanaotambulika ndani yake. Maandiko huanza kuwagusia kidogo walipokuwa katika maisha yao ya utoto, na kisha hufuata simulizi kidogo katika maisha ya ujana wao, na hatimaye sehemu kubwa ya matendo makuu ya Mungu yaliyothibitika ndani yao huzungumzwa kwa kina wanapokuwa vijana wakomavu wenye umri wa miaka 30 ama zaidi umri huo, pale wanapoihesabika kuwa ni watu wazima.

Huu ndio msingi uliowekwa kupitia torati ya Musa na manabii. Labda turejee msingi huo kupitia nukuu ifuatayo hapa chini,

Hesabu 4:30

"Tangu aliyepata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini, utawahesabu, kila atakayeingia katika huo utumishi, ili kufanya kazi ya hema ya kukutania"

Kwa hiyo maandiko matakatifu huangalia muhusika anaanza lini kazi yake ya utumishi ile aliyoitiwa na kupamgiwa na Bwana, na wala haitilii maanani kuhusu simulizi za kina za maisha yao ya awali, hasa yale ya ujana wao. Yenyewe huangalia aina ya huduma, na muhusika ameitwa na Bwana kufanya nini, na kwa wakati gani, na nini ni matokeo ya kile alichoitiwa kwa wahusika waliokusudiwa.
 
Aah kumbe ni wakati wa kuutafuta ukweli katika hiyo miaka iliyopotea
Yesu aliianza rasmi kazi iliomleta Duniani akiwa na miaka 30. Maandiko katika bible ni muongozo wa Mungu mwenyewe. Wahusika hawakulazimika kuandika taarifa kipindi hiko ambacho kazi haijaanza. Utotoni pia ukifuatilia haikuelezewa sana kwa sababu hiyo hiyo. Kilichoelezwa utotoni ni kuonyesha ujio wake na utofauti wake. Baada ya hapo ni ripoti ya kazi.
 
Maandiko matakatifu hayafichi kitu chochote kile kuhusu maisha ya ujana ya manabii, walimu ma mitume wote wanaotambulika ndani yake. Maandiko huanza kuwagusia kidogo walipokuwa katika maisha yao ya utoto, na kisha hufuata simulizi kidogo katika maisha ya ujana wao, na hatimaye sehemu kubwa ya matendo makuu ya Mungu yaliyothibitika ndani yao huzungumzwa kwa kina wanapokuwa vijana wakomavu wenye umri wa miaka 30 ama zaidi umri huo, pale wanapoihesabika kuwa ni watu wazima.

Huu ndio msingi uliowekwa kupitia torati ya Musa na manabii. Labda turejee msingi huo kupitia nukuu ifuatayo hapa chini,

Hesabu 4:30

"Tangu aliyepata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini, utawahesabu, kila atakayeingia katika huo utumishi, ili kufanya kazi ya hema ya kukutania"

Kwa hiyo maandiko matakatifu huangalia muhusika anaanza lini kazi yake ya utumishi ile aliyoitiwa na kupamgiwa na Bwana, na wala haitilii maanani kuhusu simulizi za kina za maisha yao ya awali, hasa yale ya ujana wao. Yenyewe huangalia aina ya huduma, na muhusika ameitwa na Bwana kufanya nini, na kwa wakati gani, na nini ni matokeo ya kile alichoitiwa kwa wahusika waliokusudiwa.
Kwahiyo utakubaliana na mimi kwamba yesu ameanza kuwa masihi(Kristo) Baada ga kufikisha Miaka 30 na miaka mingine yoyote ya nyuma alikuwa kama mwanadamu mwingine...?
 
Yesu aliianza rasmi kazi ikiomleta Duniani akiwa na miaka 30. Maandiko katika bible ni muongozo wa Mungu mwenyewe. Wahusika hawakulazimika kuandika taatifa kipinndi hiko. Utotoni pia ukifuatilia haikuelezewa sana kwa sababu hiyo hiyo. Kilichoelezwa utotoni ni kuonyesha ujio wake na utofauti wake. Baada ya hapo ni ripoti ya kazi.
ok Sawa kwahyo Yesu alikuwa Anointed "Masihi" ama kristo sio kwa kuzaliwa bali kwa kuteuliwa na Bwana kipindi cha kuanzia miaka 30 ya uhai wake...kama sijakunote vibaya...
 
Kipindi hicho Yesu alikuwa mafunzoni. Unakumbuka wale Mamajusi, waliropoka kwa mfalme Herode kwamba Mfalme amezaliwa. Na ndio hao waliomuonya Yusufu kuwa mtoto yesu hakuwa salama wamtoroshe. Wale mamajusi walikuwa kama kwa nyakati hizi tungewaita ni maprofesa kwani walikuwa wabobezi kwenye elimu ya utabiri na nyota. Tofauti na elimu ya leo ambayo tunasoma ili kushinda vikwazo vya mazingira yanayotizinguka. We study about matters and other living things sorrounding us. Sanasana, tumesoma yanahusu sisi ni nini na ni nani, basi tunasoma juu ya miili yetu, afya zetu na tiba zetu. Elimu ya zamani ili focus zaidi kwenye Roho, Mungu na miujiza (Spirityal knowledge). Walijua uwezo wa Roho ya mtoto Yesu ambayo kama angezaliwa kwao angelikuwa automatic ni kiongozi wao. Kwahiyo walipomwambia Herode kuwa Yesu ni Mfalme hawakukosea. Ila walijua pia lazima Yesu abatizwe( should be initiated) iliajue namna ya kuamsha utukufu aliokuwa nao autumie kuwaonyesha wengine namna kushinda kifo au awaongoze katika ya uzima wa milele. Kwa kuwa walimletea zawadi nyingi mtoto Yesu zikiwemo zile walizopewa na Herode kama mtego wa kumjua mtoto kazaliwa wapi. Wakawashauri Yusufu na mkewe, kwanza waliwafamisha wazazi kwamba mtoto waliomzaa sio wa kawaida na yuko hatarini. Pili kwa zile zawadi Yusufu na mkwewe wanauwezo wa kufanya maisha popote hivyo wamtoroshe mtoto. Lakini pia mtoto Yesu ni lazima akifika umri wa kujifunza basi wakabidhiwe wao jukumu la kumfundisha. Yesu alipofika umri wa miaka 13 na hasa siku alipowapotea wazazi wake wakitoka kusali Jerusalemu, wazazi walimtafuta wakamkuta yuko Sinagogini yuko katika ubishi mkubwa na Rabai(waalimu wa dini ya kiyahudi) wazazi walipomuuliza kwanini alikuwa pale aliwashangaa kwanini wanamtafuka wakati yeye yuko kwenye nyumba ya baba yake. Hilo liliwafanya wazazi wake kukumbuka ushauri wa wale Mamajusi. Yesu akapelekwa mashariki ya mbali kwa masomo kwenye chuo walichokuwa wanafundisha wale Mamajusi (wakufunzi wa utabiri). Elimu ilihusu Roho na Mungu msomi alipembua kwa wenzie kwa kuonyesha level ya juu kiroho(high level of spirual awareness) nguvu za miujiza (spiritual power he has) kumbuka hii sio kwa wakati wa Yesu tuu, ilikuwepo hawakati wa ushindani wa Filauni na Musa. Ili kuwakomboa wana wa Israel Musa alifanya miujiza mbele ya Filauni ambae nae aliamrisha washauri wake kushindana na Musa kimiujiza. Yesu kabla hajarudi alishatambua uhusiano wake na Mungu alipita vyuo mbalimbali kutoa mihadhala kwa Mungu ni nami na anaweza fikiwaje. Mihadhala ya mwisho aliitoa Ugiriki, watu wa mataifa mbalimbali na Wagiriki walimuusudu sana. Ndio maana mwishoni mwa maisha yake Wagiriki wamfuata Yesu Israel na hata maandishi ya kwanza kuhusu maisha ya Yesu yaliandikwa na Wagiri kwa Lugha yao. Ni kweli kuna maandiko kwenye biblia yamefichwa lakini kwenye tempo nyingi mashariki ya kati kuna simulizi za Yesu Mnazaleti. Mafundisho ya Yesu hayafanani na mafundisho ya dini kwa sasa. Mafundisho ya sasa yako kinadhalia wakati yeye alifundisha kwa vitendo. Mfano alitaka watu wamuabudu Mungu kwa njia ya Roho na Kweli. Yesu aliwabatiza wanafunzi wake kwa Roho, nao waliona maono kiroho na kutafukuli kivitendo vya Dunia. Mfano Mt.Yohana katoka visiwa vya Patmo alikuwa Rohoni maono ya Rohoni ameyaandika katika Ufunuo. Yesu alisema iliuuone ufalme wa Mungu ni lazima Uzaliwe mara ya pili. Kwanza, uzaliwe kimwili kwa Baba na Mama yako, lakini pili uzaliwe Kiroho katika Roho. Muulize Askofu au Papa kama wanajua namna ya kumbatiza mtu Kiroho hawezi. Jee hii njia ya Uzima wa Milele ikoje, inatembewaje? Hakuna mtu atakupa jibu. Ni kweli mafundisho yake yamefichwa kwani watu waliona namna ya kutengeneza fulsa. Kwenye kitabu kimoja nilisoma kuwa Yesu akitabiri juu ufichaji wa mafundisho yake, alisema na kuwaambia wanafunzi wake kuwa Mafalisayo watafanya njama ya kuficha mafundisho yangu ili watu wasijue namna ya kuingia Ufalmeni, lakini watakuta hata wao wamejifichia washindwe kuingia pia.

Kwa hiyo ni kweli biblia haonyeshi kipindi cha miaka 18 Yesu akikuwa wapi. Pia haonyeshi kama alikuwa ameoa alipata watoto. Kwa mila za Kiyahudi Yesu alipaswa kuwa na Mke. Ila nachofahamu hakuozwa na wazazi wake mila zinavyotaka. Ila akuwa na mke nae ni yule mwanafunzi wake Mary Magdalane ambaye licha ya kwamba wanafunzi wote walimkimbia Mary na Mama yake Yesu nae akiitwa Mary walikuwa na Yesu mwanzo mpaka mwisho wa mateso na kifo lakini ndie alishiriki mazishi na ndie aliyetokewa na Yesu na kupewa maagizo ya kutaka wanafunzi kuendeleza mafunzo. Inathibitisha kwenye kitabu chake ambacho hakipi kwenye Biblia. "Kwenye mkutano wa kwanza baada ya kuwakusanya wanafunzi, akasimama Peter akasema, Dada yetu Mary sisi sote twajua wewe ulikuwa kipenzi cha Masihi na mtu wa karibu jee ni kitu gani unakijua ambacho Masihi hakuwahi kutufindishe ile wewe alikufundisha. Ndio vingi tuu, Mary alijibu na akasema ...." Kwenye kitabu Mary alitiririsha nondo za kiroho mpaka Luka akaona wizu ikaleta sintofahamu.

Nasema Yesu hakuozwa bali alijitwalia mke kwanini? Yesu alitengua mila na Desturi nyingi za Kiyahudi, ndio maana alitengwa na alioigwa hakurusiwa kusiriki ibada kwenye masinagogi.

Wayahudi walijiona ni watu bora na wateule wa Mungu hivyo waliwabagua wasio Wayahudi hasa wa Israel wanzao wasio amini katika Uyahudi wale wakiitwa Wasamaria. Yesu hakuwatenga, na hata Mary alikuwa Msamaria( yule mwanamke aliyekutananae kisimani) soma Yohana 4:1-24.

Yesu akimwita Mungu kuwa ni Baba yake, wakati kiyahudi ni kufulu "Usilitaje bure Jina...." hasa wakijua amezaliwa na Maria, waliona anamtukana Mungu kwamba anamaana Mungu alizini na Maria. Wakati wao wanajua alikuwa mtoto wa fundi seremala.

Wayahudi walikuwa na mfume dume, walikuwa watengani na wanawake wale huwezi ukafanya maongezi na mwanamke, labda awe Dada, mama au shangazi. Ndoa zilipangwa na wazazi. Yeye marafiki wengi na hata wanafunzi wake walikuwa ni mchanganiko, wanawake, wanaume, wayahudi, wasamaria na mataifa mengine.

Yesu hakuheshi Sabato siku ambayo hakupaswa kufanya kazi yeye alifanya matendo ya Uponyaji.

Yesu hakuamini kwa haki ya kilipana visasi, jino kwa jino, jicho kwa jicho.

Alimuokoa mwanamke mzinifu ambaye kwa mila na desturi alipaswa kupigwa mawe hadi afe.

Wayahudi waliani kwenye extended family value, family always stay together, Yesu aliikana familia yake hadhalani.

Kwa uvunjifuu Yesu hakuozwa kama angeozwa basi ilikuwa ni jukumu la Yusufu na Maria mke. Yeye akuwa na Mary Magdalane mwanamke msamaria waliekutana nae kisimani, kwenye Biblia imeandikwa wanafunzi wake walipo rudi na kumkuta akiongea Mwanamke walishituka.

Uvunjifuu huu wa mila na desturi ndio zilizo mpelekea kupata wafuasi wengi ambao badala ya kwenda kusali masinagogini ambako wangeleka zaka madhehabuni na kuwa ipato cha Makuhani watu waliamua walimfuata Yesu alipo na kusikiliza mafundisho yake.

Pia watu walishawishika kumfuata Yesu kwa tatuzi za kisheria na matatizo ya kijamii. Watu hakwenda kwenye baraza Mafalisayo, hivyo kupelekea upungufu wa kipato cha Mafalisayo.

Makuhani na Mafalisayo baada ya kuona mapinduzi ya yesu katika jamii, na hasa kuwekwa bila kazi na kunyimwa kipato wakajenga chuki dhidi ya Yesu na kumlianjama ya kubambikia keshi ya Uhaini kwa Pirato.

******** Mwisho ******
Perfect Comments ever 👍👍👍 Nidai Soda
 
Msidanganywe Wala msidanganyike.

1. Yesu Alikuwa kama Binadamu yoyote wa KAWAIDA.
Alipotea mbele ya Baba yake na Mama yake wakiwa sokoni
Akaja kuonekana akiwa kwenye Nyumba ya Baba kanisa.

Hata alipofanya Muujiza kana alimwambia mamayake kuwa wakati wake Bado haujafika

2. Yesu aliendelea kukua zaidi na zaidi Katika hekima na kimo akimpendeza Mungu na wanadamu. Luke 2 52.

Aliendelea kumsaidia baba yake Katika kazi za uselemala, kuchonga mbao, ufugaji nk.
Rejea Amepataje kujua kusoma huyo mtoto wa Selemala.

3. Alianza kuifanya kazi ylaliyotumwa na Baba yake akiwa na Umri wa MIAKA 30-33.

TAFADHALI SANA MSIPOTOSHE UKWELI.

Mkuuu yesu kaingia kanisani??! Bibilia gani inasema ivyo
 
Back
Top Bottom