Miaka 25 - 35 ndio umri mgumu zaidi kwa vijana wahitimu wa degree, Presha ya kupata mafanikio au kuwa mtu wa level fulani inakuwa ni kubwa mno

Miaka 25 - 35 ndio umri mgumu zaidi kwa vijana wahitimu wa degree, Presha ya kupata mafanikio au kuwa mtu wa level fulani inakuwa ni kubwa mno

Wadarasa la saba wengi mafanikio yao ni ya ujanja ujanja, ndumba, ujangili na masharti kibao... Hawapo tayari kuona watoto wao wanapita walikopita wao
Nakupinga, kuna darasa la saba wengi tu wana biashara zao halali kabisa kuanzia kilimo, bajaji, maduka, n.k. ishu ni ku scale up, kama duka moja linaingiza faida elf 50 kila siku unaweza kuwa na maduka matatu, manne, hadi kumi.

waarabu wengi wameishia darasa la saba wanapiga mishe hakuna maswali ila mbongo akiishia la saba tayari zinaanza story ni jangili.

Sikatai darasa la saba wapo wanaopiga mishe za kijanja ila hata degree wapo wengi tu wanapiga hizo mishe, fuatilia story ya Patrick Ngowi.
 
Maisha kama vidole 🤔cha ajabu darasa la saba wenye fedha nyingi nao wanawapeleka shule za gharama watoto wao ili wasome pia degree tulizosoma sisi
Hii sasa inaitwa mbwa kala mbwa.dah maisha haya 😂😂
 
Wadarasa la saba wengi mafanikio yao ni ya ujanja ujanja, ndumba, ujangili na masharti kibao... Hawapo tayari kuona watoto wao wanapita walikopita wao
Plus umafia mafia. Nimekaa maeneo ya border. Nimeshuhudia hili
 
Ni kweli, na pia huwa tunakuwa wajuaji mno. Na nadhani ndo tumejaa humu tukitoa maelekezo ya namna ya kuishi, usioe hivi, usile vile, usivae hivi, huku drs la saba na form4 failure wakipiga kazi.
 
Maisha wanasema hayana formula. Lakini kwa silimia zaidi ya 70 naweza kusema elimu ya Tanzania haisaidii kijana kukabiliana na changamoto za maisha. Sana sana ndio inamfanya awe muoga na kutojiamini.

Na hapo ndipo LIKUD anapojipatia pointi

Unatumia zaidi ya Milioni 20 kumsomesha mtoto Mpaka Chuo alafu unashindwa kumpa kianzio
 
Nakupinga, kuna darasa la saba wengi tu wana biashara zao halali kabisa kuanzia kilimo, bajaji, maduka, n.k. ishu ni ku scale up, kama duka moja linaingiza faida elf 50 kila siku unaweza kuwa na maduka matatu, manne, hadi kumi.

waarabu wengi wameishia darasa la saba wanapiga mishe hakuna maswali ila mbongo akiishia la saba tayari zinaanza story ni jangili.

Sikatai darasa la saba wapo wanaopiga mishe za kijanja ila hata degree wapo wengi tu wanapiga hizo mishe, fuatilia story ya Patrick Ngowi.
Hii Tanzania bila ujanja ujanja utaishi tu kama mwalimu
 
Elimu yetu ya Tanzania inatuandaa kuajiriwa na sio kujiajiri kwa iyo Prof Mkenda punguza idadi ya udahili vyuo vikuu elekezeni nguvu vyuo vya kati na ufundi wasomi wapo wengi na kila mwaka wanahitimu,mnajaza watu ambao ata nchi haiwezi kuwaajili mfano walimu huko mnahitaji elfu 13 wanakuja malaki na malaki ,baneni nafasi za kwenda vyuo vikuu muajili waliopo mtaani.
 
Elimu bora upimwa baada ya mwanafunzi kuhitimu alichosomea. Mazingira ya mtaani yanaonyesha uhalisia wa product za vyuo vikuu.

Nowadays the jobs have evolved so much, that the jobs today may not exist or may be automated.

So preparing them for a overall development and problem solving and skills development is must.

Ukisoma World Economic forum 2025 reports, utaona dunia inatukimbia.
 
Back
Top Bottom