Miaka 22 ya TICTS nchini yafika mwisho, mamlaka ya bandari kutosaini mkataba mpya

Unaweza kukuta hao wahindi ni ticts wamekuja kivingine. Chezea wahuni utakoma tu. Mi nilifikiri bandari wangeendesha wenyewe kwanza kwani unaweza kuta tunapoteza fedha tu kuwapa watu ulaji.
 
Nawahakikishia tutawakumbuka sanasana TITCS tuliowaondoa kwa sababu binafsi!
Tutarajie;
1.migogoro ya mara kwa mara kati ya staff na wahindi hao (malipo haba)
2. migogoro ya shippers, S/Agents, CFA na watoa huduma nyingine bandarini.
 
Dah yaaani wamekosa kampuni ya kuzipa hadi kuwapa wahindi, sijaona wahindi wakifanya vyema kwenye kutumia teknolojia mpya sisi tuna matatizo
Ila ni nchi ya 5 duniani kwa Uchumi na imempita Uingereza kwa mbali sasa
Wana uwezo na sio wa kuwabeza
 
Jamani jamani jamaniiiiii!!! Mambo yale yale ya TRC na RITES ya India! Yaani kweli hawa wahindi!!
Awekwe nani maana nyie wazawa
Hamuwezi jambo lolote,zaidi ya kuiba,ufanisi wa kazi zero
Acha wahindi waje wawafundisheni kazi

Ova
 
Serikali kumejaa MAZUZU halafu ndio DECISION MAKERS.

Huwa wanakurupuka tu halafu wanakuja kujua HAWANA uwezo.

Kuna siku siasa zilianzia Bungeni, kuwa Kuna kampuni inayoweka vinasaba kwenye Mafuta ni ya kifisadi, mara inafanya kazi zinazoweza kufanywa na TBS.

Mara hiyo kampuni ikapigwa chini, kazi wakapewa TBS halafu hawajui chochote Wala pa kuanzia.

Ikabidi Sasa, wachukue Manpower ile ile iliyokuwa inafanya kazi na hiyo kampuni ndio inafanya kazi na TBS.
 
Nchi za Malawi, Rwanda, Burundi, Congo RD na Zambia pia wapewe na kuendesha magati yao maalum katika bandari ya Dar es Salaam ili kuvutia mizigo na meli nyingi bandarini Dar es Salaam
 
Maono ya shughuli za bandari ya Dar es Salaam Tanzania kama mradi wa kimkakati katika eneo hili la Afrika ya Mashariki, Kusini mwa Afrika na eneo la Maziwa Makuu:

Soma hapa chini:
 

Duu wale TICS walitupuna sana, lakini.
 
Kwamba mmebinafsisha bandari!!!

Yajayo yanafurasha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…