Miaka 20 plus unamuonesha nani? na ili iweje? ujinga ujinga tu

Miaka 20 plus unamuonesha nani? na ili iweje? ujinga ujinga tu

Fashion zingine zinawafanya watu kama vichaa.
Fashion zinawatesa watu.

weird-male-fashion-model-from-r-wtf-v0-bL3-qN_5GZea04x0geYPRLyi_14EVLDrXoVoGFBdQu4.jpg
 
hapana mkuu.
Unajua mpaka makanisan wadada wanakuja wamevaa gaun linalo mchora shepu na trako.
mpaka chupi ilipoishia unaiona kabsa ile mikanda.

Sasa upo zako unakemea kwa jina la yesu mala mbele yako unaona mikanda ya chupi, si atakutoa kweny uwepo wa Mungu
Wakiambiwa wanakuwa wakali ila huo ndo ukweli
 
Kuna jambo ambalo binafsi huwa linanikera sana; kuona mtu amevaa nguo lakini nguo za ndani zinaonekana wazi. Kwa upande wa wanawake, wengine huvaa nguo nyepesi au zinazobana kiasi kwamba chupi inaonekana kwa urahisi, naye anaona yupo sawa tu, na unakuta anakaa kwao anatoka mpaka ndugu zake wanamwona wala hajili au hata aibu halioni zamani huwezi kuta mama zetu wanavaa kama hivi vibinti vya 2004 huwezi kuta huu ujinga sijui wameutoa wapi.

Kwa upande wa wanaume, kuna wanaovaa suruali zilizoshuka hadi boxer kuonekana wazi wakiamini ni fasheni au mtindo wa kisasa. Boxer chenyewe sasa unakuta kichafu ops yaani kina rangi mbili wendawazimu tu unamwonyesha nani na ili iwaje nonsense.

Je, hii ni ishara ya kujiamini na kufuata mitindo ya mavazi ya sasa, au ni tabia inayopunguza heshima na staha katika jamii? Kwa maoni yenu, kuna tofauti kati ya fasheni na kuvaa kwa namna inayovutia umakini usio wa lazima?

Ningependa kusikia maoni yenu:

Kwa nini watu hufanya hivyo?

Je, mnadhani ni fasheni au kutafuta attention?

Kwenu ni jambo la kawaida au linawakera pia?
Mimi nilivyokua mkubwa nimekuja kugundua ! Mac Muga , Yahaya na Malebo hawakua na shida yeyote ila ni shida ilikua kwa watu wanaopenda kufuatilia mambo ya watu. Miaka 20+ kukerwa na mitindo ya maisha ya watu ni tatizo pia.
 
Back
Top Bottom