Miaka 22 ya TICTS nchini yafika mwisho, mamlaka ya bandari kutosaini mkataba mpya

Jesus Jesus Jesus… kuna nn TPA? Yaani TPA wanashindwa ku run hii bandari kweli? Tushapigwa tena na tena, Indians sio kabisa aisee, TPA nilijua walisema watafanya kazi hiyo kwa ufanisi wao wenyewe, kumbe wanaleta TICTS nyingine tena mhindi? Jamani jamani, kuna nn? TPA kweli hamna uwezo kiwango hicho? 😭😭😭😭😭😭
 



Yaani inashangaza sana aisee duuh!
 
Hii bandari kwani haiwezi kuendeshwa na Watanzania?
Kinachomshinda hapo mtu kama Roast, Mo, au Bakhresa ni kitu gani hapo?

Imenibidi niwafikirie hawa kwanza, ili kuondoa wasiwasi wako katika mambo tunayopishana, kwa sababu ni bora ya hawa kuliko hao wahindi.

Binafsi ningeuliza inakuwaje, miaka zaidi ya 20 ya TICTS, TPA haikuweza kamwe kujiandaa kuwa na uwezo wa kuendesha hiyo sehemu kwa ufanisi.
Sasa haya ndiyo tuyaite maendeleo ya nchi baada ya uhuru? Tunahitaji miaka mingapi zaidi ili tujijengee uwezo wa kuendesha shughuli zetu vizuri?
 
Hapo Kuna cheni ya miongozo mkuu, Saazingine unaweza kumlaumu mkurugenzi bure kumbe miongozo mefanya kazi.

Hii nchi kunawatu wanaamua kwa maslahi yao tu na hawajali chochote.
Huyo anjua wazi Mkurugenzi hana hili wala lile juu ya jambo hilo.
Hakumbuki aliko sasa Erick Hamis?

Watu wanapenda sana kujisahaulisha mambo, sijui kwa faida gani?
 
Nchi za Malawi, Rwanda, Burundi, Congo RD na Zambia pia wapewe na kuendesha magati yao maalum katika bandari ya Dar es Salaam ili kuvutia mizigo na meli nyingi bandarini Dar es Salaam
Kiukweli, hili siyo wazo la kubezwa hata kidogo.

Hata kama ni wazo la kujenga bandari zao wenyewe, nje ya Dar es Salaam.

Swali ni: Why Not?

Kwa vile tu halifanyiki kwingine kokote duniani?
 
Yani bora hata angepewa mzee bakhressa ataajiri watanzania na uwekezaji utabaki hapa hapa kuliko kuwapa hao wahindi . Mbona kwenye sukari amefanya vizuri kiwanda cha bagamoyo
 
Kiukweli, hili siyo wazo la kubezwa hata kidogo.

Hata kama ni wazo la kujenga bandari zao wenyewe, nje ya Dar es Salaam.

Swali ni: Why Not?

Kwa vile tu halifanyiki kwingine kokote duniani?

Linafanyika katika nchi nyingi zenye bandari kuingia ktk treaties (mikataba maalum) na zile nchi zisizo na bandari kwa namna hii uhakika wa mzigo na meli upo pia treaties hizo haziingiliwi na nani rais/ waziri mkuu yupo madarakani au mabadiliko ya viongozi wa kisiasa.

Ni sisi tu nchi za kiafrika tunaendekeza uzalendo uchwara kuwa na choyo huyu fursa hiyo ya biashara ikiwa haitumiki.

 
CCM washatuua kilichobaki watutafune tu.hivi kijani mbona ni rangi ya neema ccm wamelaaniwa na nani? Nafuu wangemwacha tu kalamagi aendelee kula
 
Za kiafrika zimejaa mazuzu ila hawa wetu ni mazunda
 
Msaada kidogo; Hivi bandari haiwezi jisimamia kuanzia sasa mbona kama mifumo mingi imeboreshwa? Bora kuajiri wazungu wachache watakaowafundisha wenyeji kazi za msingi zinazofanywa na hizo kampuni za kiwakala Ili Kwa maisha ya baadae tuhakikishe Senti zote zinabaki hapa nyumbani
 
Kiukweli, hili siyo wazo la kubezwa hata kidogo.

Hata kama ni wazo la kujenga bandari zao wenyewe, nje ya Dar es Salaam.

Swali ni: Why Not?

Kwa vile tu halifanyiki kwingine kokote duniani?
Zambia wana yard yao inaitwa ZamCargo

Malawi pia wanayo inaitwa Malawi Cargo, ila kama tunavyolalamikia wa kwetu, na wao wameshindwa kuzitumia ipasavyo. Yamebaki magofu....

Ngozi nyeusi ndivyo tulivyo
 
Inawezekana kuna tofauti na hilo la "Transit" kama ulivyolizungumzia hapo; na jinsi mimi nilivyokuelewa mwanzo.

Hii "transit treaty', bado hao majirani wataitegemea TPA na uozo wake hadi mizigo yao ifikishwe kwenye vituo vyao.

Mimi nilidhani wazo lako ni la kuwaruhusu hawa majirani, pengine kuwa na ghati zao maalum kwenye hiyo hiyo bandari inayoshughulikia mizigo yao na kuimiliki na kuiendesa sehemu hiyo, mbali kabisa na kuingiliwa na mamlaka ya TPA.

Na kama hilo haliwezekani kutokana na ufinyu wa bandari, basi tukubaliane kuwekeana mikataba, wajenge bandari zao wenyewe ambazo meli zitakuwa zikishusha mizigo hapo, na wao wakiwa ni wamiliki wa maeneo hayo na kuyaendesha wenyewe kwa ufanisi wanaoona wanao; kuliko kuendelea kuwategemea TPA.

Ninaelewa kuna maswala mengi yanayoweza kuzuia hili, lakini nadhani panaweza kuwa na majadiliano kuyatatua maswala hayo na kuyaweka kwenye mikataba ya makubaliano awali ya yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…