Miaka 63 baba mdogo hajawahi kurudi nyumbani

Siwajui ndugu wa upande wa mama,sujawahi hata kuona

mama ni mzaliwa Wa shinyanga,aliolewa na baba miaka ya 1986. Walitengena na family baada ya kuolewa wakahama na mkoa

Tangu 1986 hadi Leo 2020 mama hakuwahi kurudi nyumbani kwao

Natamani sana siku moja niwaone ndugu zangu upande Wa mama angalau hata mmoja tu lakini ilishashindika kabisa

Tafadhali kama kuna msaada mnaweza nisaidia niwapate hata mmoja

Muda mwingine nikikutana na mtu alitokea shinyanya huwa namchulia kama ndugu yangu.
Mama jina lake anaitwa Modesta misalaba, aliolewa kwenye ukoo Wa maganiko
 
Ndugu zako ni ndugu zako tu.
Ni kweli ila kuna ndugu wanapotea kutafuta maisha wakienda sehemu kama alikuwa na jina la asili linabadilishwa anaanza maisha upya...kama alikuwa mhaya akaenda Unyirambani ataitwa jina la utani la kinyiramba (kama vile mvamizi,mkosa makazi,mkosa kwao,mzururaji ila wanamuita kwa kilugha) anazaa huko watoto atawaita majina ambay sio relatives(kinship) yaani ya ukoo...hapo tena inakuwa ngumu kumpata.
 
Ndo maaan nimesema maisha ya utafutaji yana maana pana...n kweli kuna watu wanaenda kutafuta maisha sehemu tofauti kwa sababu tofauti ...na ukuchulia huyo ba mkubwa aliondoka 1957 enzi hata hatupata uhuru...uchawi...ushirikina dhuruma na chuki nje nje .hatuwez jua labda utafutaji tu wa kawaida na maisha kumpiga asiwez rudi ...sisi jirani yetu pia aliondoka kwenda mbeya alimaliza miaka 30 anadai alikuwa mgodini lakn hapati akaanza kulima mahindi anapata ila kipindi hicho akiuza anajikuta nauli haifiki kutoka na bei kuwa chee..alikuja mwishoni mwa miaka ya 2000 hivi na tyr alishapata HIV plus TB.
 
Kuna jamaa alizamia ( wale wa kitambo mnajua hii mambo) tukajua yupo mtoni (Ulaya)..akarudi baada ya miaka 20...kumbe miaka yote hiyo yupo Pwani ya Mombasa....akarudi age imesonga,na maisha yamempiga...
Yani huwa wanapikiga hadi mnasema jamaa walimgeuza ndondocha nini ?
 
Watu wanapigwa tunguli hadi wanasahau kwao.
Wanawake ni shiiida!
Hahahaaa...ila ukienda ugenini kuna akili fulani unasahau nyumban unakuwa kama fala fala flani ...usipoangalia dishi linayumba....na network ikate...manake ukienda ugenini bila hesabu unaweza kujikuta wewe ndo uwe houseboy ..utatumwa hadi condom na wenyeji hata kama ni wadogo
 
IPO siku atarudi sema watafutaji napo wakienda ugenini dish linakata network....Tz hii ni ndogo lakni kutokana na miundombinu ya mawasiliano ndugu yako akipotea kumpata ni shida..Nimesema Tz n ndogo kwa minajili kwamba kuna nchi zinaizid Tz mara 6 lkn kumpata mtu ni rahis...
 
Kaka yangu ambaye ni mzaliwa wa kwanza aliondoka nyumbani tarehe 22/9/1970 akiwa na umri wa miaka 20 akakaa Mwanza mjini kwa muda wa miaka 18 mfululizo bila kurudi nyumbani Geita vijijini. Hata baba alipofariki mwaka 1979 hakuhudhuria mazishi. Tarehe 1/9/1988 ndipo akaja nyumbani kwangu na kuniomba nimpeleke nyumbani. Nikampeleka tarehe 3/9/1988 akuwa na umri wa miaka 38. Hadi leo hajaondoka nyumbani.
 
Hongereni sana
 
Siasa nimeacha rasmi mwaka huu huu!
Jingine?
 
Kama kawaida yenu wasukuma kutotoka hom🤭
 
Ukimwambia aende kwao kusalimu anasemaje sasa? Kwa hiyo Hana hata mawasiliano na nyumbani?
 

Samahani akili za usingiz hizi bado...wewe alikuacha kwa Bibi au?
 
Nna bamdogo wangu tangu miaka ya 1990 hadi leo hajawai kurudi, baba yake kafariki hakuonekana na inasemekana yupo ndani ya jiji la makonda anakula maisha.
Kilichomkimbiza nyumbani miaka hiyo ni kesi ya wizi baada ya vijana mtaani kukamatwa na kuwekwa lock up. Alipowekewa dhamana akatoka ndio akatoroka jumla hadi leo hatujawai muona na kesi ilishaisha lakini bado hataki kujitokeza.
 
Kesi huwa haishi sema maafande ndo walishahama....ila kama ni wizi tu automatic ilishaisha...mtafuteni asije akawa teja huko Dar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…