Miaka 97 ya Mzee Mwinyi na amani ya moyoni pasipo nongwa na visasi

Pia ni somo la ucha Mungu. Kwamba ukimtegemea Mungu siku zote hataweza kukuacha ukatetereka na kuteseka kiafya.
Haupo sawa hapa Mungu ni wetu sote kwa walio wagonjwa na wazima.
Na ni hapa marais wastaafu waislam wanapokuwa ni waalimu wa uungwana unaoambatana na maisha marefu.
Kuishi maisha marefu ni mapenzi ya Mungu ambayo kila binadamu anatamani ayapate,kusema kuwa Marais wa kiislamu wameishi maisha marefu kuzidi wale wakikristo ukimtoa Mzee wetu Mwinyi ni kutudanganya.

Mzee Kikwete ana miaka 71 bado haijui kesho yake.

Rais samia ana miaka 62 Naye bado haijui kesho yake.

Je unajuaje Kama Rais Samia anaweza kufikia miaka aliyoishi Mkapa[81] au Rais Mstaafu Kikwete akafikisha miaka 77 ya baba wa Taifa.Bado ni fumbo.

Maisha ya binadamu kwa yeyote yule ni fumbo Lissu alipigwa risasi zaidi ya kumi yupo hai lakini Magufuli hayupo hayo ni mapenzi ya Mungu sitaki kukufuru.
[
Miaka 27 ya kuishi kama mstaafu ni mingi, wengi wakijitahidi sana wataishi miaka mitano au kumi na kuaga dunia.
Mwalimu aliishi miaka 14 baada ya kustaafu kwake while Mkapa 15 bado ni miaka Mingi tu kwao.
Kheri ya kuzaliwa Mzee Ali Hassan Mwinyi
Nami namtakia heri ya kuzaliwa mzee wetu.
 

Tupe mfumo wako sahihi. Au ndio huu unaopigania wa SSH.

Pamoja na mapungufu yao. Nyerere, JPM walijali maslahi ya wengi. Walisimama na kusimamia maslahi ya wananchi maskini.
 
Hata hawa wengine, kama si dhuluma za mtu yule, wangekuwepo hadi leo.
 
Kama hutojali unaweza kutufafanulia para ya tatu?
" Mrema alipambana.............kui- challenge CCM"

Sera yake ilikuwa kila kitu rukhsa. Unaruhusiwa.

Unaruhusìwa kuuza mali zote za serikali, kuuuza kwa washikaji wako kwa bei za sigara moja. kuuza unga mtaaani. Kufanya chochote. Sera hizi ndio zilizoua miundombinu yote muhimu ya kuwasaidia Watz.
 

Mvivu wa kufikiri ni wewe, think deep.
 
Ni muasisi ya kuwaweka watoto,wake,washikaju serikalini. Kuafinya nchi iwe ya hovyo sana.
 
Alijitahidi kadri ya uwezo wake, aliifanya kilichokuwa ndanii ya mipaka ya uwezo.
Point yangu ni kwamba kama mwenzake Mzee Mwinyi alitawala miaka 10 na amestaafu miaka 27 bado anadunda tu, yule mwingine ameshindwa kutoboa hata 6 tu. Maana yake huyo Magu alikuwa na visasi na roho mbaya ndo maana ameshindwa kutoboa hata miaka 70
 
Paragraph ya mwisho sio kweli! Umepuyanga.!
 
Mwinyi ndio Rais ambaye alikuwa anaongoza kwa mawazo ya Nyerere kutokea Butiama.

Alishinikizwa sana ikiwemo hata kuvunja baraza la mawaziri mara mbili kwa oda ya mzee mchonga.

Mwinyi wala hakujali, hata lilipokuja suala la maelekezo ya kuwadili Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wake wa CCM bwana Kolimba bado aliendelea kuwa mtulivu.

Huyu pengine anabakia kuwa Rais ambaye hakutawala kwa matakwa yake, Rais ambaye hakuwa na mamlaka! Lakini hakuwa na chuki wala kinyongo, leo hii ametimiza miaka 97.

Heri ya kuzaliwa kwa mzee Ali Hassan Mwinyi...Mwenyezi Mungu akutunze zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…