Niliwahi kwenda Ubungo stand by then kumpokea mgeni wangu toka JF
Kilichotokea huwa kinanichekesha mpaka leo
Akiwa yuko ubungo mataa akaporwa simu bahati nzuri nilikuwa nimeshamwambia nilivyovaa
Gari inaingia stand kati ya abiria 5 was kwanza kushuka nikamuona mmoja ananikimbilia
Basi nikampa pole ya safari nikabeba begi lake dogo mpaka kwenye gari tukasogea mpaka mgahawa mmoja ndani ya stand unaitwa Salamander
Sasa tunaanza kupiga story kuna mahali tukawa tunaachana..
Kwamfano Aliomba sehemu ya kuchaji simu, lakini akiwa kwenye basi alisema simu take iko full charge
Kwenye mavazi akadai aidha nimemdanganya au sijui rangi.. Nikabaki kushangaa
Baada ya dakika kadhaa simu yake ikaita .. Kumbe mtu wake alimpokea mtu watu na kinyume chake😂😂😂