-Serikali/TPA ilipaswa kuandaa vijana wetu wa kitanzania ambao wamehitimu kwenye vyuo vya mbalimbali na hawana ajira miaka 10 iliyopita,
-Vijana wangepewa mafunzo ya manejimenti na uongozi au utawala wa masuala ya bandari.
-Vijana hawa wangekuwa attached kwenye bandari mbalimbali kubwa huko duniani kupata uzoefu kuhusu masuala ya management na uhandisi wa mitambo ya bandari.
-Ninashauri, Serikali au TPA,ingechukua mkopo kutoka taasisi za fedha za nje au ndani kwa ajili ya uwekezaji/kununua vitendea kazi vya kisasa na kutoa mafunzo kwa watumishi,jinsi ya kuvitumia vifaa hivyo.
-Faida ya Uwekezaji huo,ni kuondoa au kupunguza changamoto ya ajira kwa wahitimu wetu, Serikali au TPA kuongeza ukusanyaji wa mapato ya kulipa mkopo, watumishi,na Pato kubwa kwa Serikali.
-Hiyo Kampuni ya India,italeta wahindi kwenye Management,wa kusimamia interest zao/ watanzania wenzetu kitwana,
- Ni nadra kampuni ya India kuwekeza kwenye miundo mbinu,kama watawekeza wataleta mitambo iliyotumika kwenye bandari zao za nje.
-Tanzania itakuwa dumping place,tuliona mkataba na kampuni ya India ya RITES na TRC walileta mabehewa yaliyotumika na mtaji waliupata hapahapa Tanzania,it was a shame and this is going to recur,if the Government is not going to be Keen.
-Kama Serikali/TPA itasisitiza kuendelea na mpango wa kukodisha and kwenye kampuni ya India,tahadhari zichukuliwe kwenye vipengere vya mkataba, suala la uwekezaji miundo mbinu iliyotumika lipigwe marufuku na masuala yote yatakayo ahidiwa kwenye mkataba yatekelezwe kwa muda mwafaka.
-Mwekezaji atatumia mkataba huo kama collateral kukopa fedha kwenye mabenki yetu au mabenki ya India.
-Mkataba wa ukodishaji wa Berths hizo 4-11 upitiwe na bunge letu kwa niaba ya wananchi,tumechoka kupigwa na watanzania wenzetu ambao hawana uzalendo na huruma kwa watanzania wenzao.
-Serikali inakwama wapi, hatuna watalaam au tamaa za watu binafsi.
Sent from my TECNO KC8 using
JamiiForums mobile app