Katika familia kuna siri nyingi sana ambazo unaweza usizijue na ukadhani aliyeondoka ni mjinga na hajielewi. Familia nyingi duniani ni za kijinga na kipuuzi sana, zimejaa chuki, khusda, mauaji ya kichawi, kuharibiana nyota n.k. wengi huondoka na wasirudi tena na haijaanzia leo ni tangu kuja kwa mwanadamu.....jambo pekee ni kumuamini Mungu pekee na sio hao wazazi, ndugu au rafiki kwani nao hao ni binadamu na wanayo mapungufu yao kibao.
Binafsi naishi Mkoa tofauti na sifikirii si tu kurudi bali hata kupata Mke kutoka eneo hilo maana hilo eneo kwangu ni hatari, kwasasa narudi kwakuwa mmoja wa walionizaa yupo hai na si vinginevyo.
Binadamu ukiwaweka sana kichwani mambo yako hayaendi, utalost, na mbaya zaidi ukisimamia future yao na yako mtalost nyote maana kuna wengine ni masikio ya kufa na umasikini.
Kijana amka na upambane na uache imani kuwa zipo dawa utafanya kumrudisha ndugu aliyepotea home muwe nae, zaidi mutamsema kuwa kala maisha na hakuwajali.... jitahidini mfanye yenu na yake muachieni Mungu kwani uliyeandika huu uzi hauwezi kujua hao unaoita nduguzo ulionao hapo home walimfanyia jambo gani huyo Mzee.. maybe walitaka kumuua, kumuweka msukule, kumharibia kwa namna yoyote ile, jitahidi uwafahamu binadamu.....itakusaidia sana pale watakapokufanyia mambo ya hovyo.
USIMWAMINI HUYO ULIYEKAA NAYE KARIBU YAWEZEKANA ANAKUFICHA UKWELI WA HILI ULILOLIANDIKA HAPA, SIKU UKIJUA UKWELI UTAMCHUKIA NA KUMSIFU SHUJAA ALIEKIMBIA TANGU 1957