round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 345
- 1,145
Wahitimu wa degree wanaopitia changamoto za kiuchumi hupata msongo wa mawazo kwa sababu jamii huwa na matarajio makubwa kwao. Jamii huamini wanapaswa kuwa wajanja zaidi kwenye fursa hata wasipopata ajira. jamii huwashusha thamani na hata kuwatania vijana hawa inapoona kuna vijana wenye elimu ya chini wana mafanikio darasa la saba, form 4, au diploma, ni jambo linaloleta stress sana kwa wahitimu.
Baadhi ya marafiki zake ambao alisoma nao wanamiliki nyumba , magari, wameoa na wana watoto ambao wanawasomesha shule za maana.
akijiangalia kila dili analofuatilia halijatiki, CV amepeleka sehem nyingi lakini kwingine hata majibu hawampi kwamba amepata au amekosa
idadi ya marafiki zake inaanza kupungua. Hawajamtenga, ila anaona bora ajitenge asijipe stress na mada zao za raha wakat yeye hana hata mia.